TANGAZO:- Majina ya Waombaji wa Leseni za Umeme Waliopitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA tarehe 23/4/2019 kupewa Leseni

Kwa tangazo hili, waombaji hawa wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za EWURA Makao Makuu – Dodoma au Ofisi za Kanda ili kupata Control Number kwa ajili ya kulipia ada za leseni na kuchukua leseni zao. Soma Zaidi:-Waombaji Leseni za Umeme-Aprili-2019

______________________________________________________________________________________

Hits: 1239

61 thoughts on “TANGAZO:- Majina ya Waombaji wa Leseni za Umeme Waliopitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA tarehe 23/4/2019 kupewa Leseni

    1. Habari Mpate,tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz na utumie kiunganishi cha Online Services,kisha bofya ewura|LOIS kujisajili, utapata fomu na utajaza fomu hiyo kwa kufuata maelekezo. Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao.
      Karibu.

    2. Ndugu Mpate
      Fomu ya maombi inapatikana katika mfumo wa maombi ya leseni uitwao LOIS. Bofya kiunganishi Online Services kisha bofya LOIS kujisajili.
      Hakikisha una nakala ya vyeti vyako zilizothibitishwa, picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu na wasifu wako (CV). Vyote hivi viwe katika nakala laini ili uweze kuvitumia unapofanya maombi mtandaoni.
      Kwa maelezo zaidi piga 0800110030.
      Karibu

        1. Ndugu Selemani,
          Maombi hufanywa kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa LOIS, unapatikana katika tovuti yetu kwa kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/
          Bofya kiunganishi hicho kujisajili kisha endelea kujaza fomu husika. Vilevile unapaswa kuwa na cheti cha ufundi, wasifu wako (CV) unaoonesha kazi mbalimbali za umeme ulizofanya, picha yenye kivuli cha bluu pamoja na kitambulisho chako (kura,leseni ya udereva au nida) kabla ya kuanza kufanya maombi.
          Gharama ya maombi ni sh. 10,000/ inayolipwa kupitia control number ambayo inapatikana katika mfumo.
          Endapo utapata changamoto yoyote tupigie bure 0800110030 siku na muda wa kazi.
          Karibu

    3. Bwana Mpate,
      Fomu ya maombi inapatikana katika kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/.
      Baada ya kufungua na kujisajili utaipata fomu hiyo.
      Unapaswa kuwa na vyeti vya elimu ya umeme vilivyothibitishwa, wasifu wako (CV) na picha pasipoti yenye kivuli cha bluu; vyote vikiwa katika nakala laini.
      Zaidi wasiliana nasi 0800110030 (bure)

  1. Mm nimeomba lesen ya umeme tokea mwezi wa tatu mwaka huuu na kulipia tayari elfu 10 mpaka sasa naona kimya

    1. Ndugu Venancy,
      Tafadhali tufahamishe umeomba leseni ukiwa wapi kwa maana ya mkoa, vilevile tunaomba namba yako ya simu kwa ufuatiliaji zaidi wa suala lako. Unaweza pia kupiga simu BURE 0800110030 muda wa kazi ili kuweza kuzungumza nasi moja kwa moja.
      Karibu

  2. Naomba kujua lesen ya umeme inatumia mda gani?? Na madalaja yanatolewaje mfano una level two unapa leseni ya aina gan??

    1. Ndugu Charles,
      Leseni ya umeme hutolewa ndani ya siku 30 tangu kupokelewa kwa maombi yaliyokamilika. Hatahivyo leseni inaweza kuchelewa kidogo endapo uthibitisho kutoka chuo alichosoma mwaombaji wa leseni kitachelewa kuwasilisha uthibitisho EWURA.
      Madaraja ya leseni za umeme yanayotolewa na EWURA ni haya yafuatayo:-
      Leseni Daraja A: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa aina zote isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja B: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa kati (33,000V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja C: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa chini (400V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

      Leseni Daraja D: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa njia moja (230V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.
      Leseni Daraja W: inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, C au D.
      Leseni Daraja “S1”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme katika msongo wa umeme wa aina zote.
      Leseni Daraja “S2”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 33,000; na
      Leseni Daraja “S3”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 1,000.

    1. Ndugu Marcel, Mfumo wa LOIS ni rafiki na rahisi, endapo unapata changamoto kuingia huenda ni tatizo la kiufundi au intaneti kutokuwa vizuri eneo ulipo. Aidha tunakupa pole kwa changamoto hiyo. Tafdhali tumia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ kuingia katika mfumo wa lois na ujisajili. Endapo utapata changamoto zaidi tuma barua pepe kupitia support@ewura.go.tz na uweke namba ya simu au piga simu 080011000 BURE muda wa kazi au fika katika ofisi yetu iliyokaribu nawe- Arusha, jengo la PSSSF zamani PPF Plaza karibu na Kibo Palce Hotel, Mwanza jengo la PSSSF Barabara ya Kenyata; Dodoma Jengo la EWURA, Medeli Magharibi, Mbeya jengo la NHIF na Dar es Salaam jengo la PSSSF Kijitonyama.

      1. Kama barua ya uthibitisho imeshafika chuoni nataarifa zika rudi, mbona Sasa mchakato unachukua muda mrefu? Tuna shida kupata leseni haraka ili tufanye kazi kwa Uhuru nasio kuambiwa tunaiibia serikali mapato yake

      2. Naitwa Thomas Simon shija kutoka kahama shinyanga namba yangu ya usajili ni ELINA/2021/0086 naomba kukamilishiwa huduma niliyo omba ya electrical installation license

    1. Nina miezi 4 Sasa tangu niombe lesseni ya electrical installation license. Lakini namba 0767000096 ilipingia ikidai uhakiki wa barua walio tuma chuoni nikawapa namba ya simu ya mkuu wa idara akadai kuwa kaongea nae, na akaniambia kuwa wamekaa nakupitisha kwahyo nisubiri control number au nimtumie hela 150000 anilipie hukohuko. Nikamwambia anipe tu control number lakini mpaka leo wiki ya 4 hajatuma control number. Naomba msaada.
      Namba yangu ni 0752731349 au 0626082753
      Email: thamassimon196@gmail.com

  3. Habari EWURA,
    Naomba kufahamu ni baada ya muda gani muombaji wa leseni ya umeme hupata leseni yake baada ya kufanya maombi na kukamilisha malipo. Nimefanya maombi tarehe 4, July 2021 lakini mpaka sasa sijaipata.

    1. Ndugu Sospeter,
      Leseni hutolewa ndani ya siku 30 baada ya kupokea maombi kamili. Hata hivyo, inaweza kuchelewa endapo uthibitisho kutoka chuo ulichosoma utachelewa kuwasilishwa EWURA.
      Tunashauri utume namba yako ya maombi kwa ufuatiliaji zaidi. Pia tungependa kufahamu umeomba ukiwa wapi ili mtaalam wetu wa eneo husika awasiliane nawe. Vilevile itakuwa vyema ukitupatia namba yako ya simu.
      Karibu

      1. Habari EWURA,

        Asante kwa maelekezo. Namba yangu ya maombi ni ELINA/2021/0081. Nimefanya maombi nikiwa Dar es Salaam. Namba yangu ya simu ni 0759859732 / 0683073395.

        Asante

      2. nashindwa jinsi ya kujiunga ili kuomba leseni mfumo mgumu niko mpimbwe kijijini naomba msaada

        1. Ndugu George,
          Nimekutumia mwongozo wa namna ya kuomba leseni.Naomba upitie mwongozo huo ili uendelee kuomba leseni.
          Karibu

  4. Mimi ninaitwa Steven Macha niko mwanza swali langu nimeweza kujiunga na lesen ya umeme jana je ninaweza kubadlisha daraja kabla lesen haijatoka??

    1. Ndugu Macha,
      EWURA hutoa leseni kulingana na elimu na uzoefu katika shughuli ulizofanya. Hivyo basi, haijalishi umeomba daraja gani kwa sasa, utapewa daraja unalostahili.
      Karibu

  5. Nina miezi 4 Sasa tangu niombe lesseni ya electrical installation license. Lakini namba 0767000096 ilipingia ikidai uhakiki wa barua walio tuma chuoni nikawapa namba ya simu ya mkuu wa idara akadai kuwa kaongea nae, na akaniambia kuwa wamekaa nakupitisha kwahyo nisubiri control number au nimtumie hela 150000 anilipie hukohuko. Nikamwambia anipe tu control number lakini mpaka leo wiki ya 4 hajatuma control number. Naomba msaada.
    Namba yangu ni 0752731349 au 0626082753
    Email: thamassimon196@gmail.com

    1. Ndugu Thomas,
      Tumefuatilia, leseni yako haijakamilika. Tahadhari: Usimtumie pesa mtu yeyote. Leseni yako itakapokuwa tayari, utapatiwa control number ili ufanye malipo. Zoezi hili halina wakala yoyote kwa niaba ya EWURA.
      Karibu

      1. Naitwa Thomas Simon shija kutoka shinyanga kahama,
        Naomba kuuliza kwenye lesseni yangu kunashida gani mpaka saivi sijapata taarifa yeyote mpaka Sasa nimuda mrefu Sana umepita na ukipiga simu kwenye namba ya huduma kwa wateja hawatuelekezi vizuri. Kama imeshindika Bora nipewe tu taarifa ili nijue lakufanya.

        1. Ndugu Thomas,
          Tumepokea suala lako,unasahuriwa kutuma namba yako ya simu na namba yako ya maombi ya leseni kwa ufuatiliaji zaidi.
          Karibu.

        2. Ndugu Thomas,
          Ufuatiliaji wetu umebaini kwamba, leseni yako ipo tayari baada ya kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi tarehe 28 Oktoba, na imeshatumwa katika Ofisi yetu ya Kanda ya Ziwa, iliyopo Mwanza. Hivyobasi, utajulishwa taratibu za kuipokea.
          Karibu

    1. Ndugu Steven,
      Tafadhali tujuze siku/mwezi uliyofanya malipo.
      Unaweza pia kutupatia namba yako ya simu kwa ufuatiaji zaidi.
      Karibu

  6. Naomba kuuliza natumiwa lini control number ya leseni maana chuo wamesha malza jukum lao bado huko lini mnanitumia namba ya malpo

    1. Ndugu Mohamedi,
      Tafadhali tupatie namba yako ya simu ili tuwasiliane kwa ufafnuzi zaidi ama piga simu 0800110030 (bila gharama) siku na muda wa kazi.

  7. Naomba kujuwa maendeleo ya leseni yangu ya umeme niliomba mwezi wa NNE (4) 2022.je, ntaipata lini? Nipo Morogoro(kilombero)

    1. Ndugu Silus,
      Kwa mujibu wa Mkataba wa Mteja wa EWURA, leseni zinapaswa kutolewa ndani ya siku 30 tangu kupokea maombi kamili. Ucheleweshaji zaidi unaweza kutokea endapo EWURA itachelewa kupokea uthibitisho kutoka chuo ulichosoma. Hata hivyo unashauriwa kuangalia maendeleo ya leseni yako kupitia LOISkwa kuzingatia muda tajwa. Aidha, unaweza kutuma namba yako ya maombi ili tuweze kufuatilia kwa karibu zaidi.
      Karibu

    1. Ndugu Mushi,
      Tafadhali tujuze uliomba lini leseni na upo Mkoa gani. Vilevile tutumie namba yako ya maoni na namba ya simu kwa ufuatiliaji zaidi.
      Karibu

  8. Naomba kujuwa maendeleo ya leseni yangu tangu niombe mwezi (wa4)2022.mpaka sahiz bdo sijapata mrejesho km ntaipata lin istoshe password zangu kila nkiingiia znagoma; naomba msaada wakuniangalizia mrejesho wa maombi yangu ya leseni.. Application no. ELINC/2022/0194… Simu no. 0620629616… Nipo morogoro

  9. Habar!! Naomba kujuwa lini leseni yang itakuwa tayali maana mpk sasa nimiezi miwili imepita tangu mwez4 2022… Nilifanya mawasiliano waliniambia vyeti vinafanyiwa uhakiki je? Lini itakuwa tayali.. Simu no. 0620629616. Application no. ELINC/2022/0194.. Nipo morogoro

  10. Nimelipia ada ya kurenew leseni yangu (ELINB-2019-2412-C)tangu 19/05/2022
    Lakini mpaka sasa naona kimya. application ref ni ELINC/2022/0246
    KWANI KURENEW NAKO KUNACHUKUA MUDA MREFU HIV?

    1. Ndugu Ramadhani,
      Maombi yako yanashughulikiwa, na utapatiwa leseni yako baada ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi. Itarajiwa Bodi iatafanya kikao kuanzia tarehe 22 Juni 2022.
      Karibu.

      1. Nashukuru sana kwa majibu mkuu….ila Nina swali la nyongeza..bodi hukaa kikao Mara ngapi kwa mwaka?

  11. Habar!! Naomba kujuwa lini leseni yang itakuwa tayali maana mpk sasa nimiezi miwili imepita tangu mwez4 2022… Nilifanya mawasiliano waliniambia vyeti vinafanyiwa uhakiki je? Lini itakuwa tayali.. Simu no. 0620629616. Application no. ELINC/2022/0194.. Nipo morogoro

  12. Nmejarbu kuangalia progress ya maombi yang ya lesen imeandika,, ELC meeting preparation and recommendation!! Je kipi kinachofuata baada ya hapo maana tangu nifanye maombi mwezi wa4 2022!! Cku30 zmeshapita Naona bdo lini itakuwa tayali?? Application no. ELINC /2022/0194. Simu no. 0620629616. Nipo morogoro

  13. Habari za kazi naomba kuuliza maombi yangu yamefikia wapi maana sipati sms yoyote mpaka sasa namba yangu ya ombi ni ELINC/2022/0311
    Namba yangu ya simu ni 0782567462

  14. Habari za kazi naomba kuuliza maombi yangu yamefikia wapi maana sipati sms yoyote mpaka sasa namba yangu ya ombi ni ELINC/2022/0311
    Namba yangu ya simu ni 0782567462
    Nipo dar es salaam

    1. Ndugu Ahadi,
      Unashauriwa kupitia barua pepe yako mara kwa mara ili kuona endapo umepokea ujumbe kutoka EWURA kuhusu maendele ya maombi yako. Ikiwa hakuna ujumbe wowote wasiliana nasi kwa simu 0800110030 (BURE) muda na siku za kazi.
      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *