TANGAZO KWA UMMA- Mwito wa Kupata Maoni ya Wadau Kuhusu Mabadiliko ya Kanuni ya Kupanga na Kukokotoa Bei ya Bidhaa za Mafuta ili Kuongeza Kanuni ya Kukokotoa Bei ya Gesi ya Kupikia

EWURA itafanya Mkutano wa Taftishi tarehe 13 Septemba 2018 katika Ofisi za EWURA Kanda ya Mashariki (Ghorofa ya 7, jengo la LAPF, Kitonyama, Dar es Salaam) kuanzia saa tatu na nusu (3.30) asubuhi ili  kukusanya maoni ya wadau kuhusu mabadiliko ya kanuni ya kupanga na kukokotoa bei ya bidhaa za mafuta ili kuingiza kanuni ya  kukokotoa bei ya gesi ya kupikia.

Wadau watakaopenda kupewa muda wa kuwasilisha maoni yao katika mkutano huo wanatakiwa kuonyesha nia yao kwa kuiandikia EWURA ifikapo tarehe 10 Septemba 2018.

Aidha, wadau wanaweza kutoa maoni kwa maandishi kupitia barua pepe info@ewura.go.tz. au kumwandikia barua Kaimu Mkurugenzi Mkuu kabla ya tarehe 14 Septemba,2018. Soma Zaidi:

_________________________________________________________

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *