Beina Tozo za Gesi Asilia

Gesi Asilia | Udhibiti wa Kiufundi | Utoaji wa Leseni za Gesi Asilia | Nyenzo za Udhibiti | Udhibiti Uchumi | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Udhibiti Uchumi

Uhitaji wa kudhibiti uchumi katika gesi asilia unachagizwa na ukweli kwamba watoa huduma wanaohodhi shughuli za gesi asilia, na kama wataachwa bila kudhibitiwa wanaweza kutumia vibaya uwezo wao, na kusababisha utoaji wa huduma kuzorota.EWURA inadhibiti kiuchumi sekta hii kwa kuweka utaratibu wa kupanga bei na kuhuisha viwango vya bei na tozo baada ya kupokea maombi au pale EWURA inapoona umuhimu wa kufanya hivyo. Ili kumwezesha mwombaji kuwasilisha maombi ya bei kwa ajili ya kupitiwa na kuidhinishwa, EWURA inatumia  Mwongozo wa Maombi ya Bei na Tozo wa Mwaka 2009.

Bei na Tozo

EWURA imepewa mamlaka ya kufanya mapitio ya viwango, bei, na tozo ama wakati maombi yamewasilishwa na mwombaji au wakati mamlaka inaona ni muhimu kufanya hivyo kama ilivyoainishwa katika ibara ya 17 Sheria ya EWURA ,Sura ya 414. Utaratibu wa maombi ya viwango vya bei  umeanishwa katika Mwongozo wa bei za Umeme na Gesi Asilia,2017Mwongozo wa Maombi ya bei na Viwango vya Gharama za huduma wa mwaka 2017.Aidha,Kanuni za Kanuni za Upangaji bei za gesi asilia za mwaka 2020 ndizo zinayotumika kupanga bei ya gesi asilia.

EWURA iliwahi kupanga bei ya gesi asilia kwa Uwekezaji Maalum wa Kimkakati tarehe 29 Desemba 2016. Agizo la bei iliyoidhinishwa hii hapa.

Visits: 107