TANGAZO KWA UMMA – Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Songea (“Songea WSSA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA) inatoa tangazo kuwa kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 5 Julai, 2018, katika Ukumbi wa Manispaa, Songea Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA k kabla ya tarehe 19 Julai, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au ofisi za Songea WSSA zilizoko mjini Songea. Soma Zaidi:

Tangazo kwa Umma-Mwito wa Maoni ya Wadau kuhusu Maombi ya Marekesho ya  Bei za Maji kutoka  Songea WSSA  kwa Mwaka 2018 – 2021

Public Notice- A Call For Stakeholders’ Views on the Tariff Application from Songea WSSA for Year 2018 – 2021

 

 

___________________________________________________________________________________________

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *