TAARIFA KWA UMMA : Ombi la kubadili umiliki wa leseni

TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi la kubadili umiliki wa leseni na jina la kituo cha Oliver Rishaely Kaaya Dabalo. Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi dhidi ya mabadiliko ya umiliki na majina ya leseni tajwa hapo juu, afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani tajwa i ndani ya siku kumi na nne toka tarehe ya tangazo hili.

Soma zaidi;- Ombi la kubadili umiliki wa leseni ya kituo

Visits: 406

2 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA : Ombi la kubadili umiliki wa leseni

 1. Swali kwa wakaguz wa vtuo vya mafuta(filling stations inspectors) hiv huwa wanaconduct huo ukaguz kila baada ya muda gan?, na no maeneo gani hasa huwa wnaangalia katka kituo na kma watabain mapunguf yyte huchua hatua gani kabla ya kufikia maamuz ya kufunga kituo au ONYO la kuashiria watafunga kituo hicho msaada ktk hili tafadhali

  1. Ndugu Abuu,
   Ukaguzi hufanywa kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya mafuta. Aidha, upo ukaguzi wa aina mbili. Ukaguzi wa kabla ya kujenga kituo ili kuthibitisha endapo vigezo na masharti ya ujenzi yamezingatiwa na ukaguzi wa pili ni baada ya mwenye kituo kupatiwa leseni ya kuendesha biashara ya mafuta. Leseni hizo huambatana na masharti muhimu ya kuzingatiwa na kila mwenye leseni husika. Kwa maana hii, ukaguzi hufanyika ili kubaini na kujiridhisha endapo masharti hayo yamezingatiwa lengo likiwa ni kumlinda mteja/ mtumiaji wa mafuta, kuhakikisha biashara inafanyika kwa kuzingatia kanuni za afya na mazingira pamoja na usalama.
   Wakaguzi hufanya ukaguzi wa aina ya pili kwa mujibu wa ratiba zinazopangwa kwenye ofisi za Kanda na Makao Makuu. Kwa ukaguzi wa aina ya kwanza, ufanyika pale kunapokuwa na hitaji husika. Aidha, unaweza kupitia kiunganishi hiki https://www.ewura.go.tz/regulatory-tools/ kusoma miongozo mbalimbali ya kisheria kwenye biashara ya mafuta.
   Karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *