Mahojiano na Vyombo vya Habari Kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Kutoka Hoima(UGANDA) hadi Tanga(TANZANIA)

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ni Mradi wa Sekta binafsi na unatekelezwa katika nchi mbili (Uganda na Tanzania). Mradi huo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani 3.55 bilioni na kuleta ajira za kati ya watu 6,000 na 10,000 ndani ya miaka mitatu (3). Mafuta Ghafi ya Hoima (ya aina yake), yatasafirishwa kutoka Uganda kwenda sokoni nchi za nje, kupitia Tanzania.  Mradi wa Bomba umbali wake ni kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.

Soma Zaidi Maelezo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Kutoka Uganda  hadi  Tanga Tanzania (002)

______________________________________________________________________________________

Visits: 403

6 thoughts on “Mahojiano na Vyombo vya Habari Kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Kutoka Hoima(UGANDA) hadi Tanga(TANZANIA)

  1. Habari

    Naomba kuelewa utaratibu wa kujisajili ili kuja kutoa huduma wakati wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda kwenda Tanga hapa kwetu Tanzania.

    Mipawa.
    +255716774233
    +255762280088

    1. Ndugu Mipawa
      Kujisajili ni kujaza fomu Na. N-100 inayopatikana katika tovuti yetu kupitia kiunganishi https://www.ewura.go.tz/local-content-lssp-database/; vilevile upo mwongozo wa mahitaji husika kupitia kiunganishi https://www.ewura.go.tz/wp-content/uploads/2021/07/Mwongozo-wa-Jinsi-ya-Kujisajili-Kwenye-Kanzi-Data-ya-Watoa-Huduma-wa-Ndani.pdf
      Baada ya kujaza fomu, itume kwenye barua pepe info@ewura.go.tz
      Endapo utapata changamoto yoyote unaweza kupiga bila malipo 0800110030 siku na muda wa kazi AU; kutembelea ofisi yetu iliyo karinu nawe katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha.
      Karibu

    1. Ndugu Edward,
      Pole kwa changamoto. Usajili hufanyika kwa njia ya mtandao kwa kujaza fomu N-100 iliyopo katika tovuti yetu na kuituma kwa barua pepe ya info@ewura.go.tz.
      Kwa msaada zaidi tupigie 0800110030 (bila gharama kwa siku na muda wa kazi)
      Asante

  2. Na kwasisi vibarua wenye shida na hizo kazi ndugu zangu tunasajili wapi maana mimi nipo Dar lakini huwa napata mitingo ya serikali lakini kwa huu sijapata muenendo wake

    1. Ndugu Edward,
      Usajili ni kwa makampuni. Vibarua mnaweza kupata kazi kupitia kampuni zilizosajiliwa na EWURA. Tizama orodha ya kampuni hizo katika tovuti yetu ili uombe kazi katika mojawapo inayokufaa.
      Asante

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *