Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira
EWURA hutayarisha ripoti za utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Mikoa, Wilaya, Miji midogo na Miradi ya Kitaifa ambazo hutoa ulinganifu wa utendaji wao.
Ripoti za utendaji hutayarishwa katika seti mbili, ambapo moja ni ya Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za mikoa na miradi ya kitaifa, na nyingine ni ya wilaya na miji midogo. Ripoti hizi zinalinganisha utendaji wa Mamlaka na kushindanishwa kwa kufuata vigezo mbalimbali vya huduma zao.