MWITO WA KUTOA MAONI : Kuhusu Maombi ya Leseni Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta yaMafuta ya Petroli

Kutokana na kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania, taarifa inatolewa kwa umma kwamba, mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote wa leseni  kwamba asipewe leseni, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

Soma Zaidi:-Mwito wa Kutoa Maoni-Maombi ya Leseni sekta ya Petroli

Visits: 316

6 thoughts on “MWITO WA KUTOA MAONI : Kuhusu Maombi ya Leseni Kujihusisha na Mkondo wa Chini wa Sekta yaMafuta ya Petroli

 1. Naweza kuanzisha kituo Cha kuuza mafuta Kwa matenki maalumu yenye pump bila kuyafukia chini? Yaani mobile fuel station

 2. Habari viongozi wa nishati Tanzania
  Naitwa Mo Bawazir ni mdau wa mafuta,
  Maoni yangu ni ktk mji wa nyakahura mzani, Kuna uhalamia mkubwa sana mafuta ya transt yanauzwa sana na hakuna mamlaka yoyote sio ewra, polis, wala viongozi wa kijiji, tunakaa ktk kituo kwa siku diesel hadi lt.70 hii ni aibu kubwa kwenu kama viongozi na tunapoelekea tunafunga kituo.
  Ili uwe mji wa mafyta haramu.

 3. Habari, naomba kujua sifa kujenga kituo cha mafuta hasa mjini ukizingatia vitu kama
  1. Ukubwa wa eneo
  2. Hati kusoma makazi,
  3. Uwepo wa makazi karibu na kituo ni umbali gani
  4. Na vinginenyo

  1. Ndugu Cris

   Ukubwa wa eneo ni kuanzia 18000 hadi 2500 (isipokuwa kwa kituo ambacho ni cha kujazia mafuta pekee yaani filling station bila huduma nyinginezo kinaweza kuanzia mita za mraba 400). Hati lazima iwe ya kituo cha mafuta; umbali wa kituo cha mafuta na makazi unashauriwa kuwasiliana na wahusika wa mipango)

   Vitu vingine ni lazima kabla ya kujenga kituo upate kibali cha ujenzi kutoka EWURA, uwe na mchoro wa kituo (huu unatakiwa kuchorwa na mhandisi aliyesajiliwa, uwe na jina la kituo lililosajiliwa, Namba ya mlipa kodi (TIN); Cheti cha Tathmini ya Mazingira kutoka NEMC. Endapo ni jina la kampuni, cheti cha usajili wa kampuni. Pia unaweza kupitia kiunganishi hiki https://www.ewura.go.tz/approval-and-licencing/ ili kupata maelezo zaidi ya namna ya kuomba na mwongozo uliandikwa (guidance) kwenye kiunganishi hicho.

   Maombi ya Kibali cha ujenzi na leseni hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa LOIS uliopo katika tovuti ya EWURA. Gharama za maombi ya kibali cha ujenzi wa kituo cha mjini ni sh. 500,000/

   Karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *