Nyenzo za udhibiti

Petroli | Miundombinu ya petroli | Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi | Nyenzo za udhibiti | Upangaji wa bei za bidhaa za petroli | Taarifa za utendaji | Ufuatiliaji wa Utekelezaji Sekta ya Mafuta | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Nyenzo za Udhibiti

Uanzishwaji wa EWURA na kazi zake, umebainishwa katika Sera na Sheria mbalimbali zinazoipa uwezo Mamlaka kutekeleza majukumu yake ya udhibiti wa mkondo wa kati na wa chini wa sekta ndogo ya petroli kwa ufanisi. Yafuatayo ni maelezo ya kina (utondoti) ya sera, sheria, kanuni na viwango vya ubora.

Sera ya Taifa ya Nishati ya 2015

Sera ya Taifa ya Nishati, 2015 ni muungano wa sera mbalimbali za nishati ambazo ni: Sera ya Petroli, Sera ya Ushirikishwaji wa Nchi, Sera ya Gesi Asilia, Sera ya Nishati Jadidifu, na Sera ya Taifa ya Nishati ya 2003. Lengo kuu la kuunganisha sera za sekta ya nishati ni kurahisisha usimamizi wake na kuboresha utawala na utendaji.

Sera inatoa mwelekeo sahihi wa maendeleo ya sekta hii kwa ujumla,kwa lengo la kuanzisha huduma bora, ununuzi, usafirishaji na usambazaji wa nishati kwa njia inayojali mazingira. Sera ya Taifa ya Nishati imewezesha kuwepo mfumo thabiti wa kisheria, kiudhibiti na muundo wa kitaasisi kwa ajili ya sekta ndogo ya Petroli.

Sheria

Mfumo wa kisheria wa sekta ndogo ya mafuta, umegawanywa katika maeneo mawili ambayo ni sheria kuu na sheria ndogo. Sheria kuu ni Sheria zilizotungwa na Bunge ambapo sheria ndogo ni Kanuni zilizotungwa na Waziri mwenye dhamana ya Petroli na Kanuni zinazotungwa na Mamlaka.

Sheria kuu za sekta ndogo ya petroli ni:-

Kanuni ndogo za sekta ya petroli ni:-

Kanuni za sekta ya petroli ni:

Viwango vya ubora vya bidhaa za petroli

Mamlaka huhakikisha kwamba, bidhaa za petroli na miundombinu yake vinazingatia viwango vya ubora. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lina jukumu la kuandaa na kupitia viwango vya bidhaa za petroli na miundombinu, ambapo, EWURA ni mdau mkuu katika suala hili. Viwango vikishaidhinishwa, EWURA huhakikisha waendeshaji wa shughuli za mkondo wa kati na wa chini wa sekta ya petroli, wanazingatia viwango vinavyopatikana kupitia tovuti ya TBS.

Viwango vinavyotumika katika bidhaa za petroli ni:-

  1. TZS 647:2014 Engine Oils – Minimum Performance – Specification
  2. TZS1068 (9):2008/ISO 6743-9 Lubricants, Industrial Oils and related products (Class I) Classification – Part 9: Family X (Greases)
  3. TZS 672: 2012 (4th Ed) EAS 158: 2012, ICS: 75.160.20: Automotive gasoline (premium motor spirit) – specification;
  4. TZS 674: 2012 (2nd Ed) EAS 177: 2012, ICS 75.160.20: Automotive gas oil (automotive diesel) – Specifications;
  5. TZS 673: 2016(2nd Ed) – Fuel oil specifications;
  6. TZS 666: 2017 (2nd Ed)– Aviation Turbine Fuel (Jet-A1) Specifications;
  7. TZS 1099: 2017 (2nd Ed) – Automotive Biodiesel fuel specifications;
  8. TZS 1074: 2009 (1st Ed) -ISO 12922: 1999 – Lubricants, industrial oils and related products (class L)- Family H (hydraulic systems) Specifications for categories HFAE, HFAS. HFB, HFC, HFDR AND HFDU;
  9. TZS 1073: 2018(2nd Ed) -ISO 15380: 2002 – Lubricants, industrial oils and related products (class L)-Family H (Hydraulic systems- Specification for categories HETG, HEPG HEES and HEPR;
  10. TZS 1066(Part 99): 2009 (1st Ed)- ISO 6743-99: 2002 – Lubricants, industrial oils and related products (class L) — Classification —General;
  11. TZS 675: 2018 (4th Ed) – Multipurpose automotive gear lubricants (EP) ― Specification;
  12. TZS 667: 2018 (2nd Ed) – Motor vehicle brake fluids – Specification;
  13. TZS 580: 2017 (3th Ed) – Illuminating kerosene – Specification;
  14. TZS 818: 2004 (1st Ed) – Liquefied petroleum gases (LPG) – Specification; and
  15. TZS 798: 2017(2nd Ed) – Automotive service greases – Specification.

Viwango vya ujenzi wa vituo vya mafuta ni: –

  1. TZS 1076: 2009 (1st Ed) – Selection, specification, installation, operation and maintenance of automatic liquid level and temperature measuring instruments on petroleum storage tanks;
  2. TZS 1113:2009 (1st Ed) – Depots for the storage of petroleum products;
  3. TZS 1115: 2009 (1st Ed) – Petroleum Products Retail Outlets;
  4. TZS1114:2015 (2nd Ed) – Road transport vehicles, containers and equipment used for the transportation of dangerous petroleum products;
  5. TZS 1079: 2009 (1st Ed) – Installation of underground storage tanks, pumps/ dispensers and pipework at service stations and consumer installation; and
  6. TZS 1007:2008 (1st Ed) – Code of practice for cleaning of the petroleum storage tanks and disposal of sludge.

Visits: 195