Utoaji wa leseni kwa Mamlaka za Maji

Taarifa za jumla | Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Nyenzo za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Utoaji wa leseni | Viwango vya bei na tozo  | Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira | Ripoti za Utendaji wa Mamlaka za Maji | Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Utoaji wa leseni

Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, sura ya 414 inaipa EWURA wajibu wa kutoa, kuhuisha, na kufuta leseni za watoa huduma zinazodhibitiwa. Watoa huduma wenye leseni na wale wanaotarajiwa kuomba leseni wanaweza kutuma maombi ya leseni EWURA kwa ajili ya leseni mpya au uhuishaji. EWURA inayachambua maombi na kuamua kutoa au kutokutoa leseni kwa utaratibu usio na upendeleo kwa mujibu wa sheria.

Mamlaka zenye leseni

Ni lazima kwa mamlaka zinazotoa huduma za maji na usafi wa mazingira kuwa na leseni ya EWURA. Leseni zinazotolewa na EWURA zimewekwa kwenye daraja tatu, ambayo ni Daraja ya I, Daraja ya II na Daraja ya III. Vigezo vya kila daraja vimeanishwa kama ifuatavyo: –

DARAJA YA I: Leseni hizi hutolewa kwa mwombaji mwenye uwezo wa kifedha, kiufundi na menejimenti katika kuendesha shirika na hukidhi gharama zote za uendeshaji.

DARAJA YA II: Leseni hizi hutolewa kwa mwombaji mwenye uwezo wa kiufundi na menejimenti katika uendeshaji wa shirika na hukidhi gharama za uendeshaji, isipokuwa sehemu ya gharama za uwekezaji.

DARAJA YA III: Leseni hizi hutolewa kwa mwombaji anayetegemea msaada wa kifedha, kiufundi na menejimenti kutoka serikalini na kwa kiasi fulani hukidhi gharama za uendeshaji.

Mamlaka za Maji kwenye daraja ya II na III zinapaswa kuboresha utendaji wao kwa mujibu wa vigezo ili ziweze kupandishwa daraja.

Utaratbu wa kutoa leseni

Utaratibu wa kutoa leseni umefafanuliwa kwenye Kanuni za Maji na Usafi wa Mazingira, GN 387, (2011). Waombaji wanatakiwa kujaza fomu za maombi Form 400 – na kuzituma EWURA kwa ajili ya uchambuzi na utoaji leseni.

Utaratibu wa kutoa leseni

Utaratibu wa kutoa leseni umefafanuliwa kwenye Kanuni za Maji na Usafi wa Mazingira, GN 849, (2020). Waombaji wanatakiwa kujaza fomu za maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa maombi ya leseni (LOIS) na kuzituma EWURA kwa ajili ya uchambuzi na utoaji leseni.

Leseni zilizotolewa

EWURA imetoa leseni kwa mamlaka za maji na usafi wa mazingira za miaka kumi kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali.

  1. Idadi ya Leseni daraja la kwanza (Class I) 2
  2. Idadi ya Leseni daraja la Pili (Class II) 6
  3. Idadi ya Leseni daraja la Tatu (Class III) 77

Visits: 112