Miundombinu ya Umeme

Umeme | Miundombinu ya Umeme | Leseni na UsajiliNyenzo za udhibiti | Mikataba ya Ununuzi wa Umeme | Utii (Ufuasi) wa Sheria| Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Miundombinu ya Umeme

EWURA inadhibiti sekta ya umeme Tanzania Bara ambayo kwa sehemu kubwa huduma hutolewa na  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nchini sanjari na kuuza kwa nchi jirani. Pamoja na TANESCO, zipo kampuni nyingine sita (6) zenye leseni za uzalishaji wa umeme kwa ajili ya kuuza.Pia zipo kampuni 13 zenye leseni za kuzalisha umeme kwa matumizi binafsi.

Aidha, zipo kampuni tatu (3) zilizosajiliwa kuzalisha umeme kwa kutumia maji na kuiuzia TANESCO; kampuni nyingine sita (6) zimesajiliwa) kuzalisha umeme wa sola chini ya megawati moja (1) ili kuuza katika maeneo yasiyo na Gridi ya Taifa. Pia, zipo kampuni mbili (2) zilizosajiliwa) kuzalisha umeme kwa matumizi binafsi.

 

(a) Uzalishaji

EWURA husimamia shughuli za uzalishaji umeme, ambapo hadi Juni 2021, jumla ya Megawati 1,608.46 zilizalishwa. Mauzo yalikuwa ni Megawati 1,573.65 kutoka Gridi ya Taifa na Megawati 34.80 kutoka nje ya Gridi ya Taifa.

(b) Usafirishaji

Mtandao wa kusafirisha umeme unajumuisha njia zenye urefu wa kilometa 5,896 na vituo vidogo 58 vinavyomilikiwa na kuendeshwa na TANESCO. Msongo mkuu wa usafirishaji unajumuisha kilometa 670 zenye kilovoti 400; kilometa 3,011 zenye Kilovoti 220;kilometa 1,672.57 zenye Kilovoti 132 na kilometa 543 zenye Kilovoti 66.

 

(c) Usambazaji

Mtandao wa usambazaji umeme kwa kampuni zilizopewa leseni una jumla ya kilometa 139,513.86; kati ya hizo, kilometa 139,092.86 ni za TANESCO na kilometa 421.00 za kampuni ya Mwenga. Aidha, upo mtandao wa usambazaji umeme wenye kilometa 447.7 kwa kampuni zilizosajiliwa na EWURA

Views: 951