Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inawatangazia watu wote wanaofanya shughuli za kufunga umeme kuwa, kutakuwa na semina ya siku moja kuhusu kanuni mpya za Huduma ya Ufungaji wa Mifumo ya Umeme za mwaka 2015. Semina hii itafanyika katika ukumbi wa ofisi za EWURA, Gorofa ya 7, Jengo la LAPF ambalo lipo mkabala na kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama kuanzia saa 4:00 asubuhi , siku ya Alhamisi tarehe 16 June, 2016. Wamiliki wote wa leseni za kufunga umeme na wawakilishi wa makandarasi wa umeme, wanakaribishwa kushiriki katika semina hii. Aidha, washiriki wa semina wanaombwa kuthibitisha ushiriki wao kwa barua pepe ifuatayo: evarist@ewura.go.tz au simu namba 0687221314 kabla ya tarehe 13/6/2016.
——————————————————————————–
Views: 182