Rejesta ya Umma

Complaints and Disputes ResolutionsTariff OrdersCompliance OrdersCode of ConductDeclarations

Rejesta ya Umma

Rejesta ya Umma ya Kielektroni ya EWURA ni njia ya kupata taarifa za udhibiti wa sekta nne ambazo ni umeme, petroli, gesi asilia na maji na usafi wa mazingira.

Kuwepo kwake kumetokana na kutambua umuhimu na uhitaji wa umma kuwa na uelewa kuhusu upatikanaji wa taarifa sahihi za uamuzi uliotolewa, utaratibu, malelekezo na kanuni za ndani, pamoja na Kanuni ya Maadili inayoongoza mienendo ya Wajumbe wa Bodi na Wafanyakazi wa EWURA.

Katika kutekeleza moja ya misingi yake ya uwazi na matakwa ya Kifungu cha 24 cha Sheria ya EWURA Sura 414, Mamlaka inahakikisha kwamba, jamii ya Tanzania na ya Kimataifa inatapata taarifa kamili na sahihi kuhusu shughuli za udhibiti kupitia Rejesta ya Umma halisi na ya kielektroni.

 

EWURA kupitia moja ya nguzo zake muhimu ya uwazi na kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 24 cha Sheria ya EWURA Sura 414, inahakikisha kwamba jamii ya Tanzania na ya Kimataifa inatapata taarifa kamili na sahihi kuhusu shughuli za udhibiti kupitia Rejesta ya Umma halisi na ya kielektroni.

Visits: 134