TAARIFA KWA UMMA-Maombi ya Leseni ya Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatoa taarifa kwa umma kuwa  imepokea  maombi ya leseni ya  kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli kutoka kwa waombaji mbalimbali. Hivyo basi, Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni  kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ndani ya siku ishirini na moja (21) kuanzia tarehe ya tangazo hili. 

Soma Zaidi: Maombi ya Leseni ya Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

_______________________________________________________________________________________

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *