Taarifa za jumla | Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Nyenzo za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Utoaji wa leseni | Viwango vya bei na tozo | Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira | Ripoti za Utendaji wa Mamlaka za Maji | Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira
Taarifa za Jumla
Kifungu Na. 28 cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira 2019 na Sheria ya EWURA Cap 414 vimeipa wajibu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kudhibiti kiufundi na kiuchumi huduma za maji na usafi wa mazingira nchini Tanzania ili kulinda wadau; kuhakikisha uendelevu wa ustawi wa kifedha kwa watoa huduma kwa ajili ya Kuhimiza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa makundi yote ikiwamo wenye vipato vya chini, na makundi maalumu. Katika kufikia malengo haya, EWURA pamoja na mambo mengine, inafanya; Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni; Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma; Kudurusu na kusimamia bei za huduma. Pia EWURA inafanya mapitio ya mipango biashara, na mikataba ya huduma kwa wateja na kuhimiza ushindani wenye tija na ufanisi kiuchumi;
EWURA inazidhibiti takribani mamlaka 85 za maji na usafi wa mazingira ambazo zinahudumia mikoa na makao makuu ya wilaya, miji na miradi ya kitaifa, kama ilivyoonyeshwa kwenye orodha ya mamlaka zinazodhibitiwa hadi kufikia Juni 2023; kama ilivyotangazwa na Waziri mwenye dhamana ya maji kama inavyoainishwa: –
Orodha ya Mamlaka Zinazodhitiwa na EWURA
Aina ya Mtoa huduma Idadi ya Watoa huduma
- Mamlaka za Mikoa 26
- Mamlaka za Miradi ya Maji ya Kitaifa 7
- Mamlaka za Wilaya na Miji Midogo 52
Jumla ya Mamlaka 85
Miundombinu
Uwezo wa Uzalishaji maji na mahitaji ya huduma ya maji
Kiwango cha uzalishaji majisafi kwa Mamlaka za mikoa na miradi ya kitaifa kwa mwaka 2021/22, kilifikia mita za ujazo milioni 356, ilhali uwezo wa uzalishaji ulifikia mita za ujazo milioni 554, na mahitaji yakiwa mita za ujazo milioni 682. Kwa Mamlaka za Wilaya na Miji Midogo, mwaka 2021/22, kiwango cha uzalishaji wa maji kilifikia mita za ujazo milioni 37.2, wakati mahitaji yalikuwa mita za ujazo milioni 105.5.
Views: 1404