Petroli | Miundombinu ya petroli | Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi | Nyenzo za udhibiti | Upangaji wa bei za bidhaa za petroli | Taarifa za utendaji | Ufuatiliaji wa Utekelezaji Sekta ya Mafuta | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro
Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi
Vibali vya ujenzi
EWURA ina jukumu la kutoa idhini ya ujenzi kwa ajili ya biashara yoyote inayohusika na mkondo wa kati na wa chini wa sekta ndogo ya mafuta. Mtu yeyote anayekusudia kuwekeza katika sekta ya mafuta anapaswa kutuma maombi EWURA ili kupata kibali. Wakati wa kutoa kibali cha ujenzi, EWURA huzingatia masuala ya kiufundi, mazingira, afya na usalama.
Mambi ya kibali cha ujenzi hufanyika kupitia mfumo wa kieletroni ujulikanao kama Licencse and Order Information System (LOIS). Mwombaji anatakiwa kutuma kwenye mfumo nyaraka muhimu kama ilivyoelezwa katika mwongozo kwa waombaji wa leseni za petroli na idhini ya ujenzi.
Ikumbukwe kwamba, kibali cha ujenzi si leseni. Baada ya kukamilika ujenzi wa kituo cha mafuta, mwombaji anapaswa kuomba leseni ya uendeshaji wa kituo cha mafuta kupitia LOIS. Mchakato wa kutoa leseni ya bidhaa za petroli huanza pale mwombaji anapotuma maombi kamili kwenye mfumo.
Aina za leseni
Zifuatazo ni aina za leseni za mafuta zinazotolewa na EWURA:-
- Leseni ya jumla bidhaa za petroli;
- Leseni ya uhifadhi wa bidhaa za petroli;
- Leseni ya rejareja ya bidhaa za petroli;
- Leseni ya bidhaa za petroli kwa matumizi binafsi;;
- Leseni ya jumla ya LPG;
- Leseni ya usambazaji wa LPG;
- Leseni ya uchanganyaji wa vilainishi;
- Leseni ya jumla ya vilainishi;
- Leseni ya usambazaji wa Vilainishi;
- Leseni ya Uratibu wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA);
- Leseni ya usimamizi wa upakiaji na upakuaji wa bidhaa za petroli majini;
- Leseni ya uendeshaji wa kiwanda cha kusafisha bidhaa za petroli;
- Leseni ya urejelezi bidhaa za petroli;
- Leseni ya uendeshaji wa bomba la bidhaa za petroli;
- Leseni ya jumla ya lami; na,
- Leseni ya jumla ya Petcoke.
Mwongozo wa maombi ya leseni na vibali vya ujenzi
Baada ya kuwasilisha maombi yaliyokamilika, Mamlaka hufanya yafuatayo: –
- Kutangaza maombi ya leseni kwenye gazeti ili kupata maoni ya umma endapo wanaridhia maombi hayo ama la;
- Ukaguzi wa awali wa kituo ili kujiridhisha endapo vigezo na masharti vimezingatiwa;
- Kuandaa ripoti ya tathmini ya maombi na kuiwasilisha katika vikao vya Bodi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa kupewa leseni ama la; na,
- Mwombaji atajulishwa kuhusu uamuzi wa Bodi.
EWURA itatoa leseni ndani ya siku 60 tangu tarehe ya kupokea maombi yaliyokamilika iwapo, itaridhika kwamba, masharti yote ya leseni yamezingatiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 133 (1) cha Sheria ya Petroli, Sura ya 392.
Orodha ya leseni ni kama inavyoonyeshwa: –
- Orodha ya Wauzaji wa jumla wa Bidhaa za Petroli
- Orodha ya Vituo vya Mafuta vyenye leseni ya Uendeshaji
- Orodha ya Wauzaji wa Jumla wa LPG
- Orodha ya Wauzaji wa Jumla wa Vilainishi
Views: 1173