TAARIFA KWA UMMA: Amri kwa Wamiliki wa Majengo ya Makazi na Biashara kuhusu Bei za Umeme

EWURA yatoa AMRI kwa wamiliki wa majengo ya makazi na biashara kwamba bei za umeme kwa ajili ya wapangaji wao zisizidi  zilizoidhinishwa na  Mamlaka. Soma Zaidi:-

Amri -Bei za Umeme -Kiswahili

The ORDER – Electricity tariff -English

 

Hits: 480

10 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA: Amri kwa Wamiliki wa Majengo ya Makazi na Biashara kuhusu Bei za Umeme

  1. Mfumo wa usajili mtandaoni siyo rafiki kabisa kwa watumiaji,sababu ni kuwa elimu ya kutosha haijatolewa,Mfano ni Mimi mwenyewe nimefika ofisi ya Ewura niweze kurenew leseni yangu naambiwa siku hizi ni online,mifumo yote ni mipya hii,ni mwezi sasa kila nikijaribu nakwamia mahali kama muomaji mpya,nashauri watu ealiokwisha kupata leseni wawe na fomu mpya inayoonesha namba ya leseni ya zamanj ili kupunguza mlolongo mrefu kwa watu ambao ewura ina taarifa nao na hawabadili daraja la leseni.

    1. Ndugu Ibrahim,
      Pole kwa changamoto na asante sana kwa mrejesho huu. Tungependa kufahamu ulitembelea ofisi ya EWURA iliyopo mkoa gani na utupate namba yako ya simu ili tuwasiliane kufahamu changamoto uliyoipata.
      Vilevile unaweza kupiga simu 0800110030 (BURE) ili uweze kuungamishwa na mtaalam.
      Karibu

  2. Kwa wakazi wa Dsm, tunanunua units 280 kwa 100,000/=.

    Average ni tzs 353 kwa unit…

    Sijaelewa nipo D1 au T1..?

    Je hizo bei mlizoziweka zimejumlisha na tax au ni bei ya tanesco tu

    1. Bwana Leo,
      Tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako ambaye ni TANESCO ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo. Endapo hutaridhirika, baada ya kuwasiliana nao; utuandikie kwa hatua zaidi, huku ukimpatia nakala mtoa huduma.
      Asante

    1. Ndugu Audax,
      Maombi yote ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao. Tafadhali bofya neno LOIS, upande wa kulia wa tovuti yetu, itakupeleka katika mfumo wa maombi. Jisajili na kisha endelea kufuata maelekezo.
      Unaweza pia kusoma namna ya kutumia LOIS kwa kubofya Online Services.
      Karibu

  3. Kama mtu amekidhi vigezo vyote, kwa kawaida huchukua muda gani kwa mtu anayetaka ku upgrade leseni yake kutoka daraja moja kwenda nyingine?

  4. Pia nahitaji kufaham ntapataje sheria ya EWURA? naamini itanisaidia kujua mipaka yangu ni ipi ninapokuwa na LESENI YA EWURA na pia nitajua ni upi wajibu wangu katika kuelimisha jamii

    1. Mhandisi Peniel,
      Leseni huchukua siku 30 za kazi tangu kupokelewa kwa maombi kamili.
      Endapo muda huo umepita na hukupata mrejesho tafadhali tupigie 0800110030(bure) ili uweze kuunganishwa na anayeshughulikia masuala ya leseni.

    2. Sheria ya EWURA ipo katika tovuti yetu.
      Pia unaweza kusoma sheria zote katika kurasa za kila sekta katika tovuti yetu, katika kila eneno lilioandikwa regulatory tools.
      Mfano. Bofya electricity, select regulatory tools–utasoma, sheria, kanuni na miongozo katika eneo hilo.
      Sekta nyingine vivyo hivyo.
      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *