Udhibiti wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira

Taarifa za jumla | Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Nyenzo za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Utoaji wa leseniViwango vya bei na tozo  | Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira | Ripoti za Utendaji wa Mamlaka za Maji | Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira

Udhibiti wa huduma za Maji na Usafi wa Mazingira una umuhimu wa kipekee, hasa kwa sababu mamlaka za maji zinahodhi biashara hii pasipo ushindani. Kwa namna nyingine, kukosekana kwa ushindani kungesababisha huduma zinazotolewa na mamlaka hizi kuwa duni.

EWURA inadhibiti huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira kwenye maeneo ya miji. Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira inaweza kutoa huduma zake moja kwa moja kwa wateja au kupitia mtoa huduma mwingine kwa makubaliano ya kimkataba.

Udhibiti wa kiufundi

Udhibiti wa kiufundi ni pamoja na usimamizi wa viwango vya ubora, kanuni za utendaji na masuala ya afya, usalama na mazingira (HSE). Katika kutimiza jukumu la kufuatilia huduma za maji safi na majitaka, EWURA imeandaa mwongozo (Water and Wastewater Quality Monitoring Guidelines 2020), ili kuzisaidia mamlaka za maji kupanga na kufuatilia ubora wa maji safi na majitaka.

Udhibiti wa Kiuchumi

Udhibiti wa Kiuchumi unajumuisha

  • Kudhibiti viwango vya uwekezaji, na
  • kuchambua na kuidhinisha mipango ya biashara ya mamlaka za maji pamoja na kupanga viwango na tozo.

EWURA imeandaa miongozo ili kusaidia upitiaji wa viwango, bei na tozo mbalimbali kwa uwazi na kwa namna inayotabirika. Miongozo inayotumika kuidhinisha viwango, bei na tozo hizo, bofya (EWURA Water Tariff Application and Rate Setting Rules 2020 na Guidelines for preparing a Business Plan for Water Supply and Sanitation Authorities, 2022)

Visits: 106