Mwito wa Kutoa Maoni : Maombi ya Leseni Kujhusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, wafuatao wameomba leseni kujihusisha na mkondo wa chini wa sekta ya mafuta ya petroli, Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni tajwa kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili kupitia anwani tajwa.

Soma zaidi:- Mwito wa Kutoa Maoni

Visits: 486

5 thoughts on “Mwito wa Kutoa Maoni : Maombi ya Leseni Kujhusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta ya Mafuta ya Petroli

  1. Ndugu Samwel,
   Utaratibu unaofuata ni EWURA kushughulikia maombi yako na leseni itakapokmilika utapewa taarifa kupitia mawasiliano yako uliyosajili katika mfumo.
   Aidha, unashauriwa kuingia mara kwa mara katika mfumo kufuatilia hali ya maombi yako.
   Karibu

    1. Ndugu Japhet,
     Leseni hutolewa ndani ya siku 40 tangu maombi kukubaliwa. Sababu ni kutokana na mchakato wa wa awali kabla ya leseni kutolewa ambao huhusisha ukaguzi stahiki sanjari na siku 14 za kupokea maoni ya wananchi kuhusu maombi husika.
     Asante.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *