Mwito wa Kutoa Maoni:Maombi ya Leseni kutoka kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shinyanga WSSA)

TAARIFA inatolewa kwa umma kuwa, EWURA  imepokea maombi ya leseni kutoka kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga  kwa ajili ya kutoa huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika Miji ya Tinde, Iselamagazi, Didia na Manispaa ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga.

Soma Zaidi:-

Visits: 245

4 thoughts on “Mwito wa Kutoa Maoni:Maombi ya Leseni kutoka kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shinyanga WSSA)

    1. Ndugu Goodluck
     Tafadhali rejea madaraja ya leseni hapa chini ili kuona endapo sifa ulizonazo zinakidhi kupata leseni

     Madaraja ya leseni, na mipaka ya shughuli zao.
     Aina ya Leseni Kazi Zinazohusika Elimu ya Ufundi wa Umeme na Uzoefu Husika Unahitajika
     Daraja A Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa umeme wa aina zote. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Cheti cha Usajili cha Utaalamu wa Uhandisi wa Umeme na vyeti husika vya elimu;
     (ii) Shahada ya uhandisi wa umeme au uhandisi wa umeme-mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au zaidi na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme,mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwenye msongo wa juu;
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme au Umeme-mitambo na
     miaka mine ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, miwili kati ya hiyo,iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa juu;
     (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/umeme-mitambo na miaka mitano ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, miaka mitatu kati ya hiyo iwe ya ufungaji mifumo ya umeme wa msongo wa juu.
     Daraja B Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa kati mpaka kiasi cha msongo wa volti 33,000. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme au
     uhandisi wa Umeme-Mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8, au zaidi na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufungaji mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo uwe wa ufungaji wa umeme katika msongo wa kati;
     (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme wa msongo wa kati; na
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au
     Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya uhandisi wa umeme/ umeme- mitambo na miaka minne ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga wa mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji wa umeme wa msongo wa kati.
     Daraja C Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo usiyozidi volti 1000. isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Shahada ya Uhandisi wa umeme/umeme-mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 8 au inayolingana na Shahada ya Uhandisi wa umeme;
     (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo au inayolingana na hiyo;
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Stashahada ya kawaida ya Uhandisi wa Umeme/U meme-Mitambo au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya Uhandisi Umeme au inayolingana na hiyo katika ufungaji mifumo ya umeme,
     (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 4, Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 5, au cheti cha kufuzu Mtihani wa ujuzi wa umeme daraja la I / Ngazi ya III au inayolingana na hiyo na miaka miwili ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme; au
     (v) Cheti cha kufuzu cha Mtihani wa ujuzi wa umeme Daraja la II/ ngazi ya II au kinacholingana na hicho na miaka mitatu ya uzoefu katika masuala ya kazi za kufunga mifumo ya umeme.
     Daraja D Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo usiyozidi volti 230. Isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi yoyote iliyo chini ya leseni maalumu (S1, S2 na S3) pasipokuwa na leseni husika (i) Cheti cha kufuzu mtihanii wa ujuzi wa Umeme daraja la I, II, III, au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 4, Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi ngazi ya 5 au ainayolingana na hiyo katika ufundi wa ufungaji wa mifumo ya umeme; au

     (ii)mafunzo ya awali,kozi fupi, kozi za kati, cheti cha Juu cha Ufundi au cheti kinacholingana na hicho na uzoefu wa miaka mitatu katika kufunga mifumo ya umeme

     Daraja W Inatolewa ili kuweza kufanya kazi za ufungaji mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa mwenye leseni Daraja A, B, S1, S2, S3, C au D. Mwombaji wa leseni anapaswa kuwa na mafunzo ya awali/kozi fupi/kozi ya kati, au cheti cha Juu cha ufungaji wa mifumo ya umeme au sifa nyinginezo kutoka Taasisi nyingine za Kiufundi zinazotambulika kutoa mafunzo ya ufungaji mifumo ya Umeme.
     Daraja S1 Inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme katika msongo wa aina zote. (i) Cheti cha Usajili cha Utaalam wa Uhandisi wa Umeme au /Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa juu.
     (ii) Shahada ya Uhandisi wa Umeme au Uhandisi wa Umeme-Mitambo au
     Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 8 na miaka minne ya uzoefu wa kazi za ufungaji mifumo ya umeme ,miaka miwili kati ya hiyo iwe ni ufungaji wa mifumo ya umeme katika msongo wa juu wa umeme;
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitano ya uzoefu wa kazi katika masuala ya kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka mitatu kati ya hiyo iwe ya ufungaji mifumo ya msongo wa juu;
     (iv) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 6 au Cheti cha Ufundi sanifu katika masuala ya Uhandisi wa Umeme/Umeme-Mitambo na miaka sita ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka minne kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme wa msongo wa juu
     Daraja S2 Inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 33,000 (i) Cheti cha Usajili cha Utaalamu Uhandisi wa Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja kati ya hiyo iwe ni kufunga mifumo ya umeme katika msongo wa kati; au
     (ii) Shahada ya Uhandisi wa umeme au Uhandisi wa Umeme- Mitambo au
     Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 8 na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, miaka miwili kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa kati; au
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Ufundi Ngazi ya 7 au zaidi, au Stashahada ya Juu ya Uhandisi Umeme/ Umeme-Mitambo na miaka minne ya uzoefu wa kazi katika masuala ya kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme, mwaka mmoja na nusu kati ya hiyo iwe ya ufungaji umeme katika msongo wa kati;Daraja S3 Inatolewa ili kufanya kazi maalum za ufungaji mifumo ya umeme mpaka msongo wa volti 1,000 (i) Shahada ya Uhandisi wa Umeme/Umeme-Mitambo au Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 8 na zaidi au inayolingana na Shahada ya Uhandisi Umeme/Umeme-Mitambo na mwaka mmoja wa uzoefu wa kazi maalumu za kufunga mifumo ya umeme;
     (ii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 7 au Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme /Umeme-Mitambo au inayolingana na hiyo, na miaka miwili ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme;
     (iii) Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 6 au Stashahada ya Kawaida ya Uhandisi Umeme/ Umeme-Mitambo au Cheti cha Ufundi kamili katika masuala ya uhandisi wa umeme au inayolingana na hiyo na miaka mitatu ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme.
     (iv)Tuzo ya Kitaifa ya Kiufundi Ngazi ya 4 au Cheti cha kufuzu Mtihani wa Ujuzi wa Umeme Daraja la I, II au inayolingana na hiyo na miaka minne ya uzoefu wa kazi maalum za kufunga mifumo ya umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *