TAARIFA KWA UMMA: Mwito wa Maoni kuhusu Maombi ya Leseni ya Uendeshaji wa Kituo cha Gesi Asilia Iliyogandamizwa kutoka Kampuni ya Tembo Energies Limited

TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba, EWURA, imepokea ombi kutoka kwa kampuni ya Tembo Energies Limited, kwa ajili ya leseni ya uendeshaji wa kituo cha gesi asilia iliyogandamizwa kilichojengwa ndani ya eneo la kituo cha mafuta cha Mount Meru, kilichopo kandokando ya barabara ya Nelson Mandela, eneo la Tabata Mwananchi, mkabala na Nida Textile Mills, Kata ya Makuburi, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam.

Hivyo basi, Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi dhidi ya ombi tajwa hapo juu, afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani iliyotajwa hapa chini ndani ya siku kumi na nne (14) toka tarehe ya tangazo hili.

Soma Zaidi:-Mwito wa Maoni-Maombi ya Leseni kutoka Tembo Energies Limited

Views: 29

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *