TANGAZO KWA UMMA – Wito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Majisafi na Majitaka Kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Jijini Tanga(“Tanga UWASA”) kwa Mwaka 2018/19 – 2019/20

Mnamo tarehe 26 Machi 2018, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilipokea ombi kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya jijini Tanga (Tanga UWASA) la kutaka kufanya mabadiliko ya bei za huduma zake za majisafi na majitaka kwa mwaka 2018/19 hadi 2019/20.

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 21 Juni 2018, katika Ukumbi wa CCM MKOA, jijini Tanga kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la Watumia Huduma zinazodhibitiwa na EWURA na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

Wadau wanaopenda kutoa maoni kwa maandishi wanaombwa kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA  kabla ya tarehe 29 Juni, 2018. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana Makao Makuu ya EWURA, GHOROFA YA NNE, JENGO LA LAPF, BARABARA YA MAKOLE, DODOMA au OFISI YA EWURA KANDA YA KASKAZINI GHOROFA YA PILI, JENGO LA PPF PLAZA, CORRIDOR AREA, ARUSHA, au ofisi za Tanga UWASA zilizo jijini Tanga.

Soma Zaidi:

________________________________________________________________________________

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *