TANGAZO KWA UMMA-Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Singida (“Singida WSSA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatoa tangazo kuwa kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 28 Juni, 2018, katika Ukumbi wa Mlade, FDC, Singida Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la Watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA   kabla ya tarehe 6 Julai, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au ofisi za Singida WSSA zilizo mjini Singida. Soma Zaidi:

Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za aji Kutoka Singida WSSA kwa Mwaka 2018 Hadi 2021

A Call for Stakeholders’ Views on the  Tariff Application from Singida WSSA For Year 2018 – 2021

________________________________________________________________________________

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *