Home

Welcome to EWURA

  • jquery slider
1 2 3 4
wowslider.com by WOWSlider.com v8.7

TANGAZO KWA UMMA – Wito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Majisafi na Majitaka Kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Jijini Tanga(“Tanga UWASA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2019/20

Mnamo tarehe 26 Machi 2018, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilipokea ombi kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya jijini Tanga (Tanga UWASA) la kutaka kufanya mabadiliko ya bei za huduma zake za majisafi na majitaka kwa mwaka 2018/19 hadi 2019/20.

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 21 Juni 2018, katika Ukumbi wa CCM MKOA, jijini Tanga kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la Watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA  kabla ya tarehe 29 Juni, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au OFISI YA EWURA KANDA YA KASKAZINI GHOROFA YA PILI, JENGO LA PPF PLAZA, CORRIDOR AREA, ARUSHA, au ofisi za Tanga UWASA zilizo jijini Tanga.

Soma Zaidi:

________________________________________________________________________________

TANGAZO- Mnada wa Samani na Vifaa Mbalimbali vya Ofisi

Wananchi wote mnatangaziwa kwamba Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), itauza kwa njia ya mnada wa hadhara samani na vifaa vingine chakavu vya ofisi katika ofisi za Mamlaka zilizopo jengo la LAPF, Makumbusho, Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 30/6/2018.

Soma Zaidi:Tangazo la Mnada wa Samani na Vifaa mbalimbali vya Ofisi

_______________________________________________________________________________

PUBLIC NOTICE-The Approved Database of Local Suppliers and Service Providers For 2018

Pursuant to Regulation 38(1) of the Petroleum (Local Content) Regulations, 2017, the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) informs the petroleum industry operators, suppliers, service providers and the general public that it has approved the Local Suppliers and Service Providers Database for the year 2018 “LSSP2018” with one hundred seventy (172) local business entities.

The approved list will be eligible to participate in the provision of various goods and services in the petroleum midstream and downstream activities in Mainland Tanzania for the year 2018. Find the attachments for more details

Preamble for LSSP REGISTER FOR 2018

Utangulizi wa Kanzidata ya LSSP2018

LSSP REGISTER 11.06.2018

______________________________________________________________________________

 

TANGAZO KWA UMMA – Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Songea (“Songea WSSA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA) inatoa tangazo kuwa kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 5 Julai, 2018, katika Ukumbi wa Manispaa, Songea Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA k kabla ya tarehe 19 Julai, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au ofisi za Songea WSSA zilizoko mjini Songea. Soma Zaidi:

Tangazo kwa Umma-Mwito wa Maoni ya Wadau kuhusu Maombi ya Marekesho ya  Bei za Maji kutoka  Songea WSSA  kwa Mwaka 2018 – 2021

Public Notice- A Call For Stakeholders’ Views on the Tariff Application from Songea WSSA for Year 2018 – 2021

 

 

___________________________________________________________________________________________

 

TANGAZO KWA UMMA-Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Singida (“Singida WSSA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatoa tangazo kuwa kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 28 Juni, 2018, katika Ukumbi wa Mlade, FDC, Singida Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la Watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA   kabla ya tarehe 6 Julai, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au ofisi za Singida WSSA zilizo mjini Singida. Soma Zaidi:

Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za aji Kutoka Singida WSSA kwa Mwaka 2018 Hadi 2021

A Call for Stakeholders’ Views on the  Tariff Application from Singida WSSA For Year 2018 – 2021

________________________________________________________________________________

Cap Prices For Petroleum Products With Effect From Wednesday 06 June,2018

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) hereby publishes Cap Prices for petroleum products, applicable in Tanzania Mainland. These retail and wholesale prices are applicable effective Wednesday, 6th June 2018

Please see attached for more details:-

Cap Prices With Effect From 06 June 2018-ENGLISH

Cap Prices With Effect From 06 June 2018-KISWAHILI

________________________________________________________________________________

 

TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni ya Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, Mamlaka imepokea maombi ya leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Hivyo basi; Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

Soma Zaidi:TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

________________________________________________________________________________

Regulatory Performance Report on Electricity Sub-sector For the Year Ended 30th June,2017

_____________________________________________________________________________

Downstream Petroleum Sub Sector Performance Review Report For Year 2017

_______________________________________________________________________

TAARIFA KWA UMMA-Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Sikonge (“Sikonge WSSA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Mnamo tarehe 13 Mei 2018 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilipokea maombi yaliyokamilika kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Sikonge (Sikonge WSSA) ya kutaka kuongeza bei ya huduma zake za majisafi kwa mwaka 2018/19 hadi 2020/21.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kuandoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA  ifikapo tarehe 20 Juni 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika ofisi za EWURA MAKAO MAKUU, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF; BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au OFISI ZA MAMLAKA YA MAJI SIKONGE. Soma Zaidi:

Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya MAarekebisho ya Bei za Maji Kutoka Sikonge WSSA kwa Mwaka 2018 Hadi 2021

____________________________________________________________________________

TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Hivyo basi;Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni hapo juu kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwakilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe ya tangazo hili kupitia anwani tajwa hapa chini. Soma Zaidi:TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni ya kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

__________________________________________________________________________

Cap Prices For Petroleum Products With Effect From Wednesday 02 May, 2018

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) hereby publishes Cap Prices for petroleum products, applicable in Tanzania Mainland. These retail and wholesale prices are applicable effective Wednesday, 2nd May 2018

Please see attached for more details:-

Cap Prices With Effect From 02 May 2018-ENGLISH

Cap Prices With Effect From 02 May 2018-KISWAHILI

 

____________________________________________________________________________________________________

TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni ya Kusambaza Umeme kutoka kwa Kampuni ya Mwenga Power Services Limited

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea maombi ya leseni ya kusambaza umeme kutoka kwa Kampuni ya Mwenga Power Services Limited. Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi kuhusiana na maombi haya awasilishe kwa maandishi kabla ya saa 10 jioni, siku  ya tarehe 27 mwezi Aprili, 2018. Maombi ya leseni yanaweza kuonyeshwa kwa mtu kwa maombi maalum ya maandishi. Soma Zaidi:

Maombi ya Leseni ya Kusambaza Umeme kutoka kwa Kampuni ya Mwenga Power Services Limited-Kiswahili

Application for a Provisional Electricity Distribution Licence from Mwenga Power Services Limited-English

_______________________________________________________________________________________

 

TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni kujihusisha na mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Sheria ya Mafuta Na. 21 ya mwaka 2015 inaipa nguvu EWURA, kusimamia shughuli za mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli huku Kifungu cha 131 (1) cha sheria hiyo kinawataka wote wanaojihusisha na sekta tajwa kuwa na leseni iliyotolewa na EWURA. Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Hivyo basi;Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni  kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Soma Zaidi: TAARIFA KWA UMMA-Kuwasilisha pingamizi kwa waombaji wa leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli

____________________________________________________________________________________

PUBLIC NOTICE-Online Applications for Constructional Approvals and Petroleum Licences Starting 05 April,2018

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) would like to inform all applicants of Constructional Approvals and Petroleum Licences that from 5th April, 2018 all applications should be done via online system. Read More:

PUBLIC NOTICE-LOIS -Online Applications for Constructional Approvals and Petroleum Licences 

TAARIFA KWA UMMA-LOIS -Maombi ya leseni na vibali vya ujenzi katika Sekta ndogo ya Mafuta ya Petroli kwa njia ya Mtandao

_________________________________________________________________________

Cap Prices for Petroleum Products With Effect From Wednesday 04 April, 2018

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) hereby publishes Cap Prices for petroleum products, applicable in Tanzania Mainland. These retail and wholesale prices are applicable effective Wednesday 4th April, 2018:- Please see attached for more details.

Cap Prices with Effect From 04 April,2018-English

Cap Prices With Effect From 04 April, 2018-Kiswahili

______________________________________________________

TAARIFA KWA UMMA-Orodha ya mafundi umeme waliopewa leseni na EWURA

EWURA inatangaza majina ya mafundi umeme ambao wamepewa leseni madaraja mbalimbali  kama yalivyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA; na waombaji hawa wanatakiwa kufika EWURA kuchukua leseni zao mara watakapopata taarifa hii.Soma zaidi:TAARIFA KWA UMMA-Orodha ya mafundi umeme waliopewa leseni na EWURA

_____________________________________________________________________________

Sheria na Kanuni za Ushirkishwaji wa Watanzania kwenye EACOP

 Sheria ya Petroli ya mwaka 2015  na Kanuni za Ushirikishwaji wa  Watanzania za mwaka 2017, zimeanisha wajibu wa EWURA katika  miradi mikubwa ya kuvuna rasilimali za asili(kama gesi). Soma Zaidi:Sheria na Kanuni za Ushirkishwaji wa Watanzania kwenye EACOP

______________________________________________________________________________________

Mahojiano na Vyombo vya Habari Kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Kutoka Hoima(UGANDA) hadi Tanga(TANZANIA)

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ni Mradi wa Sekta binafsi na unatekelezwa katika nchi mbili (Uganda na Tanzania). Mradi huo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani 3.55 bilioni na kuleta ajira za kati ya watu 6,000 na 10,000 ndani ya miaka mitatu (3). Mafuta Ghafi ya Hoima (ya aina yake), yatasafirishwa kutoka Uganda kwenda sokoni nchi za nje, kupitia Tanzania.  Mradi wa Bomba umbali wake ni kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.

Soma Zaidi Maelezo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Kutoka Uganda  hadi  Tanga Tanzania (002)

______________________________________________________________________________________