Kifungu cha 5(a) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131 ya Sheria za Tanzania, kinaipa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) jukumu la kutoa leseni kwa watoa huduma mbalimbali katika Sekta Ndogo ya Umeme. Ufungaji wa mifumo ya umeme ni shughuli mojawapo inayohitaji mtu anayefanya kazi hiyo kuwa na leseni, hivyo EWURA inatoa leseni kwa watu waliofuzu kufanya kazi mbalimbali za ufungaji wa mifumo ya umeme.
Kwa mujibu wa kifungu cha 8(1)(h) cha Sheria ya Umeme, EWURA imetoa Kanuni mpya za Huduma ya Ufungaji wa Mifumo ya Umeme za mwaka 2015, ambazo zilichapishwa kwenye gazeti la Serikali tarehe 11/9/2015 Tangazo Namba 404 la mwaka 2015. Kanuni hizo zinapatikana kwenye tovuti ya EWURA.
Attachment: TANGAZO KWA UMMA-sheria mpya-ARUSHA
_____________________________________________________________________
Hits: 202