Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta

Visits: 19110

245 thoughts on “Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta

 1. habari, naomba kuuliza inachukua mda gani kuomba lesen ya ufundi umeme baada ya kulipia bei ya ada 10,000/=

     1. Ndugu William,
      Mwombaji yeyote wa leseni ya rejareja ya mafuta, sharti afanye maombi kwa njia ya kieletroniki kupitia http://www.ewura.go.tz/lois. Taarifa muhimu zinazohitajika kuambatanishwa katika maombi hayo ni:
      (a) Nakala ya nyaraka za usajili wa Kampuni au Leseni ya Biashara;
      (b) Nakala ya Hati Miliki ya kiwanja palipojengwa kituo cha mafuta au uthibitisho
      kutoka Mamlaka husika iliyoruhusu ujenzi wa kituo hicho.
      (c) Nakala ya kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri au Manispaa husika.
      (d) Nakala ya Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira (Environmental Impact Assessment Certificate) kinachotolewa na Baraza la Hifadhi ya Mazingira.
      (e) Nakala ya cheti cha mlipa kodi (TIN Certificate).
      (f) Nakala ya cheti cha zima moto (Fire Safety Certificate) kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
      (g) Kibali cha ujenzi kutoka EWURA (kwa vituo vilivyojengwa baada ya Aprili 2009).
      (h) Orodha ya miundombinu iliyopo katika eneo hilo. Kwa upande wa matanki uooneshwe ujazo wake.
      (i) Mchoro wa kituo ambao umesainiwa na Mhandisi aliyesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania ukionesha yafuatayo:
      (i) umbali uliopo kati ya miundombinu ya kituo cha mafuta;
      (ii) mahali pa kuingilia na kutokea kituoni;
      (iii) mpaka wa kiwanja;
      (iv) mahali pampu zinapotegemewa kufungwa; na
      (j) Stakabadhi ya malipo ya ada ya maombi ya leseni.

      MASHARTI YA KUPEWA LESENI YA REJAREJA YA KUENDESHA BIASHARA YA MAFUTA

      Pamoja na kuwasilisha nyaraka zilizotajwa, kituo cha mafuta sharti kikaguliwe ili kuona kama kinakidhi masharti ya kupewa leseni. Masharti hayo ni pamoja na:

      (a) Kuwa na vifaa vya kutosha vya kuzimia moto: Angalau ndoo moja ya mchanga na mtungi mmoja wa kilogramu 9 aina ya “ABE” kwa kila eneo ilipo pampu.
      (b) Kuwepo switchi ya dharura iliyowekwa sehemu inayoonekana na kufikika kwa urahisi na mtu yeyote kwa ajili ya kuzima umeme. Swichi iandikwe “SWICHI YA DHARURA”.
      (c) Kuwepo na vyoo safi na vya kutosha kwa ajili ya wafanyakazi wa kituo na wateja kwa ujumla. Viwepo vyoo vya wanaume na wanawake.
      (d) Alama za kutosha za usalama zinazoonekana vizuri na mteja anapoingia hapo kituoni. Alama hizo ni pamoja na: Zima Injini, Zima Simu na Usivute Sigara.
      (e) Matanki, vifaa vya kupimia ujazo wa matanki (dip rods) na pampu lazima viwe vimehakikiwa na Wakala wa Vipimo (WMA). Aidha, pampu sharti ziwe katika hali nzuri ya kufanya kazi.
      (f) Mifuniko ya sehemu ya kushushia mafuta na pampu sharti iandikwe ili kuonesha aina ya mafuta yaliyomo au yanayouzwa.
      (g) Mifuniko ya matanki ya mafuta sharti ipakwe rangi zifuatazo: Petroli – Nyekundu, Dizeli – Njano na Mafuta ya taa – Bluu
      (h) Kila mfuniko wa tanki na mahali pa kuteremshia mafuta vitengenezwe kulingana na viwango vinavyokubalika katika tasnia ya mafuta.
      (i) Kituo kiwe kimesakafiwa kwa zege angalau mita nne (4) kuzunguka maeneo yote ya pampu na mahali pa kushushia mafuta na pia kiwe na mfereji uliojengwa vizuri na unaoungana na kitenganisha maji na mafuta (oil/water separator).
      (j) Kitenganisha maji na mafuta sharti kiwe na vyumba (chemba) vitatu na kila chumba kiwe na urefu usiopungua mita 1, upana wa mita 2 na kimo cha mita 1. Pia, sharti kiwe na mfuniko unaoweza kufunguliwa kwa urahisi na kuwekwa vali ya kufunga na kufungua mahali pa kutolea maji safi.
      (k) Kila tanki la mafuta liwe limeunganishwa na bomba la kupumulia (vent pipe) lenye kimo kisichopungua mita 3.5. Bomba hizo ziwe angalau mita 1.5 kutoka jengo lolote na angalau mita 4.5 kutoka chanzo chochote cha kuingiza hewa au kusababisha moto kama vile dirisha, kiyoyozi, jenereta n.k.
      (l) Eneo la pampu liwe limejengewa vizuizi vya kukinga pampu zisigongwe na gari (crush barriers). Vizuizi hivyo viwe na kimo kisichopungua mita moja kutoka sakafu ya kituo.
      (m) Kituo kiwe kimejengewa paa (canopy) linalokidhi viwango vinavyotakiwa katika ujenzi wa vituo vya mafuta. Kimo cha paa kisipungue mita 5 na upana wa mita 3 kila upande kutoka katikati ya pampu.
      (n) Kituo kiwe katika hali ya usafi.
      (o) Kuwepo kwa waya wa kuzuia mwako wa umeme (spark) ambao unaunganishwa na gari la mafuta wakati wa kuteremsha mafuta.

      Kituo cha mafuta kinachokidhi masharti tajwa hapo juu, ndicho hupewa leseni na EWURA. Vituo vya mafuta ambavyo havikidhi masharti ya kupewa leseni, haviruhusiwi kufanya biashara hadi hapo vitakapokuwa vimekidhi masharti yote.

      ADA NA MUDA WA UHAI WA LESENI
      Ada ya leseni ni Shillingi milioni moja (1.000.000/=). Muda wa leseni ni miaka mitano (5). Baada ya uhai wa leseni, mwenye kituo anatakiwa aombe kuhuisha leseni kwa kujaza fomu ya maombi na kuileta EWURA.

      Asante.

    1. Ndugu Mohamed,
     Gharama ya leseni inaazia sh. 20,000/ hadi 150,000/ kulingana na daraja husika.Madaraja ya leseni ni kuanzia w hadi A.
     Karibu.

    1. Ndugu Michael,
     Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako. Endapo utakuwa na swali au kuhitaji ufafanuzi zaidi, piga simu BURE 0800110030 au andika barua pepe info@ewura.go.tz.
     Vilevile unaweza kufika katika Ofisi zetu za makao makuu Dodoma au Kanda zilizopo Arusha, Dar es Salaam, Mbeya,Mwanza na Kanda ya Kati Dodoma.
     Karibu.

     1. Naomba kupata taratibu pia za kufungua kituo kidogo cha mafuta vijijini

    1. Ndugu Paulo,

     MADARAJA YA LESENI ZA UMEME YANAYOTOLEWA NA EWURA
     Leseni Daraja A: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa aina zote isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

     Leseni Daraja B: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa kati (33,000V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

     Leseni Daraja C: inatolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa chini (400V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.

     Leseni Daraja D: inatolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa njia moja (230V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.
     Leseni Daraja W: inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, C au D.
     Leseni Daraja “S1”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme katika msongo wa umeme wa aina zote.
     Leseni Daraja “S2”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 33,000; na
     Leseni Daraja “S3”: inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 1,000.

   1. Inabidi kuwe na utofauti wa kilomiter au mita ngapi baina ya kituo na kituo wilayani au mijin ili uweze kufungua kituo kipya?

    1. Ndugu Samson,
     Tafadhali pitia maelezo yafuatayo kwa ufafanuzi zaidi:-
     UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI

     1. Utangulizi

     1.1 Mahitaji ya mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka. Ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama “boda boda”.

     1.2 Hata hivyo, maeneo mengi ya vijijini hayana vituo vya mafuta kutokana na ukweli kwamba, wawekezaji wa biashara hiyo wenye mitaji mikubwa husita kujenga vituo vya kuuzia mafuta Vijijini kwa kuona maeneo hayo hakuna biashara ya kutosha .

     1.3 Matokeo yake, wafanyabiashara wenye mitaji midogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta, huingia kwenye biashara hii. Kutokana na mitaji yao midogo na kutokuwa na uzoefu, wafanyabiashara hawa huanza kufanya biashara ya mafuta kwa kutumia miundo mbinu hafifu na isiyo salama kama vile kuhifadhi mafuta kwenye mapipa, madumu ya plastiki na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

     1.4 Uhifadhi wa mafuta kwa namna hiyo ni hatari kwa Usalama, Afya na Mazingira. Ni dhahiri kuna matukio mengi ya moto ambayo yamesababishwa na uhifadhi wa mafuta majumbani au kwenye vibanda vya biashara. Ajali hizo za moto, zimegharimu maisha ya watu na kuharibu mali. Pia, wafanyabishara katika maeneo hayo wako hatarini kupata magonjwa ya kansa ya ngozi kutokana na kushika mafuta wakati wa kutoa huduma hiyo. Kwa upande mwingine, mafuta humwagika ardhini na kuharibu mazingira.

     1.5 Kuhifadhi mafuta kutumia vyombo vya plastiki kunaharibu ubora wa mafuta hayo na hasa mafuta ya petroli. Mafuta na vyombo vya plastiki vina asili moja. Ubora wa mafuta ya petroli pia unaweza kuathiriwa na mwanga wa jua. Hivyo, vyombo vya moto vinavyo tumia mafuta yanayohifadhiwa kwenye vyombo vya plastiki viko hatarini kupata madhara kwa sababu ya kutumia mafuta ambayo hayana ubora unaohitajika.

     1.6 Biashara ya mafuta ya petroli ni muhimu sana, lakini ni hatari ikiwa itafanyika kiholela bila kufuata misingi ya usalama na viwango. Hivyo ni vyema mafuta ya petroli yakahifadhiwa na kuuzwa kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo. Lengo ni kulinda usalama, afya, ubora wa mafuta na mazingira.

     1.7 Moja ya miundombinu ambayo inatimiza lengo tajwa hapo juu ni vituo vya kuuzia mafuta. Sababu kubwa ni kuwa, kwenye kituo cha mafuta, matenki ya kuhifadhia mafuta yanafukiwa chini ya ardhi. Hivyo, hata moto ukitokea si rahisi mafuta yaliyo ndani ya matenki hayo kulipuka.

     1.8 Kipeperushi hiki kimelenga kutoa maelezo kwa kifupi juu ya ujenzi wa vituo vya gharama nafuu kwa kuelezea vitu muhimu na vya msingi vinavyotakiwa kuzingatiwa wakati wa kujenga kituo cha mafuta. Vilevile, Kipeperushi hiki kinaelezea Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini ambazo zilitungwa mahsusi kwa ajili ya kupunguza gharama za uwekezaji wa vituo hivyo.

     1.9 Ni lengo la EWURA kutengeneza mazingira ambapo watu wa Vijijini wanakuwa na haki sawa na watu wa Mijini katika upatikanaji wa bidhaa ya mafuta kwa hali ya ubora na usalama unaohitajika na kwa bei nafuu.

     1.10 Ni matumaini ya EWURA kwamba, Kipeperushi hiki kitatoa mwanga kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa mafuta ya petroli nchini namna ambavyo uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini unavyoweza kufanywa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watumiaji wa mafuta hayo kupata huduma nzuri zaidi na salama bila kumuathiri mfanyabiashara wa mafuta.

     2 Mahitaji na Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Ujenzi

     Ili uweze kujenga kituo unatakiwa kuzingatia yafutatayo:

     (a) Uwe na kiwanja ambacho Mamlaka husika (mfano: Halmashauri ya kijiji) imeridhia kitumike kwa ajili ya biashara ya kituo cha mafuta. Ili kukidhi viwango vya usalama (safety distance requirements), kiwanja kinachofaa kujenga kituo cha mafuta kinatakiwa angalau kiwe na ukubwa wa mita za mraba 400.

     (b) Uwe angalau na tenki moja (1) la kuhifadhia mafuta. Kama utauza aina zaidi ya moja ya mafuta, matenki yaongezeke sawia. Tenki liwe na ujazo wa angalau lita 4,500 au 5,000.
     Uwe na pampu yenye mkono mmoja au miwili kulingana na aina za mafuta.
     (c) Bomba nne (4) za chuma za inchi nne (inchi ) na urefu wa mita tano (mita 5) kwa ajili ya kujengea paa (canopy). Pia, utahitaji bomba za inchi moja au inchi 1.5 na bati kwa ajili ya kenchi na kuezeka (angalia Mchoro Na 2). Bomba za kenchi zinatakiwa kuwa na urefu wa mita saba (mita 7).

     Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa ujenzi:
     (a) Matenki ya kuhifadhia mafuta inabidi yafukiwe ardhini kwa umakini mkubwa. . Kwa sehemu ambazo maji ya ardhini (water table) yapo karibu, ni vizuri matenki yakajengewa zege.

     (b) Matenki yapakwe rangi ya kuzuia kutu. Pia, matenki yanatakiwa yafukiwe na mchanga kwa ajili ya kuzuia kutu.

     (c) Kituo kinatakiwa kisakafiwe kwa zege imara la angalau inchi nne (inchi 4). Eneo mahsusi la kusakafia ni eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta (angalia Mchoro Na 1). Eneo linalozunguka pampu liwe na ukubwa wa angalu mita za mraba 45 (yaani upana mita 6.4 na urefu mita 7). Eneo la kushushia mafuta linatakiwa liwe na ukubwa wa angalau mita za mraba 16 (yaani upana mita 4 na urefu mita 4) ili gari la mafuta liweze kusimama kwenye zege hiyo wakati wa kushusha mafuta.

     (d) Eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta ijengewe mitaro inayoelekea kwenda kwenye chemba ya kuchuja mafuta na maji (Oil/water separator). Chemba ya kuchuja mafuta na maji inatakiwa iwe na vyumba vitatu. Kila chumba kiwe na urefu wa mita moja (mita 1), upana mita mbili (mita 2) na kina mita moja (mita 1). Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo. Usitumie zege, ili iwe rahisi wakati wa kusafisha (angalia Mchoro Na 3).

     (e) Kituo kinatakiwa kiwe na paa imara (canopy) kama inavyoonyesha kwenye Mchoro Na 2. Paa linatakiwa kuwa na urefu wa mita 5.

     (f) Ni vyema kutumia wahandisi wa ujenzi au mafundi wenye uzoefu wa ujenzi wa vituo vya mafuta.

     3 Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini
     EWURA imeandaa Kanuni mahsusi kwa ajili ya ujenzi na biashara ya vituo vya mafuta vijijini. Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayetaka kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate kibali cha EWURA, baada ya kutuma maombi ya kupewa kibali hicho. Pia, kabla ya kuanza biashara, mwekezaji anatakiwa kuwa na leseni ya EWURA, ambayo hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote. Baada ya hapo, EWURA itakagua kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.

     Mchoro Na 1: Ramani ya Kituo cha mafuta inayoonyesha tenki, pampu, ofisi, barabara ya kuingia na kutoka kituoni.

     Mchoro Na 2: Picha ikionyesha paa la kituo (canopy).
     .

     Mchoro Na 2: Chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator)

     Mchoro Na 3: Picha namna chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator) inavyotakiwa kujengwa. Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo.

     1. Nashukuru kwa maelezo mazuri ya kufungua au kuanziasha kituo cha mafuta vijijini.
      Naomba kupata kipeperushi

     2. Ndugu Simon,
      Kituo cha mafuta maeneo ya vijijini vinakadiriwa kugharimu kati ya milioni 50-70. Hata hivyo gharama inaweza kubadilika kutokana na masuala mbalimnali ikiwemo gharama za malighafi. Vituo vya mijini gharama yake inategemea na ukubwa wa kituo
      Karibu

    1. jenzi wa Kituo cha mafuta inategemea eneo na ukubwa wa kituo cha mafuta unachohitaji. Yafuatayo ni masuala yenye gharama katika ujenzi wa kituo cha mafuta:
     1. Jengo la ofisi: Hii inategemea ukubwa wa Ofisi itakayojengwa. Quantity Surveyor (QS) anaweza kukupa gharama halisi za ujenzi baada ya kuona mchoro wa ofisi. Suala la msingi kuwe na ofisi na vyoo angalau viwili.
     2. Matenki ya kuhifadhi mafuta. Gharama zinategemea ukubwa wa matenki na idadi. Gharama ya tenki inaweza kuanzia Shilingi milioni 12 mpaka 20. Lakini ni vyema matenki uyatengeneze (fabrication) kwenye eneo ambalo utajenga kituo.
     3. Kujenga zege eneo la kituo (paving with concrete). Hii inategemea ukubwa wa eneo na jinsi eneo lilivyo. Endapo itahijika kusawazisha (levelling) gharama zinaongezeka. Kwa wastani zege inaweza kugharimu Shilingi milioni 30 – 40.
     4. Ujenzi wa Paa (canopy) hii inategemea ukubwa wa kanopi. Kwa wastani canopy inaweza kugharimu hadi Shilingi milioni 40-50.
     5. Pampu za kuuzia mafuta. Hii inatagemea idadi na aina ya pampu. Gharama ya pampu moja mpya inaweza kuanzia Shilingi milioni 10-50 kutegemea aina ya pampu,ukubwa na uimara.

     Kimsingi hivyo ndio vitu muhimu. Inapaswa kuwaona Wahandisi washauri na QS kwa ajili ya kupata gharama halisi.

     Karibu.

  1. Kufungua kituo wilayani au mijini inabidi kuwepo na utofauti wa kilomiter ngap au mita ngapi baina ya kituo nakituo?

   1. Ndugu Nigo,
    Hatua ya awali ni kufanya maombi ya kibali cha ujenzi kupitia mtandao katika mfumo uitwao LOIS, kwenye tovuti yetu.

    Karibu.

  1. Bwana Tito,
   Ada ya maombi ni tsh 10,000/ na malipo ya leseni inategemea na daraja lako la leseni, kiwango cha juu kabisa ni tsh 120,000/ kwa daraja A. Na inaendelea kushuka mpaka kufikia wiremen. Nakushauri upitie Kanuni za Ufungaji meme za mwaka 2019, zilizopo katika tovuti yetu, ukurusa wa Umeme.
   Kwa maelezo zaidi piga simu bure 0800110030
   Karibu

    1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
     Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

     1. Habari

      Mara nyingi tunajua bei ya petrol inavouzwa ila inakonunuliwa napataje kujua bei zake kwa kila msimu je natumia website gan kujua au link ipi au nifanyaje nipate kujua bei ya manunuzi

     2. Ndugu Joseph, ununuzi wa mafuta yanayotumika nchini hufanywa kwa pamoja kwa uratibu wa Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na mafuta hununuliwa katika soko la dunia. Pitia https://www.pbpa.go.tz/ ili uweze kupata taarifa zaidi.

      Karibu

  2. Tafadhali naomba nipate utaratibu mzima wa kufungua kituo kidogo cha mafuta mikoani(vijijini) ikijumuisha na gharama zote muhimu zinazohitajika

   1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
    Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

 2. Nimepata taarifa kuwa Ewura mmerahisisha taratibu za kujenga kituo cha mafuta kijijini kwa gharama nafuu tofauti na mjini. Naomba kujua vi vitu gani vya kuzingatia ili niweze kuwekeza kituo cha mafuta vijijini.

  1. Habari Sammy,
   Nakutumia kipeperushi kwa email ukipitie. Endapo utakuwa na swali lolote usisite kuwasiliana nasi. Pia unaweza kupiga simu bure kwa namba 0800110030

     1. Ndugu Gerald,
      Mwongozo huo ufuatao:-
      UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI

      UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI
      1. Utangulizi

      1.1 Mahitaji ya mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka. Ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama “boda boda”.

      1.2 Hata hivyo, maeneo mengi ya vijijini hayana vituo vya mafuta kutokana na ukweli kwamba, wawekezaji wa biashara hiyo wenye mitaji mikubwa husita kujenga vituo vya kuuzia mafuta Vijijini kwa kuona maeneo hayo hakuna biashara ya kutosha .

      1.3 Matokeo yake, wafanyabiashara wenye mitaji midogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta, huingia kwenye biashara hii. Kutokana na mitaji yao midogo na kutokuwa na uzoefu, wafanyabiashara hawa huanza kufanya biashara ya mafuta kwa kutumia miundo mbinu hafifu na isiyo salama kama vile kuhifadhi mafuta kwenye mapipa, madumu ya plastiki na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

      1.4 Uhifadhi wa mafuta kwa namna hiyo ni hatari kwa Usalama, Afya na Mazingira. Ni dhahiri kuna matukio mengi ya moto ambayo yamesababishwa na uhifadhi wa mafuta majumbani au kwenye vibanda vya biashara. Ajali hizo za moto, zimegharimu maisha ya watu na kuharibu mali. Pia, wafanyabishara katika maeneo hayo wako hatarini kupata magonjwa ya kansa ya ngozi kutokana na kushika mafuta wakati wa kutoa huduma hiyo. Kwa upande mwingine, mafuta humwagika ardhini na kuharibu mazingira.

      1.5 Kuhifadhi mafuta kutumia vyombo vya plastiki kunaharibu ubora wa mafuta hayo na hasa mafuta ya petroli. Mafuta na vyombo vya plastiki vina asili moja. Ubora wa mafuta ya petroli pia unaweza kuathiriwa na mwanga wa jua. Hivyo, vyombo vya moto vinavyo tumia mafuta yanayohifadhiwa kwenye vyombo vya plastiki viko hatarini kupata madhara kwa sababu ya kutumia mafuta ambayo hayana ubora unaohitajika.

      1.6 Biashara ya mafuta ya petroli ni muhimu sana, lakini ni hatari ikiwa itafanyika kiholela bila kufuata misingi ya usalama na viwango. Hivyo ni vyema mafuta ya petroli yakahifadhiwa na kuuzwa kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo. Lengo ni kulinda usalama, afya, ubora wa mafuta na mazingira.

      1.7 Moja ya miundombinu ambayo inatimiza lengo tajwa hapo juu ni vituo vya kuuzia mafuta. Sababu kubwa ni kuwa, kwenye kituo cha mafuta, matenki ya kuhifadhia mafuta yanafukiwa chini ya ardhi. Hivyo, hata moto ukitokea si rahisi mafuta yaliyo ndani ya matenki hayo kulipuka.

      1.8 Kipeperushi hiki kimelenga kutoa maelezo kwa kifupi juu ya ujenzi wa vituo vya gharama nafuu kwa kuelezea vitu muhimu na vya msingi vinavyotakiwa kuzingatiwa wakati wa kujenga kituo cha mafuta. Vilevile, Kipeperushi hiki kinaelezea Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini ambazo zilitungwa mahsusi kwa ajili ya kupunguza gharama za uwekezaji wa vituo hivyo.

      1.9 Ni lengo la EWURA kutengeneza mazingira ambapo watu wa Vijijini wanakuwa na haki sawa na watu wa Mijini katika upatikanaji wa bidhaa ya mafuta kwa hali ya ubora na usalama unaohitajika na kwa bei nafuu.

      1.10 Ni matumaini ya EWURA kwamba, Kipeperushi hiki kitatoa mwanga kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa mafuta ya petroli nchini namna ambavyo uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini unavyoweza kufanywa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watumiaji wa mafuta hayo kupata huduma nzuri zaidi na salama bila kumuathiri mfanyabiashara wa mafuta.

      2 Mahitaji na Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Ujenzi

      Ili uweze kujenga kituo unatakiwa kuzingatia yafutatayo:

      (a) Uwe na kiwanja ambacho Mamlaka husika (mfano: Halmashauri ya kijiji) imeridhia kitumike kwa ajili ya biashara ya kituo cha mafuta. Ili kukidhi viwango vya usalama (safety distance requirements), kiwanja kinachofaa kujenga kituo cha mafuta kinatakiwa angalau kiwe na ukubwa wa mita za mraba 400.

      (b) Uwe angalau na tenki moja (1) la kuhifadhia mafuta. Kama utauza aina zaidi ya moja ya mafuta, matenki yaongezeke sawia. Tenki liwe na ujazo wa angalau lita 4,500 au 5,000.
      Uwe na pampu yenye mkono mmoja au miwili kulingana na aina za mafuta.
      (c) Bomba nne (4) za chuma za inchi nne (inchi ) na urefu wa mita tano (mita 5) kwa ajili ya kujengea paa (canopy). Pia, utahitaji bomba za inchi moja au inchi 1.5 na bati kwa ajili ya kenchi na kuezeka (angalia Mchoro Na 2). Bomba za kenchi zinatakiwa kuwa na urefu wa mita saba (mita 7).

      Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa ujenzi:
      (a) Matenki ya kuhifadhia mafuta inabidi yafukiwe ardhini kwa umakini mkubwa. . Kwa sehemu ambazo maji ya ardhini (water table) yapo karibu, ni vizuri matenki yakajengewa zege.

      (b) Matenki yapakwe rangi ya kuzuia kutu. Pia, matenki yanatakiwa yafukiwe na mchanga kwa ajili ya kuzuia kutu.

      (c) Kituo kinatakiwa kisakafiwe kwa zege imara la angalau inchi nne (inchi 4). Eneo mahsusi la kusakafia ni eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta (angalia Mchoro Na 1). Eneo linalozunguka pampu liwe na ukubwa wa angalu mita za mraba 45 (yaani upana mita 6.4 na urefu mita 7). Eneo la kushushia mafuta linatakiwa liwe na ukubwa wa angalau mita za mraba 16 (yaani upana mita 4 na urefu mita 4) ili gari la mafuta liweze kusimama kwenye zege hiyo wakati wa kushusha mafuta.

      (d) Eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta ijengewe mitaro inayoelekea kwenda kwenye chemba ya kuchuja mafuta na maji (Oil/water separator). Chemba ya kuchuja mafuta na maji inatakiwa iwe na vyumba vitatu. Kila chumba kiwe na urefu wa mita moja (mita 1), upana mita mbili (mita 2) na kina mita moja (mita 1). Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo. Usitumie zege, ili iwe rahisi wakati wa kusafisha (angalia Mchoro Na 3).

      (e) Kituo kinatakiwa kiwe na paa imara (canopy) kama inavyoonyesha kwenye Mchoro Na 2. Paa linatakiwa kuwa na urefu wa mita 5.

      (f) Ni vyema kutumia wahandisi wa ujenzi au mafundi wenye uzoefu wa ujenzi wa vituo vya mafuta.

      3 Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini
      EWURA imeandaa Kanuni mahsusi kwa ajili ya ujenzi na biashara ya vituo vya mafuta vijijini. Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayetaka kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate kibali cha EWURA, baada ya kutuma maombi ya kupewa kibali hicho. Pia, kabla ya kuanza biashara, mwekezaji anatakiwa kuwa na leseni ya EWURA, ambayo hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote. Baada ya hapo, EWURA itakagua kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.

      Mchoro Na 1: Ramani ya Kituo cha mafuta inayoonyesha tenki, pampu, ofisi, barabara ya kuingia na kutoka kituoni.

      Mchoro Na 2: Picha ikionyesha paa la kituo (canopy).
      .

      Mchoro Na 2: Chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator)

      Mchoro Na 3: Picha namna chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator) inavyotakiwa kujengwa. Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo.

     2. Naomba kujua taratibu za kufungua Sheri kijijini email yangu ,kilasibarnaba18@gmail.com

     3. Ndugu Barnaba,
      Utaratibu wa kuwa na kituo cha mafuta maeneo ya kijijini ni huu ufuatatao:-
      1. Kuwa na eneo, lenye hati inayoonesha matumizi ya kituo cha mafuta. Hati inaweza kuwa ya kimila au hati ya kawaida au muhtasari wa kijiji kuidhinisha eneo kutumika kwa ujenzi wa kituo. Ukubwa wa eneo ni kuanzia mita za maraba 400.
      2.Barua ya tathmini ya Mazingira,kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Wilaya.
      3.Mchoro wa kituo, uliochorwa na mhandisi aliyeajiliwa.
      4. Namba ya mlipa kodi.
      Baada ya kukamilisha masuala haya, mwekezaji atapaswa kuomba kibali cha ujenzi EWURA kwa mfumo wa LOIS kupitia https://lois.ewura.go.tz/ewura/. Gharama ya kibali cha ujenzi kwa kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/
      Baada ya kupata kibali cha ujenzi, ujenzi utaanza na baada ya kukamilisha ujenzi, mwekezaji ataomba leseni EWURA kwa mfumo huo huo wa LOIS. Gharama za maombi ya leseni ya kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/ na ada ya leseni shilingi 100,000/

      Gharama zote hulipwa kwa mfumo wa Malipo Serikalini,kwa namba maalumu ya malipo atakayotumiwa mteja kwenye kila hatua inayohitaji malipo.

      Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kutupigia kwa namba 0800110030, bila gharama, siku za kazi Jumatatu hadi Ijumaa, saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

      Karibu

  2. Bwana Sammy karibu.
   Ni kweli. Tafadhali tupatie anuani ya barua pepe ili upate kipeperushi chenye maelezo husika.
   Karibu

     1. na Mimi pia naomba kipeperushi ni namna gani nitaanza biashara ya shell na gharama zake asanteni sana

     2. Bi Theresia, ni vituo vya mafuta sio shell.
      Tafadhali kipeperushi kimetumwa katika baraua pepe yako.
      Karibu

     3. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
      Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

     1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

      Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako. Karibu

    1. Ndugu Gerald,
     Gharama ya maombi ya leseni ni shilingi 10,000/
     Ada ya leseni inatofautiana kwa aina ya leseni kuanzia shilingi 40,000 mpaka 150,000/
     Ada zote hudumu kwa muda wa miaka mitatu.

     Asante

   1. Na Mimi naombeni kipeperushi kwa mtú ambae anataka kuwekeza maeneo ya kijijini na garama zake

    1. Ujenzi wa Kituo cha mafuta inategemea eneo na ukubwa wa kituo cha mafuta unachohitaji. Yafuatayo ni masuala zenye gharama katika ujenzi wa kituo cha mafuta:
     1. Jengo la ofisi: Hii inategemea ukubwa wa Ofisi itakayojengwa. Quantity Surveyor (QS) anaweza kukupa gharama halisi za ujenzi baada ya kuona mchoro wa ofisi. Suala la msingi kuwe na ofisi na vyoo angalau viwili.
     2. Matenki ya kuhifadhi mafuta. Gharama zinategemea ukubwa wa matenki na idadi. Gharama ya tenki inaweza kuanzia Shilingi milioni 12. Lakini ni vyema matenki uyatengeneze (fabrication) kwenye eneo ambalo utajenga kituo.
     3. Kujenga zege eneo la kituo (paving with concrete). Hii inategemea ukubwa wa eneo na jinsi eneo lilivyo. Endapo itahijika kusawazisha (levelling) gharama zinaongezeka. Kwa wastani zege inaweza kugharimu Shilingi milioni 30 – 40.
     4. Ujenzi wa Paa (canopy) hii inategemea ukubwa wa kanopi. Kwa wastani canopy inaweza kugharimu hadi Shilingi milioni 40-50.
     5. Pampu za kuuzia mafuta. Hii inatagemea idadi na aina ya pampu. Gharama ya pampu moja mpya inaweza kuanzia Shilingi milioni 10-15.

     Kimsingi hivyo ndio vitu muhimu. Inapaswa kuwaona Wahandisi washauri na QS kwa ajili ya kupata gharama halisi.

     Karibu.

     1. Utaratibu wa kuwa na kituo cha mafuta maeneo ya kijijini ni huu ufuatatao:-
      1. Kuwa na eneo, lenye hati inayoonesha matumizi ya kituo cha mafuta. Hati inaweza kuwa ya kimila au hati ya kawaida au muhtasari wa kijiji kuidhinisha eneo kutumika kwa ujenzi wa kituo. Ukubwa wa eneo ni kuanzia mita za maraba 400.
      2.Barua ya tathmini ya Mazingira,kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Wilaya.
      3.Mchoro wa kituo, uliochorwa na mhandisi aliyeajiliwa.
      4. Namba ya mlipa kodi.
      Baada ya kukamilisha masuala haya, mwekezaji atapaswa kuomba kibali cha ujenzi EWURA kwa mfumo wa LOIS kupitia https://lois.ewura.go.tz/ewura/. Gharama ya kibali cha ujenzi kwa kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/
      Baada ya kupata kibali cha ujenzi, ujenzi utaanza na baada ya kukamilisha ujenzi, mwekezaji ataomba leseni EWURA kwa mfumo huo huo wa LOIS. Gharama za maombi ya leseni ya kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/ na ada ya leseni shilingi 100,000/

      Gharama zote hulipwa kwa mfumo wa Malipo Serikalini,kwa namba maalumu ya malipo atakayotumiwa mteja kwenye kila hatua inayohitaji malipo.

      Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kutupigia kwa namba 0800110030, bila gharama, siku za kazi Jumatatu hadi Ijumaa, saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

  3. Tafadhali na mimi naomba nakala ya kipeperushi cha kufuata ili kufungua kituo cha mafuta kijijini ,
   Asante

   1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
    Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

   2. Tafadhali na mimi naomba nakala ya kipeperushi cha kufuata ili kufungua kituo cha mafuta kijijini ,
    Asante

 3. Hello.
  Lubricants Wholesale Business Licence inachukua mda gani mpaka kukamilika ikiwa documents zote ziko kamili?

  1. Bwana Kijika,
   Leseni hutolewa ndani ya siku 30 za kazi baada ya kupokea maombi kamili. Endapo una suala au changamoto yoyote wasiliana nasi na unaweza kupiga simu bure 0800110030.
   Karibu

  2. Bwana Kijika,
   Kwa mujibu wa mkataba wetu wa huduma, Leseni hutolewa ndani ya siku 30 za kazi tangu tarehe ya kupokea maombi yaliyo kamili.
   Karibu

    1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
     Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

 4. Habari, ningependa kujua utaratibu na documents zinazotumika kuomba kibali au leseni ya kufanya biashara ya kuuza vilainishi/ lubricants kwa kampuni. Kama kuna kipeperushi tafadhali naomba nisaidiwe.
  Asante

 5. Naomba kujua garama za kuanzisha kituo kidogo cha mafuta nalenga boda boda na baadhi ya magari kwa upande wa vijijini.maana nimesikia kuna gharama kidogo nafuu.

  1. Ndugu Kafyome,
   Tfadhali,makadirio ya gharama ni takribani milioni 55. Hata hivyo gahrama hii inaweza kuzidi kidogo au kupungua kwa sababu mbalimbali.
   Naomba utume anuani yako ya barua pepe ili tukutumie maelezo husika.
   Asante

     1. Maombi hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu na kubofya LOIS, kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

      Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako.

    1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
     Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

   1. Tafadhali naomba kupata makadirio ya uanzishaji wa kituo kidogo cha mafuta kijijini na utaratibu wake. Nalenga watu wa bodaboda na magari pia mashine za kusaga.
    Email yangu ni jsumni@gmail.com

 6. Hellow ewura ,
  Good job,ina eneo langu njia ya kuelekea msumi mbezi DSM ina mapango wa kujenga kituo cha mafuta.naomba kufahamishwa taratibu za kuanza kujenga Hadi nafungua kituo .thanks
  Good job

  1. Ndugu Mlay,
   Karibu
   Tafadhali angalia barua pepe maelezo ya utaratibu yametumwa kwa rejea yako.
   Asante

 7. Habari za Asubuhi
  Hongereni kwa kazi kubwa mnayofanya
  Naomba kuuliza: Nina mpango kwa kuanzisha Kituo Kidogo cha Mafuta au pump kwa ajili ya kuhudumia watu wa Kijijini kwani Sheli zipo mbali. Naomba kupata utaratibu ili niweze kujua kama nitaweza.

 8. Habari, Ewura kulikuwa na mpango wa kuanza kutoa vibali kwa ajili ya uanzishwaji wa mobile petrol station (Guta Petrol Station) haswa kwa maeneo ya vijijini. Tafadhali naweza kupata maelezo zaidi juu ya utolewaji wa leseni ya vituo hivyo vya mafuta na taratibu za kufuatwa. Na je Fuel dispenser ya aina yoyote inaweza kutumika katika uuzaji wa mafuta au kuna aina za dispenser ndio zinazokidhi vigezo?. Na naomba kupata kipeperushi cha uanzishaji wa kituo cha mafuta vijijini.
  email masaganya07@hotmail.com

  1. Ndugu George,
   Utaratibu wa vituo tembezi (mobile petrol stations) bado haujakamilika. Utakapokuwa tayari au vinginevyo taarifa itatolewa. Kuhusu kipeperushi,tafadhali rejea ktk barua pepe yako.
   Kwa maelezo zaidi piga 080011030 BURE
   Asante

   1. Hello habari Ewura

    Niko interested na kupata maelezo ya kuwa na hizi mobile fuel station, na pia hiyo namba ambayo ni ya huduma kwa mteja haipatikani. tunaomba msaada zaidi

    Pia namimi naomba kupata nakala ya maelezo ya hizo petrol station ndogo vijijini.

  1. Ndugu Mohamed,
   Ukubwa wa eneo inategemea aina ya kituo na mahali kinapojengwa. Kwa maeneo ya vijini ni kuanzia mita za mraba 400.
   Kwa maelezo zaidi tupigie 0800110030 bila gaharama.
   Karibu

    1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

     Kipeperushi kimetumwa katika barua pepe yako. Karibu

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

 9. Habari,
  Naomba kujua utaratibu wa kujenga mpaka kufungua kituo cha mafuta kwa Dar es salaam na mkoani.
  Asante.

  1. Ndugu Jane,
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako. Utaratibu huu unatumika ni kwa maeneo yote. Tofauti ni katika aina ya kituo na eneo linalohtajika. Kwa maeneo ya Dar es Salaam, ukubwa wa eneo ni kuanzia sq 1500 mpaka 2400.

   Aidha, Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Karibu.

 10. Naomba kuuliza ukitaka kuanzisha utoaji wa mafuta katika maeneo Ya kijijini vigezo vikoje na gharama zake zikoje?

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako

 11. Habari Ewura, niko kwenye utafiti wa gharama za kujenga kituo cha mafuta mjini , gharama zisiuhusishe eneo. Nimejaribu kutafuta mwenyewe nimepata majibu mchanganyiko. Naomba msaada tafadhari.

  1. Ndugu James,
   Hongera kwa kazi hiyo.
   Tunashauri utupatie majibu mchanganyiko uliyopata ili tuweze kubaini endapo umepata majibu sahihi ama la.
   Hata hivyo, Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

 12. Tafadhali naomba nipate utaratibu mzima wa kufungua kituo kidogo cha mafuta mikoani(vijijini) ikijumuisha na gharama zote muhimu zinazohitajika

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.wura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/
   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.

 13. Naomba kipeperushi chenye utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta vijijini. Niliomba hapo kabla kwenye uzi wa mtu mwingine. Pia kama utaratibu wa kuuza kwa kutumia guta/kirikuu kama umekamilika tafadhali ambatanisha vipeperushi vyote. Asante

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako.
   Utaratibu wa vituo tembezi bado haujakamilika. Karibu

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako. Karibu

  1. Maombi ya leseni hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu http://www.ewura.go.tz; kisha bofya LOIS kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

   Maelezo ya utaratibu wa kuanzisha kituo cha mafuta umetumwa katika barua pepe yako. Karibu

 14. Habari za leo Muheshimiwa, Eweru ningependa kupata information zozote kuhusu kufungua kituo cha mafuta mjini na kijijini pia. Ikiwa nchini au nchini jirani hususani nchi toka Maziwa Makuu. Na nijinsi gani pia mnaweza kusaidia kufanikisha swala la ufunguaji kituo cha mafuta.

  1. Maombi hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki unaitwa LOIS.Tafadhali ingia katika website yetu na kubofya LOIS, kujisajili na kuendelea kufanya maombi. Unaweza pia kutumia kiunganishi hiki—https://lois.ewura.go.tz/ewura/

   Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako.

 15. Mimi nipo nyumba ya mungu, Simanjiro, naomba muongozo wa hatua ninazopaswa kufuata ninapotaka kufungua kituo cha mafuta, napenda kujua procedures na gharama za ada za serikali. Tayari nimeshachimba visima vya kuweka matanki

 16. Hata mm nahtaji kujua taratbu za kujenga kituo cha mafuta kijijin naomba msaaada wa maelekezo na gharama zpo vp

 17. Habari.
  Tafadhali naomba kupatiwa utaratibu wa kupata lesini ya uuzaji wa mafuta ya petroli na dizeli kwa njia ya mobile (yaani kuuza mafuta bila kua na kituo cha mafuta yaani kwa kutumia gari yenye tenki na pampu)

 18. Habari,
  Nimeomba Construction approval kwa ajili ya kituo caha mafuta , nimefuatilia hatua na kuona ipo hatua ya Review and Approval , je baada ya hatua io kuna hatua zaidi , na kama zipo bado ngapi hadi kuweza kupata kibari cha ujenzi !
  Asante
  Sanga .

 19. Habari team EWURA.
  Mimi ni mdau wa sekta ya mafuta.Napenda kufahamu sasa muongozo kamili na gharama za kuanzisha kituo cha mafuta kwa mjini na ama kijijini kiwe kikubwa au kidogo.

  Nitashkuru ombo langu likifanyiwa kazi na kupata majibu

 20. Habari, ninaitwa Nelson tafadhali naomba kujua taratibu za kufuata pamoja na ada husika ili kuweza kupata kibali cha kuuza mafuta (yaani petroli na dizeli) kwa njia ya mobile (kwa kutumia gari zenye tanki zilizofungwa pampu). Asante.

 21. Habari kiongozi naweza pata muongozo wa wauzaji mafuta wadogo na wanahitajika kukamilisha vitu gani ili waweze kupata leseni ya biashara hiyo

 22. Nathamini na kuheshimu kazi nzuri ambazo EWURA imekuwa ikifanya kwa maendeleo ya Taiga letu. Naomba nisaidiwe kipeperushi cha kufahamu namna ya uanzishaji na ufunguaji wa kituo cha mafuta vijijini.

 23. Naomba kipeperushi Cha maelekezo ya kuanzisha kituo Cha Mafuta kijijini. Na Kama naweza kupata makadirio ya gharama za uanzishaji. Nahitaji Sana.

 24. Naomba kujua utaratibu wa vituo vya mafuta kuuziana mafuta kwa mujibu wa sheria umekaaje naomba msaada hilo jambo.

  1. Ndugu Alson, vituo vya mafuta kuuziana mafuta haina tatizo kwa sababu ni maelewano yao. Jambo la msingi ni kuhakikisha katika kufanya hivyo hawavunji sheria. Hata hivyo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 26(2)(b)(ii) cha Kanuni za Bidhaa za Mafuta (Jumla, Rejareja, Kuhifadhi na Matumizi Binafsi),Tangazo la Serikali Na . 817 la mwaka 2020, kila mmoja anapaswa kuingia mkataba wa mauziano ya mafuta na wauzaji wa mafuta kwa ujumla.
   Karibu

 25. Habari za leo, naomba kupewa utaratibu wa kuanzisha na kusajili kituo cha uuzaji mafuta (petrol na diesel) kijijini. Ingekuwa vyema nikaelekezwa hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ikiwa tayari nina eneo ambalo ndilo natarajia kulitumia kwa shughuli/biashara hiyo. Pamoja na uwanja huu ni vyema nipewe majibu kwa barua pepe yangu. Asante

 26. Hello
  Nahitaji kuanzisha kituo Kidogo cha mafuta (Mini Petrol Station) Kigoma vijijini. Nisaidieni hatua za kufuata, sample bajeti structure, kusajili na kupata leseni

  1. Ndugu Mawazo,
   Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako.
   Endapo utahitaji taarifa zaidi usisiste kuwasiliana nasi.
   Karibu

  1. Ndugu Michael,
   Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako, hata hivyo, maeneo ya vijijini na mijini ni ukubwa wa eneo ambao kwa mjini ni mita za mraba 1200 hadi 2400 kulingana na aina ya kituo kinachokusudiwa kujengwa.
   Endapo utahitaji taarifa zaidi usisiste kuwasiliana nasi.
   Karibu

 27. habari za leo,
  Ninalo eneo ambalo ningependa kufungua kituo cha kuuzia mafuta na spear parts.

  Hivyo naomba kujua utaratibu kuanzia mwanzo hadi mwisho pamoja na gharama zake. Eneo lipo pugu dar es salaam

  1. Ndugu Jacquiline,
   Utaratibu umetumwa katika barua pepe yako, hata hivyo, maeneo ya vijijini na mijini ni ukubwa wa eneo ambao kwa mjini ni mita za mraba 1200 hadi 2400 kulingana na aina ya kituo kinachokusudiwa kujengwa.
   Endapo utahitaji taarifa zaidi usisiste kuwasiliana nasi.
   Karibu

 28. Habari, naomba kufahamu kuna maeneo yanahesabika yapo mjini lakini kiuhalisia ni kijijini kabisa. Kwa mfano kayenze mwanza. Inahesabika iko ndani ya manispaa ya ilemela lakini kwa waopajua ni kijijini kabisa. Hapo inakaaje kuhusu lile swala la leseni zenu za kurahisisha huduma kwa wanakijiji kama hao? Masharti yatabaki yale yale kama ya kituo cha mjini?

  1. Ndugu Samwel,

   Pokea kama ifuatavyo:-

   UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI

   UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI
   1. Utangulizi

   1.1 Mahitaji ya mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka. Ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama “boda boda”.

   1.2 Hata hivyo, maeneo mengi ya vijijini hayana vituo vya mafuta kutokana na ukweli kwamba, wawekezaji wa biashara hiyo wenye mitaji mikubwa husita kujenga vituo vya kuuzia mafuta Vijijini kwa kuona maeneo hayo hakuna biashara ya kutosha .

   1.3 Matokeo yake, wafanyabiashara wenye mitaji midogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta, huingia kwenye biashara hii. Kutokana na mitaji yao midogo na kutokuwa na uzoefu, wafanyabiashara hawa huanza kufanya biashara ya mafuta kwa kutumia miundo mbinu hafifu na isiyo salama kama vile kuhifadhi mafuta kwenye mapipa, madumu ya plastiki na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

   1.4 Uhifadhi wa mafuta kwa namna hiyo ni hatari kwa Usalama, Afya na Mazingira. Ni dhahiri kuna matukio mengi ya moto ambayo yamesababishwa na uhifadhi wa mafuta majumbani au kwenye vibanda vya biashara. Ajali hizo za moto, zimegharimu maisha ya watu na kuharibu mali. Pia, wafanyabishara katika maeneo hayo wako hatarini kupata magonjwa ya kansa ya ngozi kutokana na kushika mafuta wakati wa kutoa huduma hiyo. Kwa upande mwingine, mafuta humwagika ardhini na kuharibu mazingira.

   1.5 Kuhifadhi mafuta kutumia vyombo vya plastiki kunaharibu ubora wa mafuta hayo na hasa mafuta ya petroli. Mafuta na vyombo vya plastiki vina asili moja. Ubora wa mafuta ya petroli pia unaweza kuathiriwa na mwanga wa jua. Hivyo, vyombo vya moto vinavyo tumia mafuta yanayohifadhiwa kwenye vyombo vya plastiki viko hatarini kupata madhara kwa sababu ya kutumia mafuta ambayo hayana ubora unaohitajika.

   1.6 Biashara ya mafuta ya petroli ni muhimu sana, lakini ni hatari ikiwa itafanyika kiholela bila kufuata misingi ya usalama na viwango. Hivyo ni vyema mafuta ya petroli yakahifadhiwa na kuuzwa kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo. Lengo ni kulinda usalama, afya, ubora wa mafuta na mazingira.

   1.7 Moja ya miundombinu ambayo inatimiza lengo tajwa hapo juu ni vituo vya kuuzia mafuta. Sababu kubwa ni kuwa, kwenye kituo cha mafuta, matenki ya kuhifadhia mafuta yanafukiwa chini ya ardhi. Hivyo, hata moto ukitokea si rahisi mafuta yaliyo ndani ya matenki hayo kulipuka.

   1.8 Kipeperushi hiki kimelenga kutoa maelezo kwa kifupi juu ya ujenzi wa vituo vya gharama nafuu kwa kuelezea vitu muhimu na vya msingi vinavyotakiwa kuzingatiwa wakati wa kujenga kituo cha mafuta. Vilevile, Kipeperushi hiki kinaelezea Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini ambazo zilitungwa mahsusi kwa ajili ya kupunguza gharama za uwekezaji wa vituo hivyo.

   1.9 Ni lengo la EWURA kutengeneza mazingira ambapo watu wa Vijijini wanakuwa na haki sawa na watu wa Mijini katika upatikanaji wa bidhaa ya mafuta kwa hali ya ubora na usalama unaohitajika na kwa bei nafuu.

   1.10 Ni matumaini ya EWURA kwamba, Kipeperushi hiki kitatoa mwanga kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa mafuta ya petroli nchini namna ambavyo uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini unavyoweza kufanywa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watumiaji wa mafuta hayo kupata huduma nzuri zaidi na salama bila kumuathiri mfanyabiashara wa mafuta.

   2 Mahitaji na Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Ujenzi

   Ili uweze kujenga kituo unatakiwa kuzingatia yafutatayo:

   (a) Uwe na kiwanja ambacho Mamlaka husika (mfano: Halmashauri ya kijiji) imeridhia kitumike kwa ajili ya biashara ya kituo cha mafuta. Ili kukidhi viwango vya usalama (safety distance requirements), kiwanja kinachofaa kujenga kituo cha mafuta kinatakiwa angalau kiwe na ukubwa wa mita za mraba 400.

   (b) Uwe angalau na tenki moja (1) la kuhifadhia mafuta. Kama utauza aina zaidi ya moja ya mafuta, matenki yaongezeke sawia. Tenki liwe na ujazo wa angalau lita 4,500 au 5,000.
   Uwe na pampu yenye mkono mmoja au miwili kulingana na aina za mafuta.
   (c) Bomba nne (4) za chuma za inchi nne (inchi ) na urefu wa mita tano (mita 5) kwa ajili ya kujengea paa (canopy). Pia, utahitaji bomba za inchi moja au inchi 1.5 na bati kwa ajili ya kenchi na kuezeka (angalia Mchoro Na 2). Bomba za kenchi zinatakiwa kuwa na urefu wa mita saba (mita 7).

   Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa ujenzi:
   (a) Matenki ya kuhifadhia mafuta inabidi yafukiwe ardhini kwa umakini mkubwa. . Kwa sehemu ambazo maji ya ardhini (water table) yapo karibu, ni vizuri matenki yakajengewa zege.

   (b) Matenki yapakwe rangi ya kuzuia kutu. Pia, matenki yanatakiwa yafukiwe na mchanga kwa ajili ya kuzuia kutu.

   (c) Kituo kinatakiwa kisakafiwe kwa zege imara la angalau inchi nne (inchi 4). Eneo mahsusi la kusakafia ni eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta (angalia Mchoro Na 1). Eneo linalozunguka pampu liwe na ukubwa wa angalu mita za mraba 45 (yaani upana mita 6.4 na urefu mita 7). Eneo la kushushia mafuta linatakiwa liwe na ukubwa wa angalau mita za mraba 16 (yaani upana mita 4 na urefu mita 4) ili gari la mafuta liweze kusimama kwenye zege hiyo wakati wa kushusha mafuta.

   (d) Eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta ijengewe mitaro inayoelekea kwenda kwenye chemba ya kuchuja mafuta na maji (Oil/water separator). Chemba ya kuchuja mafuta na maji inatakiwa iwe na vyumba vitatu. Kila chumba kiwe na urefu wa mita moja (mita 1), upana mita mbili (mita 2) na kina mita moja (mita 1). Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo. Usitumie zege, ili iwe rahisi wakati wa kusafisha (angalia Mchoro Na 3).

   (e) Kituo kinatakiwa kiwe na paa imara (canopy) kama inavyoonyesha kwenye Mchoro Na 2. Paa linatakiwa kuwa na urefu wa mita 5.

   (f) Ni vyema kutumia wahandisi wa ujenzi au mafundi wenye uzoefu wa ujenzi wa vituo vya mafuta.

   3 Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini
   EWURA imeandaa Kanuni mahsusi kwa ajili ya ujenzi na biashara ya vituo vya mafuta vijijini. Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayetaka kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate kibali cha EWURA, baada ya kutuma maombi ya kupewa kibali hicho. Pia, kabla ya kuanza biashara, mwekezaji anatakiwa kuwa na leseni ya EWURA, ambayo hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote. Baada ya hapo, EWURA itakagua kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.

   Mchoro Na 1: Ramani ya Kituo cha mafuta inayoonyesha tenki, pampu, ofisi, barabara ya kuingia na kutoka kituoni.

   Mchoro Na 2: Picha ikionyesha paa la kituo (canopy).
   .

   Mchoro Na 2: Chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator)

   Mchoro Na 3: Picha namna chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator) inavyotakiwa kujengwa. Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo.

  1. Ndugu Mudhihiri,
   Leseni za biashara ya bidhaa za petroli hutolewa kwa aina ya biashara na si kwa daraja.
   Asante

 29. Nina milioni 8 kwenye akaunti! Ninaweza kuanzia kituo cha kuuzia mafuta-petrol tu hapa kijijini kwetu? Naomba msaada.

  1. Ndugu Moses,
   Kiasi hicho cha pesa hakitoshi kwa bishara unayotarajia kufanya.
   Nakushauri uangali fursa nyingine kama kuwa wakala wa gesi ya kupikia ama vilainishi ili ukuze mtaji kidogo ili uweze kuanzisha hiyo bishara.
   Tafadhali pokea kipeperushi katika barua pepe yako kupata maelezo ya uanzishwaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini.
   Karibu

   1. Umeeleza vizuri vigezo na masharti nimekuelewa lakini mkuu kiwango cha pesa tunahitaji kujua ni shingapi kwa wafanya biashara wadogo wa vituo vya mafuta kwa vijijini ili tuweze kujiwekeza mfano pump shingapi au ujenzi unaghalimu shingapi

 30. Hongera kwa kazi. Je. Ewura mnamikataba ambayo mnaweza ingia na mtu na kumfadhiri hela kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta(kijiji) . Kama huduma hiyo mnayo naomba ufafanuzi kama hamna pia naomba muongozo ni kina nan wanahusika. Sory reply via dausonbuninange@yahoo.com

  1. Ndugu Dauson,
   Tunapenda kukufahamisha kwamba EWURA haitoi huduma hiyo.
   Unaweza kujaribu kuwasiliana na wenye makamouni ya mafuta huenda ukapata ufumbuzi.
   Karibu.

 31. Naomba kufahamu kwanini kunaongezeko kubwa la vituo vya mafuta katika maeneo ya makazi ya watu Jijini Dar es Salaam. Je, ile hatari ya milipuko na athari zingine kwa mali na maisha ya binadamu hivi sasa haipo tena?

  Vituo vingi vilivyojengwa njia ya Kigogo-Ubungo Maziwa, External-Maji Chumvi viko katikati ya makazi ya watu.

  Mamlaka zinazohusika zinasubiri maafa gani?

  1. Ndugu Edgar,
   Vituo vya mafuta hujengwa kwa mujibu wa utaratibu na kabla ya kutoa kibali cha ujenzi, EWURA hujiridhisha kwamba taratibu zote zimezingatiwa. Vilevile, suala la usalama, mazingira na afya huzingatiwa kabla ya kibali husika kutolewa. Vilevile, baada ya kituo kuanza kazi, EWURA hufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kujiridhusha kuwa kanuni za uendeshaji vituo, ubora wa miundombinu na huduma vinazingatiwa.

   Karibu

 32. Nahitaji pdf nzima ya hatuavza kufuata ili kuanzisha kituo Cha mafuta mjini au vijijini. Full pdf document

 33. Hongera EWURA kwa kazi nzuri, naomba kipeperushi kinachohusu UJENZI WA VITUO VYA VYA KUUZIA MAFUTA REJAREJA VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI

  1. Ndugu Anthony,
   Makadirio ya gharama ni shs milioni 50. inaweza kuongezeka kutokana na masuala mbalimbali. Aidha EWURA imepunguza ada ya leseni kwa asilimia 90 kwa vituo vya kijijini.

   Karibu

 34. Naomba Kujua Utaratibu wa kupata kibali cha kufungua kituo cha Mafuta (Sheli) kwa upande wa vijijin au semi-town. Na Gharama zake zipoje

 35. Habari
  Naomba kipeperushi chenye maelekezo ya kujenga kuanzisha kituo cha mafuta kijijini.

 36. Habari naomba kujua,
  mtaji shilingi ngapi unahitajika kuanza biashara ya mafuta ya petrol, diesel na kerosene na je ujenzi wa hapa dar es salaam sheli inatakiwa kuwa na kiwango cha shillingi ngapi pia na kwa mkoa wa pwani pia

  1. Ms Harrieth
   Ujenzi wa Kituo cha mafuta inategemea eneo na ukubwa wa kituo cha mafuta unachohitaji. Yafuatayo ni masuala zenye gharama katika ujenzi wa kituo cha mafuta:
   1. Jengo la ofisi: Hii inategemea ukubwa wa Ofisi itakayojengwa. Quantity Surveyor (QS) anaweza kukupa gharama halisi za ujenzi baada ya kuona mchoro wa ofisi. Suala la msingi kuwe na ofisi na vyoo angalau viwili.
   2. Matenki ya kuhifadhi mafuta. Gharama zinategemea ukubwa wa matenki na idadi. Gharama ya tenki inaweza kuanzia Shilingi milioni 12. Lakini ni vyema matenki uyatengeneze (fabrication) kwenye eneo ambalo utajenga kituo.
   3. Kujenga zege eneo la kituo (paving with concrete). Hii inategemea ukubwa wa eneo na jinsi eneo lilivyo. Endapo itahijika kusawazisha (levelling) gharama zinaongezeka. Kwa wastani zege inaweza kugharimu Shilingi milioni 30 – 40.
   4. Ujenzi wa Paa (canopy) hii inategemea ukubwa wa kanopi. Kwa wastani canopy inaweza kugharimu hadi Shilingi milioni 40-50.
   5. Pampu za kuuzia mafuta. Hii inatagemea idadi na aina ya pampu. Gharama ya pampu moja mpya inaweza kuanzia Shilingi milioni 10-15.

   Kimsingi hivyo ndio vitu muhimu. Inapaswa kuwaona Wahandisi washauri na QS kwa ajili ya kupata gharama halisi.

   Karibu.

 37. Naomba kutumiwa mchanganuo wa bei za ujenzi wa kituo cha mafuta
  Mchanganuo wa bei za mafuta kutoka kwa suppliers
  Na vigezo gani vinahitajika ili kupewa leseni ya kifanya biashara hii

  1. Utaratibu wa kuwa na kituo cha mafuta maeneo ya kijijini ni huu ufuatatao:-
   1. Kuwa na eneo, lenye hati inayoonesha matumizi ya kituo cha mafuta. Hati inaweza kuwa ya kimila au hati ya kawaida au muhtasari wa kijiji kuidhinisha eneo kutumika kwa ujenzi wa kituo. Ukubwa wa eneo ni kuanzia mita za maraba 400.
   2.Barua ya tathmini ya Mazingira,kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Wilaya.
   3.Mchoro wa kituo, uliochorwa na mhandisi aliyeajiliwa.
   4. Namba ya mlipa kodi.
   Baada ya kukamilisha masuala haya, mwekezaji atapaswa kuomba kibali cha ujenzi EWURA kwa mfumo wa LOIS kupitia https://lois.ewura.go.tz/ewura/. Gharama ya kibali cha ujenzi kwa kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/
   Baada ya kupata kibali cha ujenzi, ujenzi utaanza na baada ya kukamilisha ujenzi, mwekezaji ataomba leseni EWURA kwa mfumo huo huo wa LOIS. Gharama za maombi ya leseni ya kituo cha kijijini ni shilingi 50,000/ na ada ya leseni shilingi 100,000/

   Gharama zote hulipwa kwa mfumo wa Malipo Serikalini,kwa namba maalumu ya malipo atakayotumiwa mteja kwenye kila hatua inayohitaji malipo.

   Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kutupigia kwa namba 0800110030, bila gharama, siku za kazi Jumatatu hadi Ijumaa, saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

   Karibu

  2. Pia,jenzi wa Kituo cha mafuta inategemea eneo na ukubwa wa kituo cha mafuta unachohitaji. Yafuatayo ni masuala zenye gharama katika ujenzi wa kituo cha mafuta:
   1. Jengo la ofisi: Hii inategemea ukubwa wa Ofisi itakayojengwa. Quantity Surveyor (QS) anaweza kukupa gharama halisi za ujenzi baada ya kuona mchoro wa ofisi. Suala la msingi kuwe na ofisi na vyoo angalau viwili.
   2. Matenki ya kuhifadhi mafuta. Gharama zinategemea ukubwa wa matenki na idadi. Gharama ya tenki inaweza kuanzia Shilingi milioni 12. Lakini ni vyema matenki uyatengeneze (fabrication) kwenye eneo ambalo utajenga kituo.
   3. Kujenga zege eneo la kituo (paving with concrete). Hii inategemea ukubwa wa eneo na jinsi eneo lilivyo. Endapo itahijika kusawazisha (levelling) gharama zinaongezeka. Kwa wastani zege inaweza kugharimu Shilingi milioni 30 – 40.
   4. Ujenzi wa Paa (canopy) hii inategemea ukubwa wa kanopi. Kwa wastani canopy inaweza kugharimu hadi Shilingi milioni 40-50.
   5. Pampu za kuuzia mafuta. Hii inatagemea idadi na aina ya pampu. Gharama ya pampu moja mpya inaweza kuanzia Shilingi milioni 10-15.

   Kimsingi hivyo ndio vitu muhimu. Inapaswa kuwaona Wahandisi washauri na QS kwa ajili ya kupata gharama halisi.

   Karibu.

 38. Naomba maelekezo jinsi ya kuomba kibali cha ujenzi wa kituo cha mafuta kijijini kutoka EWURA naomba uni tumie muongozo kwenye email yangu pia

 39. Mm niko tabora heneo ninaro ni nusu heka kijijini kulipia vbali ela ninayo hila mtaji wakujenga kituo ndio sina nafanyaje kupata mkopo wakujenga kijijin kwetu pikipik zipo nyingi sana napend kutua huduma hiyo yakujenga sheli hila mtaji sina nikipata hata kesho najenga

  1. Ndugu Maganga,

   Mikopo ya kuwezesha ujenzi wa vituo maeneo ya vijijini linasimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijin yaani REA. Unaweza kuwapigia simu +255 26 2323504, +255 26 2323506 au kutembelea ofisi za REA Dodoma, Jengo la LAPF.
   Karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *