Leseni na Usajili Umeme

Umeme | Miundombinu ya Umeme | Leseni na Usajili| Nyenzo za udhibiti | Mikataba ya Ununuzi wa Umeme | Utii (Ufuasi) wa Sheria| Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Leseni na Usajili

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131, kinaipa nguvu Mamlaka kutoa leseni kwa taasisi zinazofanya kazi au zinazotaka kufanya shughuli za umeme.

Aidha, kifungu cha 8 cha Sheria hiyo, kinaeleza kuwa mtu yeyote mwenye nia ya kuzalisha, kusafirisha, kufunga mifumo au kufanya biashara ya umeme na nchi nyingine, atalazimika kuomba leseni isipokuwa kama mtu huyo, amesamehewa au shughuli hiyo imesamehewa na mamlaka kwa mujibu wa kifungu cha 18 (3 au 4) cha Sheria ya Umeme.

 

Kifungu cha 37 cha Kanuni za Umeme (the Electricity Development of Small Power Projects) Rules 2020) na Notisi ya Serikali Na. 491; inawataka wazalishaji na wasambazaji wadogo wa umeme au wazalishaji wadogowadogo kuwa na leseni ya kuendesha miradi hiyo au kusajiliwa na mamlaka kabla ya kuanza kuendesha biashara ya umeme. Leseni hutolewa kwa shughuli zenye uwezo wa kuzalisha umeme zaidi ya Megawati  moja (1) na usajili hufanyika kwa uzalishaji umeme chini ya Megawati  moja (1).

 

(a) Maombi ya leseni

Maombi ya leseni au usajili hufanyika kupitia mfumo wa kieletroni kwa kubofya LOIS (Licence and Order Information System) katika Tovuti ya Mamlaka www.ewura.go.tz. Ufuatao ni soma mwongozo wa kuomba leseni za umeme wa Julai 2021.

(b) Watoa Huduma wenye Leseni

Ifuatayo ni orodha ya watoa huduma za umeme waliopewa leseni na mamlaka (Licensed Service Providers)

 

(c) Wataalamu wa Ufungaji Mifumo ya Umeme.

Ifuatayo ni orodha ya Mafundi umeme waliopewa leseni za usakinishaji wa umeme (Licensed Electrical Installation Personnel)

(d) Watoa Huduma Waliosajiliwa

Ifuatayo ni orodha ya watoa huduma za umeme waliosajiliwa na mamlaka (Registered Service Providers)

 

(e) Leseni zilizofutwa

Ifuatayo ni orodha ya leseni zilizofutwa na mamlaka (Revoked Licences)

Visits: 6467