TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni kujihusisha na mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Sheria ya Mafuta Na. 21 ya mwaka 2015 inaipa nguvu EWURA, kusimamia shughuli za mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli huku Kifungu cha 131 (1) cha sheria hiyo kinawataka wote wanaojihusisha na sekta tajwa kuwa na leseni iliyotolewa na EWURA. Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Hivyo basi;Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni  kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Soma Zaidi: TAARIFA KWA UMMA-Kuwasilisha pingamizi kwa waombaji wa leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli

____________________________________________________________________________________

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *