TANGAZO: Majina ya Waombaji wa Leseni za Umeme Waliopitishwa na Bodi Kupewa Leseni Tarehe 22/6/2019

Kwa tangazo hili, waombaji hawa wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za EWURA Makao Makuu – Dodoma au Ofisi za Kanda ili kupata Control Number kwa ajili ya kulipia ada za leseni na kuchukua leseni zao. Soma Zaidi:-Orodha ya Wakandarasi Waliopitishwa kupewa Leseni-22062019

 

Hits: 1969

44 thoughts on “TANGAZO: Majina ya Waombaji wa Leseni za Umeme Waliopitishwa na Bodi Kupewa Leseni Tarehe 22/6/2019

  1. Ndugu Mbwago,
   Fanya maombi kupitia mtandao wa intaneti. Bofya kiunganishi Online Services katika tovuti yetu na kisha bofya LOIS kujisajili.
   Hakikisha una nakala ya vyeti vyako zilizothibitishwa, picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu na wasifu wako (CV). Vyote hivi viwe katika nakala laini ili uweze kuvitumia unapofanya maombi mtandaoni.
   Kwa maelezo zaidi piga 0800110030.
   Karibu

   1. Naomba kujua mm niliomba leseni 2018 September, December nikaitwa Mwanza ili nikailipie nakuchukua ,sikukua Mwanza hinyo sikuweza kuichukua nitumie utaratbu upi ili niipate

    1. Ndugu Yona,
     Fika ofisi yetu ya Mwanza ili uweze kuchukua leseni yako.
     Unaweza pia kupiga simu bure 0800110030 ili kuunganishwa na Afisa wetu wa Mwanza anayeshughulikia masuala ya leseni.
     Ofisi yetu ya Kanda ya Ziwa ipo Ghorofa ya 4,Upande wa Mbele,PPF Plaza, Barabara Kenyatta,S.L.P 2069, Mwanza, TanzaniaSimu:+255 28 2506071-72; Nukushi +255 28 2506073

   2. Mimi ni shadrack shida yangu kila ninapo ingia mtandaoni kwaajili ya ujazaji form inagoma kuna kuwa na shida gani ?

    1. Habari Shadrack,
     Pole kwa changamoto.
     Tafadhali naomba kufahamu upo wapi na tupatie namba yako ya simu.
     Unaweza pia kupiga simu bure 0800110030 ili kutatuliwa suala lako.

    2. Ndugu Shdrack, pole sana.
     Tafadhali piga simu 0800110030 (bure) ili suala lako lifanyiwe kazi zaidi.
     Karibu

  2. Mimi ni james sanga nili omba maombi ya kuhuwisha lesseni yangu mwaka jana (Mwanza) mpaka leo sijapata JAMES SANGAELINC/2019/3481

 1. Nauliza kuhusu hizo leseni za Electrical Installation; nilipata taarifa hizi kupitia kwenye maonesho ya sabasab kupitia TV nikapata anwani ya email hii ila nimeshidwa wap haswa ndio kuna hizo process za kujiunga ili kuweza kupata hivyo leseni kwa sababu mm ni mwanafunzi nlio hitimu katk fani hiyo kwa miaka mitatu kutoka hapa RVTSC MOSHI (Veta Moshi) na punde nasubiria matokeo yangu ya mwaka wa tatu. Katika utafutaji wa rizq basi sharti utii vigezo na masharti bila kushurutishwa naomba kujiunga katika upewaji wa leseni na vipi taratibu zake ili kuipata hiyo leseni.

 2. Mimi ni mwanafunzi nliehitimu toka Veta Moshi katika fani hiyo ya Electrical Installation kwa muda wa miaka 3 naulizia taratibu za kufanya au kujiunga kuweza kuwa na leseni ya ufundi umeme.

  1. Habari Khalidi,
   Maombi ya leseni za shughuli za ufungaji umeme hufanywa kwa njia ya mtandao kupitia https://lois.ewura.go.tz/ewura/.
   Unatakiwa kuwa na nakala laini (soft copy) za vyeti vyako, picha yenye kivuli cha bluu, wasifu wako (CV)na vyote viwe vimethibitishwa na wakili au hakimu.
   Kisha inigia katika mfumo kupitia website yetu na uendelee kujisajili na kujaza fomu.
   Unaweza pia kuwasiliana nasi bure kupitia 0800110030.
   Asante

  1. Bwana Joseph,
   Mwombaji wa leseni anapaswa kuwa na elimu ya ufundi wa umeme kuanzia wiremen na kuendelea.
   Maombi ya leseni hufanywa kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Unapaswa kuwa na vyeti, picha ya passport yenye kivuli cha bluu na wasifu wako-vyote vikiwa katika nakala laini kabla ya kuanza kufanya maombi.
   Unaweza kuwasilasiliana nasi zaidi bure 0800110030
   Asante

  2. Bwana Joseph,
   Mwombaji wa leseni anapaswa kuwa na elimu ya umeme kuanzia ngazi ya cheti.
   Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Unapaswa kuwa na vyeti vilivyothibitishwa, wasifu wako (CV) na picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu, vyote vikiwa katika nakala laini.
   Kwa msaada zaidi piga 0800110030
   Karibu

  1. Ndugu Kinunda,
   Karibu katika Ofisi yetu ya Dodoma, ghorofa ya 5 jengo la PSSSF, lilipo barabara ya Makole.
   Unaweza pia kupiga simu kupitia 0800110030 kwa maelezo zaidi.

    1. Bwana Kinunda,
     Pole, tunaomba kufahamu upo mkoa gani? Pia tuma reference number yako uliyopata kupitia LOIS.
     Asante

 3. Naomba kufahamu, toka mwaka Jana 2019 mwezi wa 7 nilituma maombi ya leseni ya ufundi Umeme. Ila mpaka mda huu sijapewa mrejesho wowote na siku nazo zinazidi kwenda. Naomba msaada kwa hili FREDY BONIPHACE MAKOYE

  1. Habari Fredy,
   Samahani naomba kufahamu upo sehemu gani na namba yako ya simu.
   Unaweza pia kupiga simu bure 0800110030.
   Asante

  1. Ndugu Emmanuel,

   Tafadhali jedwali lipo LICENCE FEE
   Type / Class of
   Licence
   Renewal Annual
   Fee (TZS)
   Initial licence
   fee
   Duplicate Licences fees
   A, S1 100,000 / – 150,000 30,000
   B, S2 80,000 / – 120,000 25,000
   C, S3 60,000 / – 100,000 20,000
   D 30,000 / – 60,000 15000
   W 20,000 / – 40,000 10,000
   Application – 10,000

   Zaidi soma kanuni “The-Electricity-Electrical-Installation-Services-Rules-2019-GN-382” inapatikana katika kiunganishi https://www.ewura.go.tz/wp-content/uploads/2019/06/The-Electricity-Electrical-Installation-Services-Rules-2019-GN-382.pdf
   Endapo utakuwa na maswali zaidi piga simu 0800110030 (bure)

 4. Naitwa Joseph Ishasi mwenye Leseni namba ENLINC-2018-1610-D. Muda wa kufanya marekebisho ya Leseni yangu umekaribia, hivyo nilikuwa nahitaji msaada wa utaratibu wa kufanya Jambo hilo.

 5. Hadi sasa ninamiez minne sijapata lesen yangu ya umeme hiv inachukua muda gani….Bernard benjamini ngonyani

  1. Bwana Bernad,pole sana
   Tafadhali tungependa kujua ulipo,namba yako ya simu ili tuweze kuwasiliana zaidi na kufanya ufuatiliaji. Unaweza kupiga simu 0800110030 (Bure) ili kuwasilisha suala lako.
   Karibu

    1. Bwana Abel,
     Leseni zote zilizokamilika hutolewa kila mwezi baada ya kupitishwa na Bodi.
     Endapo uliomba leseni na hujasikikia kutoka kwetu, tafadhali tuma Reference Number yako, Mahali ulipo na namba yako ya simu.
     Pia unaweza kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya leseni yako kupitia mfumo wa LOIS.
     Zaidi piga simu 0800110030 (bure) muda wa kazi.
     Karibu

 6. Habari naomba kuuliza katika progress katika Lois Ewura nimekuta ELC meeting preparation and recommended nini kinaendelea naomba kufahamishwa.

  1. Bwana Juma,
   Asante kwa mrejesho. Tutarejea kwako.
   Pia unaweza kupiga simu bure 0800110030 muda wa kazi.
   Karibu

 7. Mimi james sanga bado sijajibiwa ombi langu karibu wiki ya pili sasa.Mimi nili omba kuhuisha leseni yangu mwaka jana nikapewa namba James sanga ELNIC 2019 3481 lakini tangu mwaka jana mpaka leo sijapata kitu.Kwani kulinew inachukuaje mda mrefu hivi.MIMI NAIPENDA NCHI YANGU NILIPIE KODI.JE MIMI MTEJA WENU EWURA NIFANYEJE?

   1. Nashukulu kwa kuliona ombi langu.Ushauli wangu natamani sana light kama mafundi umememe wote wangelipata leseni.Hata serikali yetu ingenufaika na kodi,mafundi tupo wengi sana lakini wenye reseni hata robo hawafiki.Tafuteni mbinu ili kuwafikia wote.Kama BRELLA.

 8. Nashukulu kwa kuliona ombi langu.Ushauli wangu natamani sana light kama mafundi umememe wote wangelipata leseni.Hata serikali yetu ingenufaika na kodi,mafundi tupo wengi sana lakini wenye reseni hata robo hawafiki.Tafuteni mbinu ili kuwafikia wote.Kama BRELLA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *