Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli.
Soma Zaidi:-Mwito wa Maoni-Maombi ya Leseni
Hits: 398
Kwakweii bei za umeme wa bower gen no wizi mtupu kama wanatuletea meseji umeme. Wanauza sh 1 kwa yunit moja vipi tunalipa 800 kila siku na umeme haufiki Massa 24 unatumika. Massa 8 tu has a kata ya itaswi mweshimiwa raisi wetu mpedwa tusaidie sisi wa vijijini tunaibiwa mweshimiwa rais wetu samia tunakuamini sana sisi wakulima niwanyonge sana nadio tunazulumiwa tunakuombea alla akuongoze kwahili inshaalh
Ndugu Yunus,
Maoni yamepokelewa. Hata hivyo unashauriwa kuwasilisha suala hili kwa mtoa huduma wako, endapo hutoridhika na namna lilivyoshughulikiwa, uwasilishe EWURA kwa hatua zaidi.
Karibu
Naomba kuuliza kama kuna mfumo kazi ambao unatumika kuwajua wamiliki wa vituo vya mafuta vinavyoficha mafuta na kupelekea kukosekana kwa huduma ya mafuta?
Bwana Frank
EWURA inao mfumo wa ndani wa kutambua masuala hayo lakini pia tunapokea taarifa kutoka kwa wananchi wenye nia njema. Na inapobainika hatua kali za kisheria huchukuliwa.
Hivyo tunakusihi endapo una taarifa ziwasilishe EWURA na zitashughulikiwa ipasavyo. Jina lako pia litahifadhiwa.
Karibu.