TANGAZO: Fursa za Mikopo Nafuu ya Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petrolina Dizeli) Vijijini

Wakala unakaribisha waombaji wenye vigezo kuomba mkopo ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini.Mwombaji atatakiwa kujaza fomu maalum ambayo inapatikana pia katika tovuti ya Wakala wa Nishati Vijijini (www.rea.go.tz).

Mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo ni tarehe 25/8/2023 saa tisa na nusu alasiri. 

Soma Zaidi: FURSA YA MIKOPO NAFUU YA UWEKEZAJI KWENYE VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI

Views: 1634

16 thoughts on “TANGAZO: Fursa za Mikopo Nafuu ya Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petrolina Dizeli) Vijijini

  1. Form ya hayo maombi ya ujenzi/uwekezaji wa vituo nafuu vya mafuta kwa vijijini haipatikani/haionekani kwenye tovuti ya rea kama maelezo yalivyo ainisha.

        1. Ndugu Francis,

          Fomu na Maombi ya Mkopo wa vituo vya mafuta vua vijijini huratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini yaani REA. Hivyo unashauriwa kuwasiliana na REA kwa msaada zaidi.
          Kwa upande wa EWURA, inalo jukumu la kutoa kibali cha ujenzi wa kituo cha mafuta kwa gharama ya sh 50,000/ sanjari na leseni ya uendeshaji biashara ya mafuta kwa gharama ya tsh 100,000/.
          ZINGATIA: Gharama hizi ni kwa vituo vya vijijini pekee.

          Karibu

    1. Ndugu Kaje,

      Wakala ya Nishati Vijijini (REA) ndio wasimamamizi wa mikopo hiyo. Hivyo tunakushauri kufuatilia REA.

      Karibu

    1. Ndugu Maganga,
      Utaratibu unatakiwa kuwa na eneo/ardhi yenye hati au muhtasari wa kijiji wa kuridhia ujenzi wa kituo cha mafuta, uwe na barua ya tathmini ya mazingira iliyosainiwa na mkurugenzi wa wilaya/manispaa, uwe na kitambulisho,Namba ya mlipa kodi, uwe na mchoro wa kituo uliochorwa na mhandisi aliyesajiliwa kisha utaomba kibali cha ujenzi kwa kutumia mfumo wa LOIS unaiopatikana kwenye tovuti http://www.ewura.go.tz.

      Kuhusu mikopo ya ujenzi wa vituo, Wakala wa Nishati Vijijini REA ndiye mratibu wa masuala hayo hivyo unasahuriwa kuwasiliana nae.

      Karibu

    1. Ndugu Casto,

      Suala hili linaratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) hivyo unashauriwa kuwasiliana nao.

      Karibu

  2. Habari naweza pata vipeperushi vinavyohusu ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini vikiwa na maelekezo pamoja na michoro yake

    1. Ndugu Amos;
      Utaratibu wa mikopo unafanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Hivyo unashauriwa kuwasiliana nao.

      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *