Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji Kutoka Mamlaka ya Majisafu na Usafi wa Mazingira ya Muheza WSSA Kwa Mwaka 2019/20 – 2021/22

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA Act) Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Ijumaa, tarehe 3 Mei 2019 katika ukumbi wa Tareku uliopo Muheza Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Lengo la mkutano huo ni kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali; Baraza la Ushauri la watumia  Huduma  zinazodhibitiwa na EWURA; wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Muheza na wananchi wote kwa ujumla kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa. Soma Zaidi:-

Mwito wa Maoni ya Wadau- Muheza WSSA

A Call for Stakehoders’ Views -Muheza WSSA

_______________________________________________________________________________________________________________

Hits: 25

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *