Upangaji wa bei za bidhaa za petroli

Petroli | Miundombinu ya petroli | Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi | Nyenzo za udhibiti | Upangaji wa bei za bidhaa za petroli | Taarifa za utendaji | Ufuatiliaji wa Utekelezaji Sekta ya Mafuta | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Upangaji wa bei za bidhaa za petroli

Bei Elekezi

Kila mwezi, EWURA huchapisha bei za jumla na rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa matumizi ya ndani. Bei hizo, kwa mikoa yote, hukokotolewa kutokana na majumuisho ya gharama mbalimbali kwenye ghala za mikoa ya Dar es Salaam, Tanga au Mtwara.

Mamlaka hutekeleza jukumu hili, kwa mujibu wa Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei za Mafuta ya mwaka 2009 na marekebisho yake.

Currently, the cap prices are published on monthly basis. EWURA started to publish cap prices in January 2009.

Mamlaka ilianza kuchapisha bei elekezi tarehe 6 Januari 2009. Mamlaka huchapisha bei elekezi za mafuta yanayouzwa kwa rejareja katika mikoa, wilaya na miji yote nchini. Wafanyabiashara wote hawaruhusiwi kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu ya bei elekezi.

Vituo vyote vya mafuta vinapaswa kutangaza bei ya bidhaa zao kwenye mabango katika maeneo yaliowazi na yenye kuonekana kwa urahisi. Uuzaji mafuta kwa bei inayozidi bei elekezi na kwa kutokutangaza bei za mafuta kwenye mabango yalio wazi na yenye kuonekana kwa urahisi mbele ya vituo vya mafuta ni kosa kisheria. Vitendo hivyo vitasababisha adhabu kutoka EWURA.

Piga *152*00 kupata bei elekezi ya rejareja zilizochapishwa bila gharama yoyote kwa maeneo yote.

Uagizaji mafuta wa pamoja

Kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Petroli, sura 392, uagizaji wa mafuta nchini unapaswa kufanyika kwa mfumo wenye tija, utakao ainishwa na waziri mwenye dhamana ya masuala ya mafuta. Kupitia kifungu hiki, Kanuni za Uagizaji Mafuta kwa Pamoja ziliandaliwa na Waziri mwenye dhamana ya petroli mwaka 2011 ambazo zilifanikisha kuundwa kwa taasisi itakayo shughulikia jukumu hilo ikiitwa PIC-(Petroleum Importation Coordinator)

Kwa sasa, mafuta yanayoagizwa nchini kupitia mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja (BPS) ni petroli, dizeli, JET A1 na mafuta ya taa. Kama mdhibiti, EWURA huhakikisha kuwa mfumo huu unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni, hivyo nchi haipungukiwi bidhaa za mafuta ambazo ni muhimu kwa mustakabali wa ustawi wa uchumi.

Visits: 4765