Taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli. Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni tajwa kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili kupitia anwani tajwa.
Soma zaidi :- MWITO WA KUTOA MAONI
Views: 647
Naomba kujua jinsi gani naweza kupata leseni ya ufundi umeme ninacheti cha umeme daraja la pili lakni pia ni muhitimu wa umeme daraja la tatu
Ndugu Fredrick,
Maombi ya leseni hufanyika kwa njia ya mtandao. Bofya kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ kujisajili kisha endelea kufanya maombi.
Unapaswa kuwa na viambatisho (soft copy) vya cheti cha elimu ya ufundi, wasifu unaonesha kazi ambazo umewahi kufanya, picha (pasport size) yenye kivuli cha bluu, na kitambulisho cha taifa, kura, taifa au leseni ya udereva.
Karibu.