MPANGO MKAKATI

MPANGO MKAKATI

Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2021-22 – 2025-26) umeandaliwa kupitia mchakato shirikishi na majadiliano. Kupitia mfululizo wa warsha shirikishi, kazi za EWURA na uendeshaji, zilibainishwa na kuibua masuala muhimu yanayoathiri utoaji wa huduma za Mamlaka, uwezo na udhaifu wake. Mchakato huu ulilenga kuleta uelewa wa pamoja wa Mpango Mkakati na matokeo ya baadaye.

Warsha za Mpango Mkakati zilihusisha kufanya uchambuzi wa masuala yafuatayo

  • Usuli wa EWURA
  • Kazi na Majukumu ya EWURA
  • tathimini ya utendaji wa Mpango Mkakati uliopita, kufanya uchambuzi wa jitihada za hivi karibuni, mafanikio na changamoto;
  • uchambuzi wa wadau;
  • mwonekano wa taasisi; na,
  • uchambuzi wa mwenendo wa taasisi

Uchambuzi wa EWURA uliibua masuala  muhimu yafuatayo

  • Katika kipindi cha mipango, Mamlaka itakabiliana mara kwa mara na changamoto mpya zitakazojitokeza pamoja na miongozo ya serikali.
  • Masuala mtambuko ambayo ni kuzingatia jinsia; utawala bora; VVU/UKIMWI; magonjwa yasiyo ambukiza; uimara na afya za wafanyakazi; matumizi ya madawa ya kulevya na vileo na utunzaji wa mazingira; yataendelea kushughulikiwa na kuimarishwa katika Mpango Mkakati huu.
  • Ili kukidhi matarajio ya wadau, Mamlaka itaweka mikakati ya kuimarisha uwezo wa kupokea, kuchambua na kusambaza taarifa kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Aidha, Mamlaka itaweka mfumo wa kupokea taarifa kutoka kwa sekta zinazodhibitiwa ili kuzisimamia ipasavyo kwa kuzingatia uwazi ubora na viwango vya huduma vinavyotarajiwa na wadau wake (Mkataba wa huduma kwa mteja na kupata maoni)

  • Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha biashara nchini. Ili kufanikisha juhudi hizo, Mamlaka itaendelea kuandaa nyenzo za udhibiti zitakazovutia uwekezaji katika sekta zinazodhibitiwa.
  • Ili kukabiliana na upungufu wa uwekezaji katika sekta zinazodhibitiwa, EWURA itaongeza juhudi zake za kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPs).
  • Masuala ya rasilimali watu ikiwa ni pamoja na ustawi wa wafanyakazi, ushirikishwaji, kuendana na utamaduni wa taasisi, uhuishwaji wa nyenzo za kazi,ajira, kudumisha wafanyakazi, uboreshaji wa mazingira ya kazi, ni muhimu ili kuhakikisha Mamlaka ina uwezo wa kutekeleza majukumu kwa kasi na ubora unaokubalika.
  • Uwezo wa kifedha wa Mamlaka ni eneo muhimu la kipaumbele katika Mpango Mkakati huu kwa sababu, kadiri shughuli za EWURA zinavyopanuka, mahitaji ya kifedha yanakuwa muhimu zaidi, hivyo, Mamlaka inapaswa kuwa na uchumi usioyumba kama inavyoelezwa katika Sheria ya Mamlaka (the EWURA Act, Cap 414)
  • Umma unapaswa kujua na kushiriki katika mchakato wa udhibiti wa sekta za nishati na maji. Utoaji elimu na ushajiishaji kwa umma utaendelea kutekelezwa katika Mpango Mkakati huu.

Hits: 269