TAARIFA KWA UMMA: Maombi ya Kubadilisha Umiliki wa Leseni na Jina la kituo cha Mafuta cha Lead Oil (T) Ltd Arusha kwenda Petroafrica Tanzania Limited

TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi la kubadili umiliki wa leseni na jina la kituo .

Soma Zaidi:-Ombi la Kubadili Umiliki wa Leseni na Jina la Kituo cha Mafuta

Hits: 264

2 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA: Maombi ya Kubadilisha Umiliki wa Leseni na Jina la kituo cha Mafuta cha Lead Oil (T) Ltd Arusha kwenda Petroafrica Tanzania Limited

  1. Ndugu Amiri,
   Masuala muhimu

   Ni vyema gari likifika kituoni, likae kwa muda angalau dakika 30. Kupima ujazo wa mafuta ndani ya gari.

   Kwenye upokeaji na ushushaji wa mafuta suala zima la usalama wa watu, mali pamoja na utunzaji wa mazingira (HSE) huzingatiwa kama ifuatavyo.

   Usalama:
   1. Kuhakikisha kuwa kunakuwepo vifaa vya zima moto katika eneo la kushushia mafuta kabla ya kuanza kazi ya ushushaji;
   2. Kusiwepo shughuli zozote zinazohusiana na moto au kuongeza joto (hot work) kama uvutaji wa sigari, uchomeleaji vyuma (welding), silaha za moto (bunduki, bastola) n.k;
   3. Gari lazima liunganishwe na waya wa kuondoa/kuzuia chaji (bonding cable to hazardous voltages/static charges from appearing on equipment). Kwa hiyo, sehemu ya kushushia mafuta lazima pawepo kebo husika au bomba maalum za kushushia ambazo zina kebo hiyo (bonding cable) moja kwa moja.

   Utunzanji wa Mazingira:
   1. Kuhakikisha kuwa hakuna umwagikaji wa mafuta. Kiunganishi cha bomba la kushushia na bomba la tenki (kisima) lazima kiwekwe kifaa maalum cha kukazia (Coupling); na
   2. Pawepo na mtaro uliojengwa kuunganisha sehemu ya kushushia na kichuja mafuta na maji (Oil – Water Separator) ili endapo umwagikaji wa mafuta utatokea kusiwepo uharibifu kwenye mazingira na badala yake mafuta yanaelekezwe sehemu mahsusi.

   Karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *