Sekta ndogo ya Petroli

Petroli | Miundombinu ya petroli | Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi | Nyenzo za udhibiti | Upangaji wa bei za bidhaa za petroli | Taarifa za utendaji | Ufuatiliaji wa Utekelezaji Sekta ya Mafuta | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Taarifa za jumla

EWURA, katika kutekeleza majukumu na kazi zake kwenye sekta ndogo ya petroli, inawajibika kuzingatia Sheria ya EWURA Sura ya 414 na Sheria ya Petroli, Sura ya 392. Chini ya Sheria hizi, Mamlaka ina jukumu la kudhibiti kiufundi na kiuchumi mkondo wa kati na wa chini wa sekta ndogo ya petroli kwa Tanzania Bara. Lengo kuu la udhibiti ni kulinda maslahi ya walaji, wauzaji bidhaa za mafuta na serikali, ambao kwa pamoja ni wadau wakuu wa EWURA. Kazi za udhibiti zinazotekelezwa na Mamlaka katika sekta hii zinalenga: – kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa za petroli nchini;

  1. kuweka gharama stahiki katika ununuzi, uhifadhi, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa za petroli;
  2. kuvutia uwekezaji kupitia utoaji wa leseni katika shughuli za petroli hivyo, kusaidia uhakika wa huduma na usambazaji wa bidhaa za petroli nchini kote;
  3. kuweka mazingira sawia ya kibiashara ili kulinda maslahi ya watoa huduma au wasambazaji wa bidhaa za petroli; na,
  4. kutekeleza sera za serikali kama ilivyoainishwa katika Sera ya Nishati.

 

Views: 3828