TANGAZO KWA UMMA: Onyo Kwa Mafundi Umeme

TAARIFA inatolewa kwa mafundi wa umeme na umma kwa ujumla kuwa, ni kosa kisheria kufanya kazi za kuweka mifumo ya umeme (electrical installations) bila kuwa na leseni hai iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

ONYO hili linatolewa kwa mujibu wa Ibara  ya 7 (1) ya Sheria ya EWURA namba 414 na Ibara ya 8 ya Sheria ya Umeme namba 131. Soma Zaidi:-

Onyo-Mafundi Umeme

Warning-Electrical Installation Personnel

_____________________________________________________________________________________________________________

Visits: 6623

134 thoughts on “TANGAZO KWA UMMA: Onyo Kwa Mafundi Umeme

  1. Je tufanyeje sisi tulio na leseni za ufundi umeme ili kupata mhuri na kuweza kupitisha kazi bila kumtegemea kontrakta mwingine asante

    1. Ndugu Manento,
      Cha muhimu zaidi ni kujiendeleza kupata elimu ya ngazi ya juu ili upate daraja la leseni linalokuwezesha kuwa na muhuri.Asante.

        1. Ndugu Masanja,
          Unapaswa kuwa na daraja kuanzia wiremen. Na leseni ya kufanya kazi inapatikana kwa kufanya maombi kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/
          Unpaswa kuwa na vyeti vya elimu ya ufundi vilivyothibitishwa, picha (pasipoti) yenye kivuli cha bluu na wasifu wako (CV); vyote vikiwa katika nakala laini kabla ya kuanza kufanya maombi.
          Kwa maelezo zaidi piga 0800110030 (bure) au tembelea ofisi yetu iliyo karibu nawe katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma,Mbeya na Mwanza.
          Karibu

          1. Je walio kua na shot cose ya umeme wanaweza kupata leseni ili wafanye kazi za umeme na kama awapati wanafanya kazi gan kutokana na walichosomea

  2. Asante kwa semina tumejikumbusha mengi swali langu wale waliomaliza darasa la saba wakajiunga na vyuo vya ufundi mfano trede test ana grade one au two je anapata leseni? Maana kuna ile mtu mpaka awe na cheti cha fomu 4 tusaidie maelezo

        1. Ndugu Samson,
          Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ katika tovuti ya Mamlaka.
          Unapaswa kuwa na
          1. Picha (passport size ) yenye kivuli cha bluu
          2. Vyeti vya elimu ya Ufundi
          3.Wasifu (CV) inayoonesha shughuli za ufungaji umeme ulizofanya.

          Kisha utatumia nakala laini kufanya maombi, kwa kufungua mfumo wa LOIS, kujisajili na kufanya maombi ya leseni.

          Karibu

  3. Je kama kwenye nyumba yangu nime jenga mabanda mawili naweza kutoa umeme kwenye nyumba kubwa kupeleka kwenye mabanda ayo

    1. Ndugu Deus ,

      MADARAJA YA LESENI ZA UMEME YANAYOTOLEWA NA EWURA
      Leseni Daraja A: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa aina zote isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja B: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa kati (33,000V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja C: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa chini (400V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja D: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa njia moja (230V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.
      Leseni Daraja W: inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, C au D.
      Leseni Daraja “S1”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme katika msongo wa umeme wa aina zote.
      Leseni Daraja “S2”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 33,000; na
      Leseni Daraja “S3”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 1,000.
      Karibu

        1. Ndugu Pastory,
          Kwa daraja C, elimu ni (i) shahada (digrii) ya uhandisi wa umeme au mwenye NTA Daraja ya 8
          (ii) NTA Daraja ya 7 au stashahada ya usakinishaji mifumo ya umeme (iii) NTA Daraja ya 6 au stashahada ya masuala ya umeme au oFTC ya uhandisi wa umeme au elimu inayolingana na hiyo ; (iv) NTA Daraja ya 4,NTA Daraja ya 5, au Trade Test Daraja ya I /Ngazi ya III na uzoefu wa miaka miwili katika usanikishaji mifumo ya umeme; au (v) Trade Test Darja ya II /Ngazi ya II au elimu sawia na uzoefu wa miaka mitatu ya usanikishaji mifumo ya umeme.

          Karibu

          1. 1.Nilikuwa nahitaji Zile Gharama za awali baada ya kusubmit Form baada ya kujaza ambazo huwa mteja anatumie namba ya malipo.
            Class C na Class D n shiling Ngap..
            2.Mfano mm nimemaliza chuo 2017 baad yakumaliza Nilipata Level 1 ya Certificat (VC1)
            Nikaingia kazin nikawa nafanya kazi ila sasa mwaka Jana Nmerudia na nmepata VC 2 yaan Level 2 Certificate. Tukija kwenye Sifa za Class C Mojawapo naona Mtu hawe na Level 2 but Awe amefanya kazi miaka Isiopungua Mitatu sasa Cheti cha level 2kinasoma 2021
            Hapa Je Haiwezi kuonekana Kama ubabaishaji.
            Naomba muongozo kwenye Ilo..

          2. Ndugu Shawwal,
            Madaraja ya leseni yanatolewa kwa mujibu wa kanuni zilizopo,hivyo jambo la msingi ni kuandika wasifu wako vizuri ili kubainisha uzoefu ulionao.

            Baada ya kuwasilisha maombi mwombaji atapewa namba ya malipo (Control Number) ambayo atalipia ada isiorejeshwa (non -refundable fees) kama inavyooneshwa hapa chini.
            Aina/daraja la leseni Ada isiyorejeshwa (Shilingi) Ada ya nakala(kopi) ya leseni (Shilingi)
            A, B, S1, S2 130,000 20,000
            C, D, W, S3 50,000 20,000
            Muhimu: Ada isiyorejeshwa inalipwa mara moja kila baada ya miaka mitano, kwa kuwa muda wa kuhuisha leseni ni baada ya miaka mitano.
            Mwombaji anaweza kufuatilia mwenendo wa maombi yake katika mfumo wa LOIS, kwa kutumia jina na nywila yake
            Mamlaka itachakata maombi hayo na mwombaji atajulishwa kwa njia ya barua pepe au ujumbe kwenye simu yake ya mkononi namna ya kuchukua leseni yake
            Karibu

      1. Naomba kujua utofauti wa leseni ya electrical istallation na Leseni ya wireman….Na kama kuna utofaut je leseni ya wireman inapatikana kwa vigezo gan???

        1. Ndugu Dickson,
          Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa LOIS unaopatikana kwenye tovuti ya EWURA. Bofya kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ kujisajili kisha endelea kujaza taarifa zako kwenye mfumo. Unatakiwa kuwa na picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu, cheti cha elimu ya ufundi (kilichothibitishwa), kitambulisho (KURA, Leseni ya Udereva ama Cha Taifa),na Wasifu wako (CV) katika nakala laini kabla ya kufanya maombi kwenye mfumo.

          Karibu

    2. Najiamini nanina uwezo mkubwa wakufanya way ring
      ninahitaji kujazia yale nisiyo yajua nakupata leseni je nifanye nini? nipo babati manyara

      1. Tafadhali unasahuriwa kwenda VETA kuomba kufanyia tathmini ya ujuzi na uwezo wako wa ufundi umeme, kisha watakupa barua au cheti cha utambuzi na utakitumia kuomba keseni EWURA.
        Karibu

    1. Ndugu Peter Mbando,
      Endapo uliomba leseni mwezi Machi, unapaswa uwe umeshapata leseni yako. Endapo sivyo tunakushauri kutembelea ofisi yetu iliyo karibu nawe katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya au piga simu BURE 0800110030 siku na muda wa kazi kwa ufuatiliaji zaidi.
      Karibu

    1. Habari Majaliwa,
      Zipo fursa ambazo hutangazwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kurasimisha ujuzi. Tunakusahuri kufuatilia matangazo hayo au kutembelea Ofisi ya Waziri Mkuu(sekta ya vijana) kupata taarifa zaidi.
      Karibu

    1. Ndugu Majaliwa,
      Unapaswa kwenda chuo cha ufundi kurasimisha ujuzi wako. Wasiliana na VETA ili upate ushauri sahihi.
      Karibu

  4. Mimi nmetuma maombi toka 01/07/2021 kwa maana ndo siku nililipia ile fomu ya maombi ya leseni pengne bado muda kuipata?? Na pia nipo ifakara Sehemu ambapo naweza kuipata kirahisi ni wapi au mnatuma maeneo tulipo??

    1. Ndugu Gadiel,
      Utataarifiwa leseni itakapokuwa tayari kupitia barua pepe yako uliyotumia kuomba leseni ili uweze kulipia leseni kulingana na daraja utakalopata. Na lesni yako itakapokamilika utapigiwa simu ili ukaichukue. Kama uliomba ukiwa Ifakara, utapaswa kuchukua leseni yako Dar es Salaam.
      Karibu

      1. Naomba Kama mtaona inafaa nikichukulie dodoma lkn maana nitakuwa na safari kwenda dodoma kwahiyo naona dodoma inaweza kuwa rahisi kwangu naomba kuwasilisha

  5. Nimependezwa sana kwa maelezo yenu mazuri ila naomba kujua je mtu aweza kujifunza ufundi wa umeme Short course na akaruhusiwa kufanya wiring majumbani?? Kama hapana je atatakiwa awe na level gani? Ahsante

    1. Ndugu Bashiru,
      Endapo wewe ni fundi,na umesoma kozi fupi chuo cha ufundi kinachotambulika na kupatiwa cheti, unaweza kuomba leseni daraja la chini yaani W.
      Karibu

      1. Naomba kufahamishwa je mimi niliesoma chuo cha ufundi cha serikali miaka miwili kwa kuchukua somo moja tu la electrical installation na kupewa cheti cha chuo nilipoitimu masomo yangu je nastaili daraja gani la leseni? Naomba kuwasilisha

        1. Ndugu Johanes,
          Utakapofanya maombi ya leseni uchambuzi utafanyika kulingana na elimu na uzoefu wa kazi, kisha utapewa leseni kwa daraja linalostahili.
          Vigezo vya daraja la leseni vimeanishwa hapa chini kwa rejea yako.

          KANUNI ZA UMEME (HUDUMA ZA UFUNGAJI MIFUMO YA UMEME), 2022

          (Imetolewa chini ya kifungu cha 8(3), 33(2) (b) na 45 cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131)

          Kwa mujibu wa Kifungu cha 8(1) (h) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa Kanuni mpya za Umeme (Huduma za Ufungaji Mifumo ya Umeme) za mwaka 2022. Kanuni hizi zilitangazwa kwenye gazeti la Serikali tarehe 4 Machi 2022 kupitia Tangazo la Namba 113 na zinapatikana kwenye tovuti ya EWURA; http://www.ewura.go.tz.Kanuni hizi mpya, zinabatilisha zile za awali “Kanuni za Umeme (Huduma za Ufungaji Mifumo ya Umeme) za 2019”.
          Kanuni hizi ni nyenzo ya udhibiti na usimamizi wa leseni za utoaji wa huduma za ufungaji mifumo ya umeme Tanzania Bara na zinatoa mwongozo kwa mtu yeyote anayehitaji kuomba leseni ya uwekaji umeme kutoka EWURA kwa ajili ya kufanya kazi zozote za ufungaji wa mifumo ya umeme.

          Kanuni zinatoa, pamoja na mambo mengine, utaratibu wa utoaji wa leseni ya ufungaji za umeme kwa waombaji waliokidhi vigezo. Aidha, Kanuni zimeongeza muda wa kuhuishwa leseni hizo kila baada ya miaka mitano badala ya miaka mitatu.

          KWA HIYO, TAARIFA INATOLEWA KWA UMMA KWAMBA:

          (a) madaraja ya leseni yamebaki kuwa yale yale ambayo ni A, B, C, D, W, S1, S2, na S3;
          (b) mwombaji aliyekidhi vigezo atapewa leseni ya ufungaji umeme pekee bila cheti tofauti na ilivyokuwa katika Kanuni za awali;
          (c) leseni zitakazotolewa kwa mfumo wa Kanuni hizi mpya zitaisha muda wake baada ya miaka mitano;
          (d) waombaji watalipa “ada za maombi zisizorejeshwa” badala ya “ada ya maombi na ada ya leseni” kama ilivyokuwa awali;
          (e) Wale wote waliotuma maombi yao ya leseni kabla ya tarehe 4 Machi 2022, watalipa ada za maombi na ada za leseni na muda wa mwisho wa leseni utakuwa ni miaka mitatu;
          (f) “Kiwango cha ada za maombi zisizorejeshwa” zitakuwa kama zilivyo orodheshwa kwenye jedwali namba moja la Kanuni mpya (ambazo zimewekwa kwenye tovuti ya EWURA) na ambapo pia taarifa itapatikana kwenye mfumo wa uombaji wa leseni wa EWURA (LOIS).

          (g) maombi yote ya leseni yataendelea kutumwa kupitia mfumo wa LOIS kwenye Tovuti ya Mamlaka http://www.ewura.go.tz ;
          (h) leseni, inapokaribia kwisha muda wake, mwenye leseni ataomba kwa Mamlaka kuhuisha leseni hiyo miezi miwili kabla ya leseni ya awali kuisha;
          (i) mwenye leseni ambaye atashindwa kuomba kuhuisha leseni miezi sita baadaya ya muda wake kumalizika, atalazimika kuomba leseni mpya.

          Pamoja na hayo, marekebisho madogo madogo yamefanyika kwenye taratibu za maombi ya madaraja ya leseni, uwanda wa shuguli zinazofanyika kwa mujibu wa daraja za leseni, elimu ya ufundi ya umeme na uzoefu unaohitajika kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini;-

          Aina ya Leseni Kazi Zinazohusika Elimu ya Ufundi wa Umeme na Uzoefu Husika Unahitajika
          Daraja A Imetolewa kutekeleza kazi za usakinishaji wa mifumo ya umeme katika viwango vya vyote vya volti isipokuwa kazi zinazoruhusiwa chini ya daraja S1, S2 na S3. (i) Cheti cha Usajili kama Mtaalamu
          Mhandisi wa Umeme wa taaluma husika;
          (ii) Shahada ya uhandisi wa umeme au
          uhandisi wa umeme-mitambo au
          Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au zaidi na miaka mitatu ya uzoefu katika katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme,mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwenye msongo wa juu;
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya juu ya umeme au umeme-mitambo na
          miaka mine ya uzoefu katika kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme, miwili kati ya hiyo,iwe ya ufungaji wa umeme katika msongo wa juu;
          (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 6 au cheti cha ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo na miaka mitano ya uzoefu wa masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, mitatu kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme wa msongo wa juu.
          Daraja B Inatolewa kwa kazi za usakinishaji wa mifumo ya umeme wa kiwango cha volti ya kati hadi volti 33,000 isipokuwa kazi zinazoruhusiwa chini ya darasa S1, S2 na S3. (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme au
          uhandisi wa Umeme-Mitambo au
          Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8, na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufungaji mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo uwe wa ufungaji wa umeme katika msongo wa kati;
          (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 7 au Stashahada ya juu ya Uhandisi wa umeme/Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu husika katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme wa msongo wa kati; na
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au
          Cheti cha ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo na miaka minne ya uzoefu katika masuala ya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme, miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa umeme wa msongo wa kati.
          Daraja C Hutolewa kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme zisizozidi Volti 400 isipokuwa kazi zinazoruhusiwa chini ya darasa la S1, S2 na S3. (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme/umeme-mitambo au Tuzo ya KItaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au inayolingana na Shahada ya Uhandisi wa umeme;
          (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya juu ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo au inayolingana na hiyo;
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Stashahada ya kawaida ya Uhandisi wa Umeme/umeme-mitambo au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi umeme au cheti kinacholingana na hicho
          (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi umeme ngazi ya 4, Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 5, au cheti cha kufuzu Mtihani wa ujuzi wa umeme daraja la I / Ngazi ya III au kinacholingana na hicho na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme; na
          (v) Cheti cha kufuzu cha Mtihani wa ujuzi wa umeme Daraja la II/Kiwango cha II au kinacholingana na hicho na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme.
          Daraja D Imetolewa kutekeleza kazi za ufungaji wa umeme zisizozidi Volti 230 isipokuwa kazi zinazoruhusiwa chini ya darasa la S1, S2 na S3. (i) Cheti cha kufuzu ufungaji wa mfumo wa umeme daraja la I, II, III, au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 4, ngazi ya 5 au cheti kinacholingana; au

          ii) mafunzo ya awali,kozi fupi, kozi za kati, cheti cha juu au cheti kinacholingana na hicho na uzoefu wa miaka mitatu katika kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme.

          Daraja W Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, S1,S2, S3, C au D. Mwombaji wa leseni anapaswa kuwa na mafunzo ya awali/kozi fupi/kozi za kati, au cheti cha juu cha uwekaji wa mifumo ya umeme au sifa nyinginezo kutoka Taasisi nyingine za Kiufundi zinazotambulika.
          Daraja S1 Hutolewa kufanya kazi maalum za ufungaji wa umeme wa volti zote. (i) Cheti cha Usajili kama Mtaalamu
          Mhandisi wa Umeme/umeme-mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalumu wa kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa juu.
          (ii) Shahada ya uhandisi wa umeme au uhandisi wa umeme-mitambo au
          Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au zaidi na miaka minne ya uzoefu katika katika masuala ya kazi maalumu za kufunga mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwenye msongo wa juu;
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya juu ya uhandisi umeme/ umeme-mitambo na
          miaka mitano ya uzoefu katika kazi maalumu za ufungaji wa mifumo ya umeme, mitatu kati ya hiyo,iwe ya ufungaji wa umeme katika msongo wa juu;
          (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 6 au cheti cha ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo na miaka sita ya uzoefu wa masuala ya kazi maalumu za kufunga mifumo ya umeme, minne kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme wa msongo wa juu.
          Daraja S2 Hutolewa kufanya kazi maalum za ufungaji wa umeme hadi volti 33000. (i) Cheti cha Usajili kama Mtaalamu
          Mhandisi wa Umeme/umeme-mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalumu wa kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa kati; au
          (ii) Shahada ya uhandisi wa umeme au
          uhandisi wa umeme-mitambo au
          Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 na miaka mitatu ya uzoefu katika katika masuala ya kazi maalumu za kufunga mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwenye msongo wa kati; au
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 7 au zaidi, au Stashahada ya juu ya uhandisi umeme/ umeme-mitambo na
          miaka minne ya uzoefu katika kazi maalumu za ufungaji wa mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo,iwe ya ufungaji wa umeme katika msongo wa kati;
          Daraja S3 Hutolewa kufanya kazi maalumu za ufungaji wa umeme hadi volti1000. (i) Shahada ya Uhandisi wa Umeme/umeme-mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au Zaidi au inayoingana na shahada ya uhandisi umeme/umeme-mitambo na mwaka mmoja wa uzoefu wa kazi maalumu wa kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa chini;
          (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 7 au stashahada ya juu ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo au inayolingana na hiyo, na miaka miwili ya uzoefu katika katika masuala ya kazi maalumu za kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa chini; au
          (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 6 au Stashahada ya kawaida ya uhandisi umeme/ umeme-mitambo na miaka mitatu ya uzoefu katika kazi maalumu za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa chini.

    1. Ndugu Boniphace,
      Unashauriwa kujiunga na program za uendelezaji taaluma ambazo hutolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, sekta ya vijana. Tafadhali fuatilia matangazo mbalimbali amabyao hutolewa kwenye vyombo vya habari ili uweze kujiunga kurasimisha ujuzi wako. Aidha, VETA pia huwa na program ya kurasimisha ujuzi, unaweza kuwasiliana nao. Moja ya program hizi, itakuwezesha kupata cheti ambacho utatumia kuombea leseni.
      Karibu

    2. Ndugu Boniphase,
      Unapaswa kuramisha ujuzi wako kupitia vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ama kupitia utaratibu wa uendelezaji ujuzi unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ambao hutangazwa mara kwa mara ili kupata cheti ya elimu ya ufundi, kisha kuomba leseni.
      Karibu

    1. Ndugu Emmanuel,
      Ndio unaweza kuomba leseni.
      Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ katika tovuti ya Mamlaka.
      Unapaswa kuwa na
      1. Picha (passport size ) yenye kivuli cha bluu
      2. Vyeti vya elimu ya Ufundi
      3.Wasifu (CV) inayoonesha shughuli za ufungaji umeme ulizofanya.

      Kisha utatumia nakala laini kufanya maombi, kwa kufungua mfumo wa LOIS, kujisajili na kufanya maombi ya leseni.

      Karibu

      1. Nimeingia kweny website ya ewura nimejaza form lakn sijaona sehem ya kuambatanisha cv,cheti na passport naomba msaada

        1. Ndugu Isaya,
          Tafadhali piga simu 0800110030 bila gharama ili uweze kupata ufafanuzi wa suala lako.

          Karibu

    1. Ndugu Emmanuel,
      Anaruhusiwa kuomba lseni

      Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ katika tovuti ya Mamlaka.
      Unapaswa kuwa na
      1. Picha (passport size ) yenye kivuli cha bluu
      2. Vyeti vya elimu ya Ufundi
      3.Wasifu (CV) inayoonesha shughuli za ufungaji umeme ulizofanya.

      Kisha utatumia nakala laini kufanya maombi, kwa kufungua mfumo wa LOIS, kujisajili na kufanya maombi ya leseni.

      Karibu

        1. Ndugu Pastory,
          Unaweza kupata leseni, inapaswa kuwa na cheti cha elimu ya ufundi, picha ndogo (pasipoti) yenye kivuli cha bluu, kitambulisho (leseni ya udereva, kitambulisho cha kupigia kura au cha uraia)na wasifu (CV).

          Karibu.

          1. Kama mtu ame soma Veta miaka mi2 na bahati mbaya aka feli mtihani wa level 2 anae living Ana ruhusiwa kufanya maombi ya kupata leseni akiwa na uzoefu takribani miaka mitano yupo mtaani Ana fanya kazi

          2. Ndugu Athumani,
            Cheti cha ellimu ni nyenzo muhimu katika maombi ya leseni. Kwa kuwa umeshapata uzoefu wa kazi mtaani, tunakushauri kwenda VETA kuomba kufanyiwa tathmini ya taaluma na ujuzi wako ilimupate barua au utambuzi kisha utatumia nyaraka hizo kuomba leseni.

            Karibu.

    1. Ndugu Mahamudu,
      Gharama ya maombi ya leseni ni shilingi 10,000/
      Na ada ya leseni daraja D ni shilingi 60,000/
      Jumla shilingi 70,000/
      Asante

  6. Ningependa kufahamu kanuni zinazomuongoza mtu kupata muhuri je akiwa na level 2 anaruhusiwa kumiliki mhuri wa 250V au ni kanuni zipi anapaswa kuzifuata,.

    1. Ndugu Stephen,

      Gharama za maombi ya leseni ni shilingi 10,000/ kwa leseni zote za umeme.
      Hata hivyo, ada ya leseni inatofautiana kulingana aina ya daraja la leseni.

      Asante

        1. Ndugu Hamidi,
          Maombi ya leseni ni kwa njia ya mtandao kupitia simu yako au kompyuta. Ingia katika mfumo wa LOIS kwenye tovuti yetu, jisajili na kisha uendelee na maombi ya leseni. Unatakiwa kuwa na cheti kilichotibitishwa, wasifu wako (CV) picha ya karibuni yenye kivuli cha bluu na kitambulisho (cha kura, au leseni ya udereva, cha taifa au hati ya kusafiria). Vyote katika nakala laini.
          Gharama za leseni zinatofautiana kulingana na daraja kama ifuatavyo:-
          Daraja A,B, S1, S2 ni tsh 130,000/
          Daraja C,D na S3 ni tsh 50,000/
          Malipo hufanyika kwa namba maalumu ya malipo ambayo hupatikana mtandaoni baada ya kuwasilisha maombi.
          Leseni hudumu kwa miaka mitano.
          Endapo utahutaji maelezo zaid, tupigie 0800110030 (bila gharama) , wakati na siku za kazi, Jumatatu hadi Ijumaa (saa 2asubuhi hadi saa 10 jioni)
          Karibu

  7. Naitwa Thomas simon kutoka kahama, niliomba lesseni tayari nimeshaipata, sasa naomba kuuliza utaratibu wa kupata mhuri ili nijitegemee Mimi mwenyewe nipitishe kazi zangu mim mwenyewe. Msaada tafadhari

    1. Ndugu Thomas, ukishakuwa na lsesni huna haja ya kuwa na mhuri. Andika namba yakO ya leseni kwenye fomu inatosha. Endapo unapata changamoto yoyote kuhusu suala hilo utujulishe mapema.
      Karibu

      1. Maelekezo ya kutumia namba ya lesseni imegoma, kwa mfumo wa nikonect kuna sehem ya mkandarasi na kunapassword ukiingiza namba ya lesseni haitambui kuwa wew nimkandarasi, nitumie njia gan sasa kwa kuwa mmesema kuwa kama ninalesseni haina haja kuwa na mhuri

  8. Naitwa Bushira mussa haruna, nimepata lesseni ya ewura class D je naweza kupitisha kazi zangu mwenyewe kwa kugonga mhuri kama contractor
    Msaada tafadhari

    1. Ndugu Bushira,
      Hakuna haja ya kugonga muhuri ukiwa na leseni.
      Andika namba yako ya leseni kwenye fomu, inatosha. Endapo utapata changamoto yoyote utujulishe mapema.
      Karibu.

  9. Naitwa Bushira mussa haruna nimepata lessen class D je naweza kupitisha kazi zangu mwenyewe kwa kugonga mhuri kama contractor
    Msaada tafadhari

    1. Ndugu Ally,
      Endapo kila kitu kipo sawa, leseni yako inashughulikiwa na itakapokuwa tayari utapewa taarifa ili uweze kuipata.
      Tunakushauri kupitia kwenye barua pepe yako mara kwa mara ili kubaini endapo kuna ujumbe wowote kutoka kwetu.
      Karibu

  10. Mm nomejisajili kwenye mfumo na nimejaza form ya maombi ya leseni ya umeme nikatumiwa user name na pasward lakini Kila niliingiza kwa umakini na bila kukosea inanikatalia naweza kutumia njia gani ili nipate leseni!?

      1. Vilevile, unasahuriwa kutuma anuani ya barua pepep yako na nywila (password) ili tufuatilie na kujiridhisha endapo kuna changamoto yoyote.
        Karibu.

  11. Habar!! Nmeomba leseni tangu mwezi 4,2022.mpk sahz bdo sijapata ilaaa nmeangalia progress yang IPO step no 6.imeandika(ELC MEETING preparation AND recommendation… Then page inayofuata imeandika PENDING!! JE, kipi kinachofuata baada ya hapo na lini ntaipata lesen yang maana cku30 zmeshapita mpk sahz bdo! Nipo morogoro.. Application no. ELINC/2022/0194… SIMU NO. 0620629616.

    1. Ndugu Alfred,
      Unapokuwa na leseni huna sababu ya kumiliki muhuri. Sehemu ya kugonga muhuri unaandika tu namba ya leseni yako.
      Karibu

  12. Changamoto yangu baada ya kujisajili nikitaka kulogin inakuwa ni ngumu sana msaada tafadhari pia naomba kujua gharama za leseni kwa mtyu wa certificate level three

    1. Ndugu Henrick

      Gharama za leseni ni kama ifuatavyo:-

      Daraja A,B, S1, S2= 130,000/
      Daraja C,D, W,S3= 50,000/

  13. Nimepata lesseni yangu class C lakini sijaunganishwa na nikonekt Tanesco wansema hawaioni kwenye data base ipoje hii,..?

    1. Ndugu Omari

      Wakati Mamlaka inaendelea kufuatilia suala lako tafadhali tupatie namba ya leseni,Ofisi ya TANESCO ilikupatia majibu, na namba ya simu ya ofisa wa TANESCO aliyekuhudumia endapo unayo.

      Karibu.

    1. Ndugu Boaz,
      Tafadhali tupatie namba ya maombi ya leseni sanjari na namba yako ya simu kwa ufuatiliaji zaidi.
      Asante

  14. Mimi nimesoma kozi fupi Veta ya miezi 6. Vipi naweza kuomba leseni na natakiwa kupata daraja lipi la leseni,na ilo daraja litaniruhusu kufanya kazi za aina gani???

    1. Ndugu Moses,
      Unaweza kupata leseni ya Daraja w.
      Utaratibu wa kuomba leseni ni kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa LOIS ulipo katika tovuti ya EWURA. Unaweza kuingia kwenye mfumo kwa kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ ambapo utatakiwa kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unapaswa kuwa na cheti, kitambulisho(taifa,leseni ya udereva au cha kura), picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu na wasifu wako (CV) inayoonesha kazi ulizofanya.
      Gharama ya leseni ni shs. 130,000/ kwa daraja A,B ,S1,S2 na shs.50,000/ kwa daraja C,D,S3 na W.

      Madaraja ya leseni, na mipaka ya shughuli zao.
      Aina ya Leseni Kazi Zinazohusika Elimu ya Ufundi wa Umeme na Uzoefu Husika Unahitajika
      Daraja A Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa umeme wa aina zote. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Cheti cha Usajili cha Utaalamu wa Uhandisi wa Umeme na vyeti husika vya elimu;
      (ii) Shahada ya uhandisi wa umeme au uhandisi wa umeme-mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au zaidi na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme,mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwenye msongo wa juu;
      (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme au Umeme-mitambo na
      miaka mine ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, miwili kati ya hiyo,iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa juu;
      (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo na miaka mitano ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, miaka mitatu kati ya hiyo iwe ya ufungaji mifumo ya umeme wa msongo wa juu.
      Daraja B Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa kati mpaka kiasi cha msongo wa volti 33,000. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme au
      uhandisi wa Umeme-Mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8, au zaidi na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufungaji mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo uwe wa ufungaji wa umeme katika msongo wa kati;
      (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme wa msongo wa kati; na
      (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au
      Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/ umeme- mitambo na miaka minne ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga wa mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa umeme wa msongo wa kati.
      Daraja C Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo usiyozidi volti 1000. isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme/umeme-mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au inayolingana na Shahada ya Uhandisi wa umeme;
      (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo au inayolingana na hiyo;
      (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Stashahada ya kawaida ya Uhandisi wa Umeme/U meme-Mitambo au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya Uhandisi Umeme au inayolingana na hiyo katika ufungaji mifumo ya umeme,
      (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 4, Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 5, au cheti cha kufuzu Mtihani wa ujuzi wa umeme daraja la I / Ngazi ya III au inayolingana na hiyo na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme; au
      (v) Cheti cha kufuzu cha Mtihani wa ujuzi wa umeme Daraja la II/ ngazi ya II au kinacholingana na hicho na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme.
      Daraja D Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo usiyozidi volti 230. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Cheti cha kufuzu mtihanii wa ujuzi wa Umeme daraja la I, II, III, au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 4, Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 5 au ainayolingana na hiyo katika ufundi wa ufungaji wa mifumo ya umeme; au

      (ii)mafunzo ya awali,kozi fupi, kozi za kati, cheti cha Juu cha Ufundi au cheti kinacholingana na hicho na uzoefu wa miaka mitatu katika kufunga mifumo ya umeme

      Daraja W Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, S1, S2, S3, C au D. Mwombaji wa leseni anapaswa kuwa na mafunzo ya awali/kozi fupi/kozi ya kati, au cheti cha Juu cha ufungaji wa mifumo ya umeme au sifa nyinginezo kutoka Taasisi nyingine za Kiufundi zinazotambulika kutoa mafunzo ya ufungaji mifumo ya Umeme.
      Daraja S1 Inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme katika msongo wa aina zote. (i) Cheti cha Usajili cha Utaalam wa Uhandisi wa Umeme au /Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa juu.
      (ii) Shahada ya Uhandisi wa Umeme au Uhandisi wa Umeme-Mitambo au
      Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 8 na miaka minne ya uzoefu wa kazi za ufungaji mifumo ya umeme ,miaka miwili kati ya hiyo iwe ni ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa juu wa umeme;
      (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitano ya uzoefu wa kazi katika masuala ya kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka mitatu kati ya hiyo iwe ya ufungaji mifumo ya msongo wa juu;
      (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 6 au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya Uhandisi wa Umeme/Umeme-Mitambo na miaka sita ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka minne kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme wa msongo wa juu
      Daraja S2 Inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 33,000 (i) Cheti cha Usajili cha Utaalamu Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa kati; au
      (ii) Shahada ya Uhandisi wa umeme au Uhandisi wa Umeme- Mitambo au
      Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 8 na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa kati; au
      (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 7 au zaidi, au Stashahada ya Juu ya Uhandisi Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka minne ya uzoefu wa kazi katika masuala ya kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa kati;

      Karibu

  15. Mimi Nimemaliza diploma yangu ya umeme mwaka 2021, uzoefu nilionao kwenye kazi za umeme ni field nilizifanya mwaka miezi miwili ya mwaka 2019 na mwaka 2020, baada ya kumaliza diploma nimekaa karibia mwaka mzima kazini nikifanya wiring za kiwandani na majumbani pamoja na kuunda control box za umeme, je naweza nikapata class gani? naomba majibu ili nifanye application asante

    1. Ndugu Ahadi
      Yafuatayo ni madaraja ya leseni za umeme na sifa husika kama zilizvyoainishwa katika Kanuni za ufungaji mifumo ya umeme za mwaka 2022 kwa rejea yako.

  16. Je mtu mwenye elimu ya shotcose ya umeme anaweza kupata leseni ili afanye kazi za umeme na kama apati munamsaidiaje ili afanye kazi za umeme

  17. Nimefanya maombi tangu 19oct 2022 na nifanya malipo ya application fee lakini mpaka leo sijapata majibu yoyote na mnasema ni ndani ya siku 30 leseni hotolewa ,je kwa wale tuliomaliza chuo kipindi kirefu mwaka 2013 kunachangamoto kupata leseni naomba kujua

  18. Naitwa Mussa naomba kufahamu maendendeleo ya leseni nilituma mombi trh 1/11/2022 ila bado sijapata mrejesho. ahasante

    1. Ndugu Musa,

      Tafadhali angalia katika barua pepe yako kuona endapo kuna taarifa kuhusu maombi yako kutoka kwetu.
      Endapo hakuna taarifa, tupatie namba ya maombi na namba yako ya simu kwa ufuatiliaji zaidi. Pia ni vyema tufahamu upo mkoa/wilaya gani.
      Karibu.

        1. Ndugu Modric,

          Unatakiwa kurasimisha ujuzi wako kwa kwenda kufanyiwa majaribio VETA au kupitia programu maalumu ya kurasimisha ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili upate cheti kisha uombe leseni.

          Karibu.

  19. Mnasema kuwa “Ni kosa kisheria kufanya kazi za kuweka mifumo ya umeme (electrical installations) bila kuwa na leseni hai iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)”. Lakini pia hapo hapo, ili mtu aweze kupata leseni anatakiwa aambatanishe Wasifu wake (CV) inayoonyesha Shughuli za uwekaji wa mifumo ya umeme alizozifanya!, Na wakati mnasema kuwa hairuhusiwi kufanya kazi hizo bila kuwa na Leseni, Hii imekaaje?. EWURA, Ninaomba ufafanuzi kuhusu hili Tafadhari .

    1. Ndugu John,
      Wasifu (CV) inaonesha kazi ulizofanya, endapo pia hukufanya kazi yoyote utaeleza. Ikumbukwe kuwa, Kanuni za Ufungaji Umeme zilitungwa mwaka 2009, kipindi ambacho mafundi umeme walishakuwepo, hivyo kigezo hicho kimewekwa ili kutambua shughuli ambazo mtu/fundi/mtaalamu wa umeme amefanya ambayo itasaidia kumpatia daraja stahiki la leseni.
      Karibu.

    1. Maana nikiingia kwenye hii link kisha nagusa maandish ya blue yanayosomeka “jisajili” naletewa orodha ya vipengele vya kujib sasa pale vitu ambavyo hatuna Mafund inakuaj maana nmejarib kuacha waz naona system ina dai nijaze. Au Mimi ndo nakosea utaratibu

      1. Ndugu Mohammed,
        Unapaswa kujaza fomu inayoonekana baada ya kubofya jisajili ili taarifa zako za awali ziwekwe kwenye mfumo.
        Karibu

  20. je ambao tumepata elimu ya mtaani tunafanyaje na ujuzi tunao wa kufanya wiring majumbani ila hatuna vyeti vya veta tuna vyeti vya elimu ya secondary tuu?

    1. Habari Bogohe
      Unashauriwa kwenda VETA kuomba wakufanyie tathmini kisha watakupatia cheti kulingana na ujuzi wako. Baada ya hapo, ndipo uombe leseni. Pia, uwe unafuatilia matangazo ambayo hutolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu ya kurasimisha ujuzi kwa vijana ili urasimishe ujuzi wako na kupatiwa cheti.
      Karibu

    1. Naomba kujua gharama za kulipia lesseni CLASS C Kwa mchanganuo Ufuatao;
      1.Gharama za fomu
      2.Gharama ya kulipia leseni yenyewe

  21. Nina cheti Cha level 2 na 3 leo nimeingia kweny website ya ewura nimejaza form lakn sijaona sehem ya kuambatanisha cv, cheti na passport piah naomb kuuliza nikipata leseni naruhusiwa kuwa na muhuri wang mwenyew kufanya kazi??

  22. Naomba kujua sifa za kuweza kujaza/kupitisha fomu za wateja wanaoomba huduma ya umeme Tanesco.
    Au fundi akiwa na leseni tayari anaweza kupitisha fomu za Tanesco?

    1. Ndugu William,
      Leseni huchukua muda wa siku 30 za kazi tangu kupokelewa maombi kamili. Maombi kamili ni yale yasiyo na marekebisho yoyote.
      Hivyo basi, endapo muda huo umepita tafadhali wasiliana nasi kwa namba 0800110030, wakati na siku za kazi, Jumatatu hadi Ijumaa (saa 2asubuhi hadi saa 10 jioni).
      Karibu

      1. Najiamini nanina uwezo mkubwa wakufanya kazi ya ufungaji mfumo wa umeme wandani
        ninahitaji kujazia yale nisiyo yajua nakupata leseni je nifanye nini? nipo babati manyara

        1. Ndugu Maulid,

          Tafadhali unasahuriwa kwenda VETA kuomba kufanyia tathmini ya ujuzi na uwezo wako wa ufundi umeme, kisha watakupa barua au cheti cha utambuzi na utakitumia kuomba keseni EWURA.
          Karibu

          1. Naomba msaada nimelipia leseni mpk sahv sijapata mrejesho jna Ipembe Masingija Mbunda No,ELIND/2024/0046

  23. Naomba msaada nimelipia leseni mpk sahv sijapata mrejesho jna Ipembe Masingija Mbunda No,ELIND/2024/0046

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *