Kwa mujibu wa Kifungu cha 19 (2) (b) cha Sheria ya EWURA, Sura ya 414, kutakuwa na mkutano Jumatatu, tarehe 14 Juni 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Kijiji cha Igoda Mufindi kuanzia saa 4:00 asubuhi. Lengo kuu la mkutano huo ni kukusanya maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali (GCC), Baraza la Ushauri la Watumiaji (CCC), wateja na umma kwa jumla juu ya uhalisia wa maombi ya mabadiliko ya bei zinazopendekezwa.
Soma Zaidi:-
- Mwito wa Maoni ya Wadau-Mwenga
- A Call for Stakeholder’s Views-Mwenga- ENGLISH 2021
- Mwenga_Tariff Application
Views: 359
Nataka kuwa wire man
Ndugu Hamis,
Karibu. Maombi ya leseni za umeme hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa LOIS unaopatikana katika tovuti ya EWURA.
Tumia kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/ kujisajili kisha endelea kujaza fomu ya maombi.Unatakiwa kuwa na picha yenye kivuli cha bluu, cheti cha ufundi, kitambulisho na wasifu wako (CV) inayoonesha kazi ulizofanya; vyote vikiwa katika nakala laini (soft copy).
Endapo utapata changamoto yoyote wasiliana nasi BURE 0800110030 siku na muda wa kazi.
Karibu