Tangazo kwa Umma -Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Maganzo WSSA

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Ijumaa, tarehe 15 Septemba 2017 katika Ukumbi wa Maganzo BM Conference uliopo mji wa Maganzo kuanzia saa 4:00 asubuhi,  kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali na Baraza la Ushauri la watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla,  kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa. Soma zaidi….Tangazo kwa Umma -Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Maganzo WSSA