Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Taarifa za jumla | Shughuli za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Nyenzo za Udhibiti wa Maji na Usafi wa Mazingira | Utoaji wa leseniViwango vya bei na tozo  | Masuala ya Afya, Usalama na Mazingira | Ripoti za Utendaji wa Mamlaka za Maji | Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Utatuzi wa Malalamiko yanayohusu Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Kifungu cha 34 cha Sheria ya EWURA Sura ya 414 kinaitaka Mamlaka kushughulikia malalamiko dhidi ya mtoa huduma zinazodhibitiwa kwa  suala lolote linalohusu usambazaji, uwezekano wa kusambaza huduma au mapendekezo ya usambazaji wa huduma.

Utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya watumiaji unazingatia:-

  1. Ulinzi wa Mtumiaji huduma- Haja ya watoa huduma kutoa huduma za uhakika, unafuu na zenye ubora;
  2. Kupendelea kutumia utaratibu wa usuluhishi wa malalamiko dhidi ya utaratibu wa madai;
  3. Kuweka utaratibu wa kushughulikia malalamiko kwa haraka zaidi, unaozingatia na usio na urasimu.

Nani anaweza kuwasilisha malalamiko?

  1. Mtu yeyote (mtumiaji wa huduma zinazodhibitiwa);
  2. Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma zinazodhitiwa na EWURA (EWURA CCC) au mwakilishi aliyeidhinishwa na upande unaolalamika;
  3. Kikundi cha watu- kinaweza kuwasilisha malalamiko kwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:-
  • Orodha ya majina na saini;
  • Muhtasari wa mkutano wa kikundi unaoonyesha azimio la kuwasilisha malalamiko; na,
  • Jina au majina ya mwakilishi/wawakilishi na mawasiliano yao.

Mamlaka inazo Kanuni za Utatuzi wa Malalamiko ya Watumiaji ambazo huzitumia katika kushughulikia malalamiko. Ili kumfanya mtoa huduma kuwajibika, malalamiko yanapaswa kuripotiwa ndani ya muda ulioanishwa. Ukomo wa muda hutegemea aina ya malalamiko. Malalamiko yatakayowasilishwa baada ya kikomo cha muda hayatazingatiwa, kwa hivyo watumiaji huishia kupoteza haki zao za huduma bora au bidhaa. Sababu kubwa ya kuweka ukomo wa muda ni kuwezesha Mamlaka kufanya kazi kwa wakati, kukusanya ushahidi, ambao utasaidia katika kutatua suala hilo kwa uadilifu.

Asili ya Kipindi cha Malalamiko ya Kikomo Kikomo cha Muda wa Kuwasilisha Malalamiko
Kukatishwa kwa huduma kinyume cha sheria miezi kumi na mbili
Bili isiyofaa miezi kumi na miwili
Kushindwa au kukataa kuunganisha huduma miezi kumi na mbili
Ubora duni wa huduma kwa miezi ishirini na nne
Mengine miezi kumi na mbili

Visits: 146