TAARIFA KWA UMMA: EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta kuanzia Julai 01, 2021

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Alhamisi, Tarehe 1 Julai 2021 ili kuendana na na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2021 na mabadiliko mengine ya sheria ambayo yataanza kutumika ifikapo tarehe 1 Julai 2021. Mabadiliko yanayohusu bidhaa za petroli kama yalivobainishwa katika Sheria ya Fedha ya Mwaka 2021 na mabadiliko mengine ya sheria ni: (i) ongezeko la tozo ya mafuta kwa shilingi 100 kwa kila lita moja ya mafuta ya petroli na dizeli na (ii) kuongezeka kwa ada ya petroli kwa shilingi 100 kwa kila lita moja ya mafuta ya taa.

Soma Zaidi:-https://www.ewura.go.tz/fuel-prices/

Hits: 2795

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *