Kituo cha Taarifa

Kituo cha Taarifa

kifungu cha 6 (e) cha Sheria ya EWURA (the EWURA Act, Cap 414), kinaeleza kuwa, ni wajibu wa Mamlaka kutoa elimu kwa umma, kukuza ufahamu na uelewa wa sekta zinazodhibitiwa, kuhusu haki na wajibu, kazi na majukumu ya Mamlaka na njia zitakazotutumika kutatua migogoro itakayotokea kutokana na huduma zinazodhitibiwa.

Ili kuwianisha matarajio ya umma, mkakati sahihi wa mawasiliano ni muhimu, hasa ikizingatiwa kuwa, miongoni mwa majukumu ya Mamlaka ni kutoa elimu na kuimarisha uelewa kuhusu sekta zinazodhibitiwa.

Kwa hiyo, kituo hiki ni kitovu cha taarifa kuhusu udhibiti wa sekta za Umeme, Petroli, Gesi Asilia na Maji na Usafi wa Mazingira.

 

Views: 327