Miundombinu ya Sekta ndogo ya Gesi Asilia

Gesi Asilia | Udhibiti wa Kiufundi | Utoaji wa Leseni za Gesi Asilia | Nyenzo za Udhibiti | Udhibiti Uchumi | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Udhibiti wa Kiufundi

EWURA hufanya udhibiti wa kiufundi kwenye miundombinu na huduma zinazodhibitiwa pamoja na Afya, Usalama na Mazingira. Kabla ya kuanzishwa EWURA, viwango vya ubora wa miundombinu na huduma ikiwemo, ainisho dhahiri la mabomba ya gesi, viwango vya kiuhandisi katika ujenzi na usakinishaji vilitokana na makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na anayepewa leseni.

Mara kadhaa, viwango vilivyotumika vilizingatia mlolongo wa viwango vya the American Petroleum Institute (API) Standards, International Organization for Standardization (ISO), American Society for Testing and Materials (ASTM) International Standards, and American Society of Mechanical Engineers (ASME) Standards, including the Canadian Standards Association (CSA) Standards, such as CSA Z662-07

 

Udhibiti wa Usalama

Masuala ya Afya na Usalama mahali pa kazi yanadhibitiwa na Sheria ya OSHA, 2003 chini ya Wakala ya Usalama na Afya mahali pa kazi. Kwa kawaida EWURA hufuatilia kwa karibu masuala ya afya na usalama kwa kuzingatia mfano wa kuigwa katika tasnia. Udhibiti wa kiufundi huzingatia usalama.

Sheria zinazosimamia masuala ya afya na usalama mahali pa kazi Tanzania wakati wa ujenzi na uendeshaji ni:

  1. The Occupational Health and Safety Act, 2003,
  2. The Contractors Registration Act, 1997,
  3. The Workers’ Compensation Regulations, 2016; na,
  4. Fire and Rescue Force Regulations, 2007.

EWURA inalinda na kuhifadhi mazingira kwa kuhakikisha kuwa waombaji leseni wanafanya utafiti unaohitajika ili kutoa uamuzi sahihi kuhusu mradi. Mamlaka pia inashiriki katika kupitia Tathmini za Athari kwa Mazingira.

Visits: 73