EWURA Yaendelea Kuboresha Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji

EWURA  Yaendelea kuboresha Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji

Visits: 1246

23 thoughts on “EWURA Yaendelea Kuboresha Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji

  1. Ndugu Mbatina,
   Wasiliana na mtoa huduma yako ambaye ni Mamlaka ya Maji Mwanza, atakupatia bei ya huduma na mchanganuo wa gharama yoyote unayohitaji ufafanuzi.
   Kwa masuala zaidi piga simu 0800110030 (bure)

   1. Nipo Kigoma mjini hawa Kuwasa wamenifungia maji kwa kuchelewa Sana nishapeleka malalamiko Ewura ni kimya tu Wala siambiwi mwenendo wa malalamiko yangu

 1. Swala la kudhibiti mafundi wanaofunga mifumo ya umeme bila leseni bado linachangamoto kubwa sana. kwasababu asilimia kubwa ya mafundi wasio na leseni hawana hamasa ya kuomba leseni kwakua wanaaminika na wateja na wanapata kazi kurahisi sana kutokana na uzoefu wao na umaharufu walionao.Mteja hana muda wa kumuuliza fundi kama analeseni anachojali yeye ni kazi yake ifanyike tu..Nyie mkiwa kama mamlaka ya nishati kwanini msiweke mfumo utakao mbana mteja na fundi? mpaka mje mkamate fundi asiye na leseni je,mmeweka au kusambaza mawakala wenu ili kudhibiti hilo?..kwakua mtaishia kusema tu mtakamata fundi na kumpeleka jela lakini mifano hatuioni na mafundi wasio na leseni wanazidi tu kufanya kazi kila siku,au mnasahau kua fundi mwenye leseni huwa analipia leseni yake kila baada ya muda ili leseni yake iendelee kua hai??…hii inavunja moyo kwa mafundi walio na leseni kwakua hawapati kazi za kufunga mifumo ya umeme kwenye nyumba za wateja na wasio na leseni hawana hamasa ya kuomba leseni kwakua wanapata kazi mitaaani na hakuna sheria inayowabana., hadi akamatwe si rahisi
  .
  CHAKUFANYA; Wekeni mfumo utakao wabana wateja na mafundi…..kaeni vikao na Tanesco na mkubaliane tanesco zote Tanzania..kua mteja mpya anaeenda tanesco yoyote kuchukua kadi aende na fundi aliyemfungia mfumo mpya wa umeme alafu fundi aonyeshe leseni yake ambayo ipo hai iwe kama ndiyo kibari cha kupewa kadi au fundi atoe copy ya leseni yake alafu ampatie mteja aendenayo tanesco kuchukua kadi..Hii itasaidia kwa kiasi kibwa sana kudhibiti mafundi wasio na leseni na itajenga hamasa ya mafundi wasio na leseni watafute lesenika.INAUMIZA SANA KUMILIKI LESENI AMBAYO UNAILIPIA KILA MUDA ALAFU AIFANYI KAZI INAKUA KAMA PAMBO ALAFU MAFUNDI WASIO NA LESENI WANAENDELEA KUPETA MTAANI…EBU LIFANYIENI KAZI HILO SWALA LINATUUMIZA SANA MAFUNDI WENYE LESNI

   1. Hilo ni lamsingi kabisa…wala hakuna majadiliano katika hilo…Mimi naona hakuna haja ya kusuburi kufanya hilo…
    Uwezo wa kufanya hivyo upo…kwanini lisifanyike??
    Kuna watu Wana Leseni na wanalipa kodi wakati mwingine wanakosa kazi kwasababu ya mafundi wa vichochoroni….na Mamlaka ipo tu.

 2. vipi kuhusu movable fuel filing stations mesharuhu hapa nchini zitumike hususani maeneo ya vijijini , utaratibu wake ukoje?

  1. Ndugu Samwel,
   Utaratibu wa kupata leseni ni kufanya maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ ambacho hupatikana kwa kubofya neno LOIS katika tovuti yetu.
   Viambatisho muhimu ni nakala ya cheti cha elimu ya ufundi, kitambulisho (leseni ya udereva, kadi ya mpiga kura au kitambulisho cha taifa), picha ndogo (paspoti) yenye kivuli cha bluu na wasifu (CV).
   Endapo ukipata changamoto yoyote wasiliana nasi kwa 0800110030-siku na muda wa kazi.

   Karibu

 3. habari naitwa Fadhili nipo Tanga muheza mimi fundi umeme lakini sina vyeti vya ujuzi wa kusomea ktk vyuo ,lakini nina vyeti nilivyopata vya uzoefu katika shirika la umeme tanesco zaidi ya miaka saba na mpaka xx naendelea kufanya kazi za umeme majumban chini ya wakandarasi wa umeme waliosajiliwa na ewura,Hvyo basi nahitaji kupata leseni kutoka ewura ili niweze kulipa kodi,.Nahitaji msaada

  1. Ndugu Fadhili
   Tafadhali unaweza kupata leseni ila unapaswa kwanza kwenda VETA ili wakufanyie majaribio ya ujuzi wako kisha watakupatia barua ya utambuzi kulingana na ngazi utakayofaulu usaili, kisha utawasilisha matokeo hayo wakati wa kuomba leseni. Vilevile, upo utaratibu wa kurasimisha ujuzi ambao husimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na hutoa matangazo yake kwa mwaka mara mbili. Unaweza kufuatilia hilo pia ili uweze kurasimisha ujuzi wako na upate leseni stahiki.
   Karibu.

 4. EWURA MNATOA HUDUMA NZURI NA KWA WAKATI. HATA HIVYO, NASHAURI MTUMIE MFUMO WA ONLINE KWENYE UTOAJI WA LESSENI KAMA WANAVYOFANYA BRELA ILI KUWE NA KUMBUKUMBU ZA KUDUMU WAKATI WOTE WA UENDESHAJI WA MRADI.

  1. Ndugu Cosmas
   Tunashukuru kwa ushauri, tutaangalia namna ya kuboresha mfumo wetu wa kieletroni ambao tunautumia kutoa huduma za maombi ya leseni, vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta na gesi asilia, kupokea malalamiko sanjari na kusajili watoa huduma na wataalamu kwenye kanzidata ya LSSP NA TPD.

   Karibu

 5. KWENYE UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI UPANDE WA VITUO VYA MAFUTA, NASHAURI ITUMIKE BARUA YA USAJILI WA MRADI NEMC NA BAADA YA UJENZI KUKAMILIKA KITUMIKE KIBALI CHA MAZINGIRA KWENYE KUOMBA LESENI YA KUENDESHA BIASHARA YA MAFUTA.

  1. Ndugu Cosmas,
   Tufadahli, endapo utaratibu unaopendekeza utafuatwa, EWURA itakuwa na jukumu gani kwenye ujenzi wa vituo vya mafuta na sasa vya gesi asilia pia?
   Ama lengo hasa ni ninI? Pia tungependa kufahamu changamoto katika utaratibu unaotumika kwa sasa.
   Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *