Miundombinu ya Petroli

Petroli | Miundombinu ya petroli | Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi | Nyenzo za udhibiti | Upangaji wa bei za bidhaa za petroli | Taarifa za utendaji | Ufuatiliaji wa Utekelezaji Sekta ya Mafuta | Utatuzi wa Malalamiko na Migogoro

Miundombinu ya petroli

Miundombinu ya kushughulikia petroli ni pamoja na gati la kupokelea mafuta, maghala ya kuhifadhi, vyombo vya usafirishaji, vituo vya mafuta vya rejareja na vya matumizi binafsi.

Miundombinu ya kupokelea bidhaa za petroli

Miundombinu inayotumika kupokelea meli zinazoleta bidhaa za petroli ipo katika bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Bandari ya Mtwara ilianza kupokea bidhaa za petroli Julai 2018; na kuwa bandari ya tatu kwa Tanzania Bara baada ya bandari ya Dar es Salaam na Tanga. Bandari ya Mtwara inahudumia mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Bandari ya Tanga inahudumia Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara wakati Bandari ya Dar es Salaam inahudumia mikoa mingineyo pamoja na nchi jirani. Bofya hapa kuona kiwango cha juu cha uwezo wa kufanya kazi kwa usalama na bidhaa zinazopokewa kwenye gati ya kila bandari.

Ghala za kuhifadhi bidhaa za petroli

Tanzania Bara ina ghala 22 za kupokelea mafuta zilizopo katika bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, zenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 1,288,101. Ghala hizi hupokea bidhaa za petroli kutoka melini. Aidha, kuna ghala 29 nchi kavu, zenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 75,625. Hata hivyo, ghala hizo, nyingi hazifanyi kazi. Pia, Kampuni ya Bomba la Mafuta la TAZAMA inapokea mafuta ghafi kupitia boya (SBM) na kuhifadhi bidhaa hizo kwenye ghala lake lenye mita za ujazo 232,000.

Miundombinu ya usafirishaji bidhaa za petroli

Duniani kote  zipo njia kuu nne za usafirishaji wa bidhaa za petroli ambazo ni bomba, reli, barabara na maji. Licha ya kuwapo njia mbalimbali za usafirisahaji, kwa sasa, Tanzania Bara, barabara inategemewa zaidi kuwa ndiyo njia kuu ya kusafirisha bidhaa za petroli. Malori hutumika kusafirishia bidhaa za petroli kutoka kwenye maghala ya kupokelea (Dar es Salaam, Tanga na Mtwara) kwenda kwa watumiaji nchini kote na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, DR Congo na Uganda.

Aidha, lipo bomba la TAZAMA linalosafirisha mafuta ghafi kutoka Kigamboni, Dar es Salaam hadi Ndola, Zambia.

Vituo vya mafuta

Vituo vya mafuta, ni sehemu ya mwisho kabla ya bidhaa za petroli kumfikia mteja. Hadi tarehe 31 March, 2022, kulikuwa na vituo 2,032 vinavyofanya kazi Tanzania Bara. Mwenendo unaonyesha kuwa uwekezaji katika vituo vya mafuta nchini kote unakua, kutokana na ongezeko la mahitaji ya mafuta

Vituo vya gesi ya kupikia inayotokana na  petroli (LPG)

Uwekezaji katika gesi ya kupikia itokanayo na petroli (LPG) unalenga kuhakikisha kuwa, gesi hiyo ambayo ni safi, inayozingatia kanuni za afya, mazingira na gharama nafuu ikilinganishwa na matumizi ya kuni, mkaa na mafuta ya taa, inapatikana kwa urahisi kwa watumiaji wa nyumbani.

Hadi kufikia 31 Machi 2022, kulikuwa na ghala (6) za kuhifadhi gesi ya kupikia yaliyopo.  Dar es Salaam na Tanga yenye uwezo wa kuhifadhi tani za ujazo 15,750. Pia, vipo vituo 33 vya kuhifadhi na kujazia gesi nchini, vyenye uwezo wa jumla ya tani za ujazo 1,671.

Visits: 265