TANGAZO KWA UMMA-Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji na Usafi wa Mazingira Kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Bukoba (BUKOBA WSSA) Kwa Mwaka 2018/19 – 2020/21

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Ijumaa, tarehe 21 Septemba 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa ELCT uliopo Bukoba Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi. Lengo la mkutano huo ni kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali na Baraza la Ushauri la watumia  Huduma  zinazodhibitiwa na EWURA, wateja wa Mamlaka ya Maji Bukoba na wananchi wote kwa ujumla kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa.

_________________________________________________________________

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *