TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba, EWURA imepokea ombi la kibali cha ujenzi wa kituo cha kujaza gesi asilia iliyogandamizwa kwenye magari kutoka Energo Tanzania Limited kitakacho jengwa kandokando ya barabara ya Coca Cola, eneo la viwanda Mikocheni, Mtaa wa Mikocheni B, Kata ya Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Hivyo, Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi dhidi ya ombi tajwa hapo juu, afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani iliyotajwa hapa chini ndani ya siku kumi na nne toka tarehe ya tangazo hili.
Soma Zaidi:- Mwito wa Maoni -Ombi la Kibali cha Ujenzi cha CNG kutoka Energo Tanzania Limited
Views: 109