Kwa mujibu wa Kifungu cha 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA, Sura ya 414, kutakuwa na mkutano wa wadau utakaofanyika siku ya Jumatano, tarehe 16 Juni 2021 ) kuanzia saa 4:00 Asubuhi, katika ofisi za EWURA zilizopo kanda ya Mashariki, Ghorofa ya 7, Jengo la PSSSF, Mkabala na kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo ni kukusanya maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali (GCC), Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), wateja pamoja na wananchi kwa ujumla
Soma Zaidi:-
- Mwito wa Maoni ya Wadau-Songas
- A Call for Stakeholder’s Views-Songas
- Tariff Application Document
- Songas Customer Service Charter
- Audited FS for the year ended December 2020
Hits: 832
Habari?
Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika sekta za mafuta maji na umeme nchini.
Ninahitaji kuanzisha Kituo kidogo kijijini cha kuuza mafuta hapa Hedaru na Makanya Wilaya ya Same Mkoa wa KILIMANJARO; Ninaomba kupata maelekezo na utaratibu wa kufuata ili kufanikisha wazo langu biashara.
Nitafurahi kujibiwa mapema ili nisipoteze fursa hiyo.
Asante
Mcharo, Abraham Daudi.
0788026573
Ndugu Abraham,
Tafadhali, umetumiwa kipeperushi katika barua pepe yako kuhusu suala ulilowasilisha kwetu na kanuni husika katika eneo hilo.
Maombi ya leseni na kibali cha ujenzi huombwa kupitia mfumo wa LOIS ambao unapatikana katika tovuti ya Mamlaka kwa kiunganishi https://lois.ewura.go.tz/ewura/
Hata hivyo, suala lako limewasilishwa katika Ofisi yetu ya Kanda ya Kaskazini iliyopo Arusha, jengo la PSSSF ghorofa ya pili, mkabala na Kibo Complex.
Karibu
Natumain msalama naomba kutoa keto ya huku mtaani ges tuna uziwa gali Sana mtungi wa 14.5Tsh23000
Ndugu Avity,
Imepokelewa.
Karibu