Taarifa za jumla | Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Nyenzo za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Utoaji wa leseni | Viwango vya bei na tozo | Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira | Ripoti za Utendaji wa Mamlaka za Maji | Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira
Utekelezaji wa Miongozo
Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira
Mamlaka za maji zinatakiwa kuhakikisha kwamba maji yanayotolewa na namna ambavyo maji taka yanashughulikiwa ni kwa mujibu wa viwango vilivyoidhinishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Zaidi ya hayo, Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira zinawajibika kufanya ukaguzi wa athari ya kimazingira kwa miradi iliyokamilika na kupewa cheti kutoka Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Utelekezaji wa Maelekezo
Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira zinapaswa kufuata na kutii maelekezo yaliyotolewa wakati wa kaguzi mbalimbali zilizofanyika katika maeneo yao, kutekeleza Mkataba wa Huduma kwa Mteja, kufikia malengo yaliyoainishwa katika Mipango Biashara, kutekeleza maelekezo yaliyotolewa kwenye Taarifa ya Mwaka ya Utendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira
Views: 70